Asasi ya CHAYODE kufuatilia rasilimali ya umma sekta ya elimu

Na Thadei Hafigwa – Morogoro Press Club (MPC)
27April 2017
Asasi ya CHAYODE ni miongoni wa mashirika yasiyo ya kiserikali yaliopo hapa nchini imeyojikita katika kusaidiana  wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo kuibua na changamoto zinazowakabili wananchi vijijini kiwemo mazingira,haki za vijana,watoto na makundi maalum.
Hussein Rajab ni mratibu wa mradi wa ufuatiliaji wa rasilimali za umma  sekta ya elimu katika tarafa ya Mgeta wilayani Mvomero kupita asasi ya CHAYODE yenye makao makuu yake sabasaba mjini Morogoro.
Rajabu anasema asasi yake ya CHAYODE ni ufupisho wa maneno ya kiingereza ambayo ni Children and Youth Development Centre ilisajiliwa 20/2/ 2001 ambapo katika tafsiri isiyo rasmi kwa lugha ya Kiswahili ni kituo cha maendeleo ya watoto na vijana.
Ufuatiliaji wa rasilimali za umma imekuwa ni suala mtambuka katika vinywa vya watanzania kutokana na baadhi ya watumishi wa serikali wachache kutokuwa waadilifu katika usimamiaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoibuliwa na wananchi katika maeneo husika.
Utafiti uliofanywa na Asasi cha CHAYODE katika tarafa ya Mgeta wilaya ya Mvomero imebaini ya kuwa rasilimali fedha zinapotolewa na serikali kuu hususan sekta ya elimu imekuwa ikikosa usimamizi madhubuti na kusababisha pesa nyingi kupotea na miradi mingi kufanywa chini ya kiwango.
Asasi  hiyo chini ya ufadhili wa  shirika la the foundation for civil society inatekeleza mradi wa mafunzo ya ufuatiliaji wa rasilimali za umma kwa wananchi wa vijiji vya Langali,Nyandira,Bumu,Ng'unguru, Nugutu,Tchezema na Kibegala na kuwashirikisha vongozi wa Vijiji,kata, watendaji wa kata,waratibu elimu,madiwani na wananchi wa kawada wanaoishi katika maeneo yao.
Rajabu anasema katika utekelezaji wa mradi huo,amewakumbusha jamii kuwa waadilifu na kuzingatia masuala ya utawala bora ambapo aliwataka viongozi  na jamii kutambua wajibu wao wa kuwahudumia wananchi bila ya upendeleo na kuondokana na tabia ya kupendelea kutoa na kupokea rushwa wakati wa utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.
Ruth Michael ni Afisa tarafa ya Mgeta ambaye wakati wa mafunzo hayo alikuwa mgeni rasmi ambapo pamoja na mambo mengine aliwaasa watumishi wa umma na watendaji wa vijiji na kata kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kanuni zake kwa kutumia busara ili kupunguza kero za wananchi na kutekeleza miradi ya serikali kwa  kuzingatia vipaumbele vilivyotolewa na wananchi wenyewe.
“Watumishi wengi tunafanya kazi kwa mazoea kuondokana na tabia hiyo ili kuwatumikia wananchi ili kuharakisha maendeleo yao na kwamba Tarafa ya mgeta kuwa mfano mwema”alisema Afisa tarafa wa Mgeta,Bi Ruth
Aidha, mafunzo hayo yaliweza kufanyika katika maeneo mengine katika mkoa wa Morogoro ambayo ni kata ya Langali,Nyandira na Tchenzema zilizopo katika tarafa ya Mgeta halmashauri ya wilaya ya Mvomero kutokana na changamoto nyingi katika sekta ya elimu kulalamikiwa na wananchi.
Kamati ya ufuatiaji wa kukusanya takwimu za elimu.watendaji wa vijiji,kata na wananchi wa kawaida ambao kila mmoja alipata fursa ya kuelezea changamoto wanazokabiliana nazo katika maeneo wanayotoka ziliundwa ili kurahisisha wananchi kutambua rasilimali zao zinatumika kwa kadri ya vipaumbele walivyoanisha kwenye vikao vyao halali.
Afisa wa Tarafa ya Mgeta,Bi.Ruth .aliweka msisitizo kutokana na kazi zilizofanywa na asasi ya CHAYODE katika tarafa ya Mgeta atasisimamia na kuwa mfano kwaWilaya ya  Mvomero, kubaini changamoto zilizokuwa zikiwakabili sekta ya elimu ambapo kwa wilaya ya Mvomero kumekuwa na kiwango cha ufaulu kuwa cha chini katika mitihani ya kitaifa.
Ruth  alisema “watendaji na watumishi wa umma mnapaswa kuwapa ushirikiano wa kutosha wadau wa eilimu ikiwemo Asasi ya CHAYODE katika maeneo yetu ya kazi kwa kuzingatia uadilifu kwa kufata mifumo sahihi ya ufuatiliaji wa rasilimali za umma ili kupunguza migongano katika jamii ili kuhakikisha ya kuwa tarafa ya Mgeta inakuwa ya mfano kwa kutoa huduma bora kwa kuzingatia misingi ya utawala bora”.
Aidha,CHAYODE na wadau wake  na kuliweza kuungana kwa kubadilishana uzoefu na maarifa katika kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi hususan vijijini ambako asilimia kubwa ya watanzania wanaishi.
Afisa tarafa Bi Ruth hakusita kuwaelekeza watendaji wa vitongoji,vijiji na kata kutumia busara na hekima wakati wa kuwahudumia wananchi ambao wakati mwingine wanashindwa kutambua taratibu za upatikanaji huduma kwa kuruka ngazi ambapo ofisi yake imekuwa mara kwa mara ikiwaelekeza katika kufuata utaratibu.
Alisema ofisi yake mara kwa mara imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wananchi baada ya kutoridhishwa na huduma kutoka kwa watendaji wao wa vitongoji,vijiji na kata hali inayopelekea wananchi kuwa na dhana ya kukosa imani katika ngazi za chini.
Katika mafunzo hayo mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwa ni kuhakikisha ya kuwa viongozi wanakuwa na uelewa wa kutosha katika kusimamia rasilimali za umma katika sekta ya elimu,mada hizo ni pamoja na utawala bora,ufuatiliaji wa mali za umma na masuala ya maadili ambayo yaliwasilishwa na Rajabu Hossein.
Rajabu analiwaeleza washiriki wa mafunzo hayo kuwa suala la maadili limekuwa ni changamoto kubwa kwa viongozi wa serikali ambapo baadhi ya washiriki walianisha suala la rushwa na uadilifu katika maeno ya kazi.
“Ili kuondokana na hali hiyo ndugu washiriki mbadilike katika maeneo yetu ya kazi,wananchi wanawategemea sana ninyi katika kusimamia maadili ya kazi na utoaji wa huduma kwa ujumla”Alisema Rajabu
Katika suala la utawala bora iliwasilishwa na mmoja kati ya wajumbe wa bodi ya CHAYODE,Esther Chissunga aliwasisitiza viongozi wa serikali za vijijini na kata kwamba dhamana walio nayo ni moja ya nyezo ya kuwaondolea kero wananchi kwa kufuata misingi ya utawala bora ambayo ni uwazi,uwajibikaji na kuondokana na urasimu katika utoaji wa huduma.
Washiriki waliweza kukumbushwa sheria na 7 ya mwaka 1982 kifungu cha 5 na 12(1) kinachoelezea halmashauri za wilaya huanzishwa katika kila eneo la utawala la wilaya,ambapo ni mamlaka ya juu kabisa kisiasa katika wilaya na zina hadhi ya uhai wa kudumu wa sheria ,kuwa na nembo na uwezo wa kushitaki na kushitakiwa.
Mada hiyo ilitolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii Mstaafu,Esther Chissunga alifafanua kuwa sheria hiyo inatoa mamlaka halmashauri za wilaya zina uhuru kamili kisheria kuhusu fedha,utawala na mipango.
Halmashauri za wilaya pia huratibu mamlaka za miji midogo ambayo huanzishwa chini ya sheria na 8 ya 1982 pamoja na halmashauri za vijiji ambazo ni mamlaka hai za ngazi za chini kisheria.Halikadhali,kata na vitongoji ni ngazi za utawala na kamati za maeneo chini ya halmashauri za wilaya.
John Koba kutoka shirika la Umwema aliwapa uzoefu washiriki wa mafunzo hayo kwenye ufuatiliaji wa rasilimali za umma hali ambayo iliwafungua masikio na kuona kwamba iwapo misingi ya utawala bora,maadili ya utumishi wa umma na utumiaji wa rasilimali za umma kuna harakisha maendeleo ya wananchi bila ya kuwepo manung’uniko na kero kwa wananchi.
Koba alibainisha ya kuwa madiwani wanawajibu mkubwa wa kusoma na kufuatilia mipango mbalimbali inayowekwa kwenye halmashauri mipango iliyowekwa ili kuhakikisha wapi mipango imewekwa na imekwamisha na kitu gani katika utekelezaji wake.
Mratibu Elimu kata ya Langali, Augustine Mkude alichangia hoja wakati wa mafunzo hayo alisema changamoto zinazojitokeza katika maeneo mbalimbali ya kiutawala inatokana na baadhi ya wateuliwe kutokuwa na sifa za uadilifu hali inayopelekea kuwepo kwa malalamiko mengi katika sehemu ya kazi.
“Ukiangalia changamoto si kwenye sekta ya elimu pekee  ni miongozo iliyotolewa na serikali ya shule ya msingi na sekondari kwamba ufinyu wa bajeti unapotokea wadau wanaweza kushirikishwa ili kukabiliana changamoto hizo,tatizo ipo dhana kwa jamii kwamba elimu ni bure hivyo wanapohamasishwa kuchangia utekelezaji wake unakuwa mgumu” alisema Mkude.

