Masheikh piganieni Uchumi kuyapa nguvu mawaidha

Na Alhuda 
Mei 4 ,2017
Wito wa Mufti Mkuu wa Tanzania katika Baraza la Maulid kwamba Misikiti iwe na vitega uchumi unastahili kupewa uzito maalum na jamii ya Waislamu kwani Uchumi ni moja ya kanuni kuu mbili za kujenga, kustawisha na kuimarisha dini yao.
Uislamu unazitazama nafsi na mali kama rasilimali kuu za ustawi wake katika jamii. Kwa maneno mengine, amri ya kupigania Uislamu kwa mali na nafsi inatoa changamoto kwa Waislamu kujijenga kiimani na kiuchumi.
Udhaifu wa kimojawapo kati ya hivyo viwili katu hauwezi kuupa nguvu Uislamu. Imani tupu bila uchumi itawaacha Waumini wakiwa wanyonge mbele ya jamii nyingine, na uchumi tupu bila Imani utawaacha Waislamu wakiwa mateka wa dunia kama walivyo watu wa jamii nyingine walioghafilika.
Kwa sababu hizo, jitihada lazima zifanyike sanjari katika kujenga imani na uchumi wa jamii ya Waislamu. Miundombinu yote ya kujenga imani na dini inahitaji uchumi. Elimu, afya, maadili vyote vinahitaji uchumi.
Bila elimu, hakuna la maana linaloweza kufanyika katika imani na dini. Imani bila elimu haileti tija kubwa ya kijamii, na dini bila elimu haiendi popote. Hivyo, uchumi wa kujenga miundombinu ya elimu, ni muhimu.
Taasisi za elimu kuanzia Madrasa, chekechea, shule za awali, shule za msingi, sekondari na Vyuo vya elimu ya juu na Vyuo Vikuu ni hitajio kubwa la jamii ya Waislamu katika kujenga imani na dini yao.
Bila taasisi hizo, Uislamu utabaki zaidi katika nadharia kuliko uhalisia wa umbile lake kama mfumo pekee bora na sahihi wa maisha ya mwanadamu hapa ulimwenguni, na njia pekee ya mafanikio ya mwanadamu katika maisha ya Akhera.
Lazima jamii ya Waislamu iwe na taasisi bora za elimu katika ngazi zote hizo kama inataka kuupa nguvu, heshima na hadhi yake halisi Uislamu katika dunia ya leo. Lakini yote hayo hayawezekani bila uchumi.
Japo jitihada za kutafuta elimu zimefanyika kwa sura nyingi, na japo tayari jamii ina taasisi mbalimbali za elimu ambazo kila mtu anaweza kujiunganazo lakini kama jamii yenye dira lake la duniani na Akhera, Waislamu wanahitaji taasisi nyingi za mlengo wao ili kutimiza lengo la maisha yao hapa duniani.
Hivyo, dhana ya uchumi ina nafasi muhimu katika uhai wa dini ya Kiislamu kwani ndiyo injini inayoendesha taasisi muhimu za elimu na miundombinu yake. Si hivyo tu, bali Uislamu pia hustawi kimaadili. Bila maadili, umbile la Uislamu haliwezi kuchukua uhalisia wake.
Ujenzi wa maadili katika jamii huwa mgumu pale ambapo hali za wanajamii kiuchumi si nzuri. Watu ‘huitupa dini’ na ‘kujihalalishia’ maovu mbalimbali ili ‘kujinusuru’ kiuchumi.
Rushwa, ukahaba, utapeli, wizi, ujambazi, ni miongoini mwa kadhia ambazo zinashirikisha wanajamii wa Kiislamu. Walewale wanaoonekana na alama za sijida kwenye mapaji ya uso ndio hao hao, kwa namna moja au nyingine, wamo katika munkari wa aina moja au nyingine.
Kifamilia, hali ni tete zaidi kwani familia zimefungulia milango maasi ili kujikimu kimaisha. Taasisi ya ndoa imeadimika na nafasi yake imechukuliwa na uovu wa zinaa. Uovu huu umekuwa mkubwa kiasi cha kuonekana wa kawaida! Leo hii hakuna tofauti kati ya Waislamu na wasio Waislamu katika sura ya kimaadili.
Uislamu utabaki katika vazi la kanzu na kofia lakini hauwezi kustawi katika mazingira hayo ya uovu. Kwa kiasi kikubwa, kuyumba kiuchumi ndiko kunakosambaratisha maadili kifamilia na kijamii.
Hivyo basi, suala la kujenga uchumi mdogo, wa kati, na mkubwa linahitaji kipaumbele kikubwa kwa Waislamu kama wanataka kujinusuru kiimani. Mawaidha yanahitaji kwenda sanjari na nguvu za kiuchumi ili kuondosha maovu ya kijamii.
Inahitajika hata mifuko ya fedha ya kuimarisha taasisi ya ndoa ili msingi wa mahusiano ya kijinsi urudi katika uimara wake na hivyo, kurudisha muruwa wa kuzaa maadili sahihi.
Ni vema ajenda za Masheikh zikabeba vipaumbele vya kiuchumi ili nasaha zitekelezeke katika jamii. Mikutano ya Masheikh lazima iijadili jamii kwa ujumla wake.
Na iutazame uchumi kama ‘roho’ ya dini kinyume na mtazamo wa kudhani kuwa dini ni kutoa ‘mawaidha’ na kuyaacha hewani bila hatua za utekelezaji. Matokeo yake mawaidha yamepoteza nguvu na kubaki kama mazoea tu ya kupitishia muda.

Matangazo maalum ya kibiashara (nafasi hii inalipiwa)

زيت ارغان    Mafuta ya Arghani mafutayaarghani

Matoleo mapya ya kitabu kipendwacho cha Mkweli Mwaminifu yako tayari.Agizia mapema kutoka kwetu.

mkweli mwaminifu 

Suruali za kuvalia kanzu za kiume. na za kike

Zipo za ukubwa na rangi mbali mbali .Ni mali kutoka nchini Morocco.

Zinapatikana Kwa reja reja na kwa jumla .Ili Kujua zaidi wasiliana nasi hapa.

 

  SURUALI MOROCO      SURUALI MOROCCO

MWANGAZA KWA UMMA

Tofauti kati ya Tohara na kukeketa
Na Skh Mussa Kileo

Kila inapofika tarehe 6 Februari, Umoja wa Mataifa huadhimsha siku ya kupinga ukeketaji wa wanawake Duniani . Kwa wanaharakati wa Haki za binaadam na jinsia huiadhimisha siku hii kwa kauli mbiu mbalimbali na maazimio ya kushinikisha jamii ibadilike ili iachane na kuwakeketa wanawake.

Ukeketaji ni jambo lilioenea katika vinywa vya watu na kuandikwa na asasi mbali mbali za kijamii,na ipo haja kubwa kwa jamii ya kiislaam kulichambua jambo hili kwa kina,na ufafanuzi kama ifuatavyo:

Endelea