MKASA WA ABUSHIRI BIN SALIM NA WAJERUMANI

  Falme ya Ujerumani ilijisimika rasmi kueneza na kuimarisha ukoloni katika Afrika Mashariki.   

Mnamo tarehe 1 Januari, 1891, bwana Julius von Soden, ambaye hapo awali alikuwa Gavana wa Kijerumani nchini Cameroon, aliteuliwa kuwa Gavana wa kwanza wa Koloni la Wajerumani la Afrika ya Mashariki.

VITA KATI YA WANANCHI NA WAJERUMANI (1891 – 98)

Baada ya kuwashinda Waarabu na wananchi wa mwambao katika vita ya mwaka 1888 – 89.  Wajerumani walipeleka majeshi madogo mawili kwenda kukomesha upinzani wa Wasitu na Wahehe dhidi ya utawala wao wa kikoloni.  Majeshi hayo ya Wajerumani yalishindwa vibaya sana.  Wakati Meja Hermann von Wissmann alipojiuzulu katika kazi yake ya kuongoza majeshi katika Koloni la Wajerumani la Afrika ya Mashariki.  Luteni Hauptmann Emil von Zelewsky alishika cheo hicho na akaamua kuanzisha vita dhidi ya Wahehe ambao walikataa kutawaliwa na Wajerumani

Hivyo mnamo mwezi Juni, 1891, jeshi la Wajerumani lenye askari wapatao 1,000 chini ya uongozi wa Luteni Hauptmann Emil von Zelewsky mwenyewe, lilifunga safari kuelekea Iringa likitokea Kilwa.  Mutwa (mtemi) Mkwawa, aliyekuwa mtu mwerevu sana katika mambo ya vita, alipeleka wapelelezi wake kila mahali alipata habari zote adui zake mapema kabla hawajaingia nchi ya Uhehe. Hivyo mnamo tarehe 16 Agosti, 1891 wakati jeshi la Zelewsky lilipofika Lugalo katika njia itokayo Kilosa kwenda Mahenge, lilishambuliwa kwa ghafla na askari wa Kihehe waliongozwa na nduguye Mkwawa aliyeitwa Mpangile.  Karibu askari wote wa Kijerumani waliuawa, akiwemo Zelewsky mwenyewe.  Ni askari watatu wa Kijerumani pamoja na wenzao sitini na wawili tu wenye asili ya Kiafrika ndio waliookoka wakakimbia salama. Katika vita hiyo Mkwawa aliteka zaidi ya bunduki 250, mizinga mitatu na zana nyingi za vita, nyingi kati ya hizo zikiwa risasi na baruti.  Kwa upande mmoja vita hiyo iliwadhalilisha sana Wajerumani, na kwa upande mwingine iliwatia moyo Wahehe waendelee na upinzani wao ya utawala wa kikoloni wa Kijerumani.

Na huko upande wa kaskazini wa Koloni la Wajerumani la Afrika ya Mashariki, Wachagga nao, chini ya Mangi (Mteni) Meli wa Moshi, walikataa katakata kutawaliwa na Wajerumani.  Katika jitihada za kutaka kuwatiisha Wachagga, serikali ya kikoloni ya Wajerumani ilipeleka jeshi la askari huko Kilimanjaro, lililoongozwa na Burlow akisaidiwa na Luteni Wolfrum.  Jeshi hilo la Wajerumani lilishambuliwa na askari wa Mangi Meli waliolizingira kwa ghafla kutoka maoteoni.  Bwana Burlow, Luteni Wolfrum pamoja na askari wengi wa Wajerumani waliuawa.  Askari wa Kijerumani walionusurika walirudi haraka Marangu, mahali ambapo makao yao makuu yalikuwa yamehamishiwa.

Baada ya kuunda jeshi jingine lenye nguvu.  Wajerumani walikusudia kwenda tena Kilinjaro kumpiga vita Mangi Meli aliyekuwa akikataa kuwekwa chini ya utawala wao.  Safari hii jeshi hilo la Wajerumani lilitokea pwani kuelekea Kilimanjaro, liliongozwa na Gavana mwenyewe bwana Friedrich von Schele.  Baadhi ya wamangi (Watemi) wa Uchaggani waliokuwa na uhasama na ******** 

Matangazo maalum ya kibiashara (nafasi hii inalipiwa)

زيت ارغان    Mafuta ya Arghani mafutayaarghani

Matoleo mapya ya kitabu kipendwacho cha Mkweli Mwaminifu yako tayari.Agizia mapema kutoka kwetu.

mkweli mwaminifu 

Suruali za kuvalia kanzu za kiume. na za kike

Zipo za ukubwa na rangi mbali mbali .Ni mali kutoka nchini Morocco.

Zinapatikana Kwa reja reja na kwa jumla .Ili Kujua zaidi wasiliana nasi hapa.

 

  SURUALI MOROCO      SURUALI MOROCCO

MWANGAZA KWA UMMA

Tofauti kati ya Tohara na kukeketa
Na Skh Mussa Kileo

Kila inapofika tarehe 6 Februari, Umoja wa Mataifa huadhimsha siku ya kupinga ukeketaji wa wanawake Duniani . Kwa wanaharakati wa Haki za binaadam na jinsia huiadhimisha siku hii kwa kauli mbiu mbalimbali na maazimio ya kushinikisha jamii ibadilike ili iachane na kuwakeketa wanawake.

Ukeketaji ni jambo lilioenea katika vinywa vya watu na kuandikwa na asasi mbali mbali za kijamii,na ipo haja kubwa kwa jamii ya kiislaam kulichambua jambo hili kwa kina,na ufafanuzi kama ifuatavyo:

Endelea