Uteuzi Jaji Mkuu, Rais katimiza Matarajio ya wengi

Na ALHUDA

Hatimaye Tanzania imepata Jaji Mkuu mpya. Ni Profesa Abdurahman Hamisi Juma ambaye awali alikaimu nafasi hiyo baada ya kustaafu kwa Jaji Othman Chande.
Kipindi kirefu cha kukaimu kilizusha maswali na mijadala huku baadhi wakidhani Rais amefanya jambo linalokinzana na Katiba na Sheria. Sio siri wengi walitilia shaka usahihi wa kuuacha Muhimili huu muhimu wa Dola mikononi mwa Kaimu Jaji Mkuu kwa kipindi kirefu!
Hata hivyo, Prof. Kagudi Paramagamba, Waziri wa Sheria, alitumia vema nafasi yake ya kuzungumza katika hafla ya kumwapisha Jaji Mkuu mpya kwa kutoa ufafanuzi na mifano juu ya Uhalali wa Jaji kukaimu nafasi ya Jaji Mkuu kwa kipindi kirefu.
Rais, kwa upande wake, alitia nyongeza ya ufafanuzi huo kwamba alihitaji kujiridhisha ili kupata mtu wa kukaa muda mrefu katika nafasi hiyo. Tunachukua fursa hii kumpongeza Rais kwa hatua hiyo muhimu.
Tunaamini Taifa sasa limepata Jaji Mkuu ambaye ametimiza vigezo alivyovihitaji Rais kwa mnasaba wa mapambano dhidi ya kadhia za rushwa na ufisadi ambazo zinahitaji hukumu za mashauri Mahakamani.
Prof. Jaji Abdurahman Juma sio tu ametimiza vigezo vya Rais bali pia ametimiza matarajio ya wananchi wakiwemo Majaji na wanasheria wenziwe. Kama ni malalamiko basi labda wengi walikuwa wakilalamika kwa nini Jaji huyu bobezi alikawia kuapishwa.
Majibu yaliyotolewa na Rais baada ya malalamiko hayo ya muda mrefu, bila shaka, yamejitosheleza. Kama ambavyo wengi walitarajia kuona hatimaye Prof. Juma anaapishwa kuwa Jaji Mkuu ndivyo alivyofanya Rais.
Kwa maneno mengine, wengi hawakutarajia kuwa baada ya Jaji Prof. Juma kukaimu nafasi hiyo, angeteuliwa mtu mwingine badala yake. Wasifu wa Uprofesa ambao haukuwahi kusikika katika kiti cha Ujaji Mkuu, huenda ndio uliowapa wengi imani kuwa huyu ni Jaji bobezi aliyekienea kiti cha Ujaji Mkuu.
Ni ukweli usiopingika kuwa  Prof. Juma amepata Ujaji Mkuu katika kipindi ambacho serikali imejitoa muhanga kuendesha mapambano dhidi ya ufisadi uliojichimbia na kuota mizizi nchini.
Ni wakati ambao nyuso za Mihimili yote mikuu zinapaswa kuondokana na aibu katika kushughulikia mashauri ya mapapa wa ufisadi na rushwa. Tanzania ilishawahi kuwa na mapambano ya aina hii katika awamu ya kwanza ya utawala wake ambapo Waziri Mkuu Edward Sokoine anakumbukwa kwa kujitoa kwake muhanga dhidi ya Wahujumu uchumi.
Hata hivyo, mapambano hayo yalikuwa magumu kisheria kwani kwa mujibu wa Jaji Mkuu wa wakati huo, hayati Francis Nyalali, nchi haikuwa na sheria ya kushughulikia baadhi ya hatua za serikali.
Huenda kwa Jaji Nyalali, jukumu lilikuwa zito kwa wakati wake. Hata hivyo, kwa kulipima na jukumu la sasa la Jaji Prof. Juma, jukumu hilo ni zito zaidi kwa kuzingatia ukweli kuwa Nchi sasa imeingia vitani dhidi ya kadhia za Kimataifa za ufisadi.
Serikali sasa haipambani na wahujumu uchumi wa ndani ya nchi tu kama ilivyokuwa mwanzoni mwa miaka ya 1980 bali inakabiliana na mikono ya kifisadi ya makampuni ya Kimataifa ambayo yanakuja nchini kwa mikataba ya kisheria.
Ndiyo kusema kuwa macho makali zaidi yanahitajika upande wa sheria ambao mabeberu wanaweza kuutumia kuhujumu rasilimali zetu. Ni changamoto kwamba Mahakama kama Muhimili wa Dola isikae kusubiri mashauri ya kushitakiana bali ishiriki kikamilifu katika michakato ya nchi kuingia mikataba mbalimbali.
Badala ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kushughulika peke yake na jukumu la kupitia mikataba ya Kimataifa ya kisheria baina ya serikali na Makampuni na taasisi za Kimataifa, Ofisi ya Jaji Mkuu nayo ishirikishwe kupitia mikataba hiyo kabla haijasainiwa.
Bila shaka, hilo litaipa wepesi Mahakama kushughulikia kadhia za ufisadi na, pengine, mara zote, ushindi unaweza kuwa wa serikali kulinganisha na sasa ambapo Serikali huburuzwa Mahakamani na wanyonyaji kwa uhakika kuwa Mahakama itawapa ushindi kwa misingi ya mikataba.
Kama Taifa limebaini udhaifu katika eneo la mikataba, basi ni wakati sasa kwa Ofisi ya Jaji Mkuu kuwa na kitengo chake cha kupitia Mikataba yote ya Kimataifa kabla ya kusainiwa.
Ni matumaini yetu kuwa chini ya Jaji Mkuu mpya, Prof. Abdurahman Juma, Mahakama itazidi kulisaidia Taifa bila kuathiri uhuru wake na urari wa mizani yake ya kuwatendea haki wateja wake wote

Matangazo maalum ya kibiashara (nafasi hii inalipiwa)

زيت ارغان    Mafuta ya Arghani mafutayaarghani

Matoleo mapya ya kitabu kipendwacho cha Mkweli Mwaminifu yako tayari.Agizia mapema kutoka kwetu.

mkweli mwaminifu 

Suruali za kuvalia kanzu za kiume. na za kike

Zipo za ukubwa na rangi mbali mbali .Ni mali kutoka nchini Morocco.

Zinapatikana Kwa reja reja na kwa jumla .Ili Kujua zaidi wasiliana nasi hapa.

 

  SURUALI MOROCO      SURUALI MOROCCO

MWANGAZA KWA UMMA

Tofauti kati ya Tohara na kukeketa
Na Skh Mussa Kileo

Kila inapofika tarehe 6 Februari, Umoja wa Mataifa huadhimsha siku ya kupinga ukeketaji wa wanawake Duniani . Kwa wanaharakati wa Haki za binaadam na jinsia huiadhimisha siku hii kwa kauli mbiu mbalimbali na maazimio ya kushinikisha jamii ibadilike ili iachane na kuwakeketa wanawake.

Ukeketaji ni jambo lilioenea katika vinywa vya watu na kuandikwa na asasi mbali mbali za kijamii,na ipo haja kubwa kwa jamii ya kiislaam kulichambua jambo hili kwa kina,na ufafanuzi kama ifuatavyo:

Endelea