Adhana Misikitini kupigwa marufuku

·         Yadaiwa inaleta kelele
Tel Aviv,
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anaunga mkono pendekezo la kupunguza sauti za wito wa ibada 'adhan', akisema kuwa amepokea malalamishi ya kelele.
Kwa mujibu wa taarifa ya mapema juma hili ya shirika la utangazaji la Uingereza (BBC), siku ya jumapili kamati ya serikali imejadili mswada ulio na mpango huo.
Vyombo vya habari vya Israel vinasema kuwa mikakati hiyo inazuia misikiti kutotumia vipaza sauti mara tano kwa siku ili kuwaita wafuasi wa dini hiyo kufanya ibada.
Wakosoaji wanasema sharia hiyo itakuwa ya ukadamizaji, na itaathiri dini zote lakini itatumika sana miongoni mwa wito wa ibada miongoni mwa Waislamu au 'adhan'.
Adhan ya kwanza hufanyika mapema alfajiri huku ya mwisho ikifanyika baada ya jua kutua.
Takriban asilimia 17.5 ya raia wanaoishi Israel ni Waarabu na wengi wao ni Waislamu.

Matangazo maalum ya kibiashara (nafasi hii inalipiwa)

زيت ارغان    Mafuta ya Arghani mafutayaarghani

Matoleo mapya ya kitabu kipendwacho cha Mkweli Mwaminifu yako tayari.Agizia mapema kutoka kwetu.

mkweli mwaminifu 

Suruali za kuvalia kanzu za kiume. na za kike

Zipo za ukubwa na rangi mbali mbali .Ni mali kutoka nchini Morocco.

Zinapatikana Kwa reja reja na kwa jumla .Ili Kujua zaidi wasiliana nasi hapa.

 

  SURUALI MOROCO      SURUALI MOROCCO

MWANGAZA KWA UMMA

Tofauti kati ya Tohara na kukeketa
Na Skh Mussa Kileo

Kila inapofika tarehe 6 Februari, Umoja wa Mataifa huadhimsha siku ya kupinga ukeketaji wa wanawake Duniani . Kwa wanaharakati wa Haki za binaadam na jinsia huiadhimisha siku hii kwa kauli mbiu mbalimbali na maazimio ya kushinikisha jamii ibadilike ili iachane na kuwakeketa wanawake.

Ukeketaji ni jambo lilioenea katika vinywa vya watu na kuandikwa na asasi mbali mbali za kijamii,na ipo haja kubwa kwa jamii ya kiislaam kulichambua jambo hili kwa kina,na ufafanuzi kama ifuatavyo:

Endelea