Morocco,nchi ya amani, usafi na usafiri rahisi

 Treni za Rabat

Na mwandishi wetu.Dar es salaam

26 Juni 2017

Leo ni zaidi kidogo ya miezi mitatu tangu nirudi safari yangu ya mwanzo nchini Morocco ambayo ilinipeleka pia kwenye jiji la kibiashara la Casablanca linalojulikana na wenyeji kama Daarul Baidhaa

Makazi yangu rasmi yalikuwa ni jijini Rabat pembezoni kabisa mwa bahari ya Atlantic na sehemu ambapo mto Bouregreg unakutatana na bahari hiyo yenye upepo mkali na mawimbi daima.

Yapo mengi ya kusimulia na niliyojifunza hata hivyo kulingana na mazingira ya nyumbani nilikotoka nilivutiwa zaidi na usafi wa barabara za jiji hilo na wepesi wa  safari za kuzunguka huku na kule ndani ya jiji hilo.Hii bila shaka inachangiwa na kuwepo kwa mabasi ya abiria ya umma na treni zake za umeme na za kawaida zinazovinjari mchana na usiku kwenye vichochoro vyote vya jiji hilo.

Ukiachana na aina hizo za usafiri, usafiri mwengine ni gari ndogo ndogo za abiria watatu na hata zaidi mfano wa teksi kwa miji mengine.Gari hizi ziko zenye alama maalum ya kutumika kwa kazi hiyo na nyengine nyingi zinazoshiriki bila alama yoyote.Hii ni moja ya kazi zenye kutoa ajira kwa maelfu ya wakazi wa jiji hilo.

Jambo jengine linaloondoa changamoto za usafiri  zinazokuwepo miji mengine ni wingi wa njia za kupishana hewani kuelekea kila mji.Kwa mfano ukitoka Rabat kuelekea Daarul Baidhaa kuna njia nyingi za kukupeleka huko kuanzia treni za mwendo kasi njia kadhaa zenye lami  maridadi kabisa.

Safari moja tulikwenda jijini huko kupitia njia inayotambaa ufukweni mwa bahari kupitia moja ya Qasri la mfame Muhammed wa sita kupitia mlji wa Muhammadia.Njia hii ni ndefu kidogo lakini ni tulivu kwani inaelekea upande mmoja tu na huenda magari mengi yanakwepa kwa makusudi kupita pembezoni mwa ikulu hiyo kwani  unakutana na askari wengi sana kiasi kwamba kosa dogo la kidereva au kiufundi linaweza likakutia matatani.Safari ya pili tulitumia njia nyengine ambayo  ina kizuizi cha kielektronic kukuzuia usipite mpaka ulipe ada maalum ya barabara.Hata hivyo hakuna foleni kwa kazi hiyo na mara unapolipa haraka uaondoka kupinda na kupanda madaraja ya hewani bila hata kuonngozwa na mataa ya barabarani isipokuwa maeneo maalum ya kiusalama.

Ama kuhusu usafi wa jiji hilo ni jambo jengine lenye kupendezesha macho ya yeyote mwenye kutembelea jiji hilo.Mapema kabisa kabla hakujakucha tayari magari ya kuzoa taka huwa tayari yamemaliza kazi zake na kuliacha jiji liking'ara kwa kijua chake ambacho daima kinaambatana na baridi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kuhusiana na usalama wa wakazi wake huenda jiji la Rabat ni moja ya miji yenye kiwango cha juu cha usalama duniani.Ni nadra sana kusikia kelele za mwizi pamoja na kwamba wizi kama wa simu za mkononi huwa kila mgeni anatahadharishwa na wennyeji wake.Hisia ya amani kwa mkazi wa jiji hilo inatokana na kila eneo kuweplo askari wanaovinjari kwa miguu na silaha na pingu za kuwadhibiti wahalfu.

Watu wa Rabbat na Morocco kwa ujumla ni mashujaa sana wa kazi za aina zote,ndio maana si aghalabu kukuta wageni waliojiriwa kufanya kazi hata zile zenye kukirihisha nafsi,bali wao wenyewe ndio wafanyaji wa kazi hizo.

Nikirudi kwenye ubora wa usafiri na kupungua msongamano,tofauti na mataifa mengi ya kiafrika yanayoendelea kiuchumi.Nchini Morocco foleni za magari hazidumu zaidi ya dakika tano katika hali ya kawaida.

 Sehemu kubwa ya uoto wa asili wa nchi ya Morocco ni majani madogo madogo na mauwa ya rangi kali kali yanayotandawaa pembezoni mwa barabara utadhani yameotoshwa na kupangiliwa kwa ajili ya mapambo. Kwa upande mwengine ardhi yake si tambarare wala si ya milima mirefu bali ni uwanda unaopelekea macho kuona upeo wa mtazamaji.

 

Katika uwanda huo unaounganisha miji na vijiji ni nadra kukuta wakulima wa mazao ya kila namna yanayopatikana kwenye masoko ya nchi hiyo.Katika ufuatiaji wangu niligundua mazao mengi ya kilimo ni kutoka nchi za mbali hasa za Ulaya zinazopakana nayo.Hili linasaidiwa sana na kuwepo kwa mtandao ambao si mdogo wa usafiri wa anga wa shirika la ndege la nchi hiyo linalojulikana kama Royal du Maroc.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Muhammad Khamis uliopo jijini Daarul Baidhaa ambao ni mkubwa sana na wa kisasa na ambao unachukua nafasi kama kituo kikuu cha Royal du Maroc umeunganishwa na kituo cha reli ambayo inaelekea miji yote mikubwa ya nchi hiyo kusini na kaskazini.Kwa abiria ambaye hana usafiri binafsi hapati tabu kabisa kwani mara amalizapo taratibu za kutoka uwanjani hapo anakutana na gari moshi hizo bila hata kutoka nje hata hatua moja.

 
Treni za Rabat

 

Matangazo maalum ya kibiashara (nafasi hii inalipiwa)

زيت ارغان    Mafuta ya Arghani mafutayaarghani

Matoleo mapya ya kitabu kipendwacho cha Mkweli Mwaminifu yako tayari.Agizia mapema kutoka kwetu.

mkweli mwaminifu 

Suruali za kuvalia kanzu za kiume. na za kike

Zipo za ukubwa na rangi mbali mbali .Ni mali kutoka nchini Morocco.

Zinapatikana Kwa reja reja na kwa jumla .Ili Kujua zaidi wasiliana nasi hapa.

 

  SURUALI MOROCO      SURUALI MOROCCO

MWANGAZA KWA UMMA

Tofauti kati ya Tohara na kukeketa
Na Skh Mussa Kileo

Kila inapofika tarehe 6 Februari, Umoja wa Mataifa huadhimsha siku ya kupinga ukeketaji wa wanawake Duniani . Kwa wanaharakati wa Haki za binaadam na jinsia huiadhimisha siku hii kwa kauli mbiu mbalimbali na maazimio ya kushinikisha jamii ibadilike ili iachane na kuwakeketa wanawake.

Ukeketaji ni jambo lilioenea katika vinywa vya watu na kuandikwa na asasi mbali mbali za kijamii,na ipo haja kubwa kwa jamii ya kiislaam kulichambua jambo hili kwa kina,na ufafanuzi kama ifuatavyo:

Endelea