Matangazo maalum ya kibiashara (nafasi hii inalipiwa)

زيت ارغان    Mafuta ya Arghani mafutayaarghani

Matoleo mapya ya kitabu kipendwacho cha Mkweli Mwaminifu yako tayari.Agizia mapema kutoka kwetu.

mkweli mwaminifu 

Suruali za kuvalia kanzu za kiume. na za kike

Zipo za ukubwa na rangi mbali mbali .Ni mali kutoka nchini Morocco.

Zinapatikana Kwa reja reja na kwa jumla .Ili Kujua zaidi wasiliana nasi hapa.

 

  SURUALI MOROCO      SURUALI MOROCCO

MWANGAZA KWA UMMA

Tofauti kati ya Tohara na kukeketa
Na Skh Mussa Kileo

Kila inapofika tarehe 6 Februari, Umoja wa Mataifa huadhimsha siku ya kupinga ukeketaji wa wanawake Duniani . Kwa wanaharakati wa Haki za binaadam na jinsia huiadhimisha siku hii kwa kauli mbiu mbalimbali na maazimio ya kushinikisha jamii ibadilike ili iachane na kuwakeketa wanawake.

Ukeketaji ni jambo lilioenea katika vinywa vya watu na kuandikwa na asasi mbali mbali za kijamii,na ipo haja kubwa kwa jamii ya kiislaam kulichambua jambo hili kwa kina,na ufafanuzi kama ifuatavyo:

Endelea