Istiqaama Tanga ni shule ya mfano Tanzania.

Istiqaama Tanga Sec mbele

Na mwandishi wetu

Jumamosi 11 Novemba 2017

Pongezi nyingi zimetolewa kwa uongozi wa shule,walimu na wanafunzi wa shule ya kiislamu ya istiqaama

Mtiririko huo wa pongezi ulianzia kwa wazazi,wageni wengine waalikwa waliopata nafasi za kuzungumza na kuhitimishwa na mgeni rasmi kwenye hafla ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne kwa mwaka 2017.

Bi Mayasa Hashim ambaye ni afisa taaluma mkoa wa Tanga,alisema amevutiwa mno na shule ya istiqaama Tanga hasa katika maeneo matatu.Kwanza ni nidhamu na usafi wa hali ya juu ya wanafunzi wa shule hiyo,ambao alisema unaendana na usafi na mpangilio mzuri wa majengo ya shule hiyo.

Katika hafla hiyo iliyofanyika shuleni hapo mnamo tarehe 11 Novemba 2017,mwalimu Mayasa aliendelea kuisifia shule hiyo kwa kuweza kushika nafasi za juu kitaifa na kuongoza kimkoa na wilaya katika mitihani kadhaa iliyoshiriki kuifanya mpaka sasa.

Awali katika hafla hiyo,mwenyekiti wa bodi ya shule na katibu wa taasisi ya istiqaama  inayomiliki shule hiyo,sheikh Mohammed Said Albusaidy aliweka wazi baadhi ya mikakati iliyochukuliwa na shule hiyo hadi kufikia kiwango hicho cha mafanikio.

Sheikh Mohammed aliwashukuru sana wazee wa taasisi hiyo na viongozi wastaafu kwa kubeba majukumu mengi ya gharama za kuendesha shule hiyo.Pamoja na kwamba shule daima ina nakisi ya kibajeti kutokana na ada kuwa chini na kutokulipwa ada kwa wakati lakini bado shule hiyo imekuwa ikifanya matumizi ya lazima kwa wakati.

Katika risala yao,wanafunzi wa kidato cha nne walikabidhi malalamiko yao kwa mgeni rasmi ikiwa ni changamoto walizopambana nazo kipindi chote cha masomo.Kubwa katika hizo ni ukosefu wa maji safi ya kunywa kutokana na visima vya shule hiyo kutoa maji  magumu.

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo,mwalimu Mohammed alitaja tatizo la ukosefu wa mawasiliano ya uhakika shuleni hapo kutokana na mashirika ya simu kutokuwa na minara ya mawasiliano karibu yao.Sambamba na hilo pia alilalamikia suala la ukosefu wa kituo cha polisi jirani na shule ili kuimarisha usalama wa wanafunzi,walimu na mali za shule hiyo.

Pamoja na pongezi nyingi alizozitanguliza mgeni rasmi kwa shule ya Istiqaama,bi Mayasa aliahidi kuziwasilisha kero zote za shule kwa mamlaka husika za kiserikali ili kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Matangazo maalum ya kibiashara (nafasi hii inalipiwa)

زيت ارغان    Mafuta ya Arghani mafutayaarghani

Matoleo mapya ya kitabu kipendwacho cha Mkweli Mwaminifu yako tayari.Agizia mapema kutoka kwetu.

mkweli mwaminifu 

Suruali za kuvalia kanzu za kiume. na za kike

Zipo za ukubwa na rangi mbali mbali .Ni mali kutoka nchini Morocco.

Zinapatikana Kwa reja reja na kwa jumla .Ili Kujua zaidi wasiliana nasi hapa.

 

  SURUALI MOROCO      SURUALI MOROCCO

ZINDUKA

  • MKUU wa kitengo cha Habari na Malezi cha Chuo Kikuu cha al Mansoura nchini Misri amesema, kuzusha vita baina ya Waislamu kwa kutumia fitna ya kimadhehebu, yaani sunni na Kishia ndilo lengo kuu la Marekani katika njama zake za kuwarafakanisha Waislamu..Shirika la habari la Rasa limemnukuu Amin Said, akisema hayo mwishoni mwa mkutano uliopewa jina la Nafasi ya Vyombo vya Habari katika Kupambana na Ugaidi, ambao ulifanyika kwa lengo la kutafuta njia za kupambana na njama za Marekani.Annuur Na. 1220 JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA , MACHI 11-17, 2016

MWANGAZA KWA UMMA

Tofauti kati ya Tohara na kukeketa
Na Skh Mussa Kileo

Kila inapofika tarehe 6 Februari, Umoja wa Mataifa huadhimsha siku ya kupinga ukeketaji wa wanawake Duniani . Kwa wanaharakati wa Haki za binaadam na jinsia huiadhimisha siku hii kwa kauli mbiu mbalimbali na maazimio ya kushinikisha jamii ibadilike ili iachane na kuwakeketa wanawake.

Ukeketaji ni jambo lilioenea katika vinywa vya watu na kuandikwa na asasi mbali mbali za kijamii,na ipo haja kubwa kwa jamii ya kiislaam kulichambua jambo hili kwa kina,na ufafanuzi kama ifuatavyo:

Endelea