Tanga kujenga hospitali kubwa ya kiislamu.

TANGA KUJENGA HOSPITALI YA KIISLAMU

Na mwandishi wetu,Tanga

Jumapili 18 Ramadhani 1436H,Julai 5-2015.

Waislamu nchini kwa uwezo wa Allah s.w  wataendelea  kupata nafuu ya huduma za matibabu baaada ya kongamano kubwa kufanyika jijini  Tanga kuchangia ujenzi wa hospitali itakayofuata maadili ya dini yao.

Hospitali  hiyo inatarajiwa kujengwa  eneo la Neema nje kidogo ya jiji la Tanga njia iendayo  Pangani.

Akizungumzia  historia ya azma ya kujengwa  kwa kituo hicho  cha aina yake,mweka hazina wa taasisi  ya TIDF,sheikh  Omar Zubeir  alisema,  utoaji  wa huduma  kwa  jamii za aina hiyo  ni moja ya malengo  ya taassisi  ya Tanga Islamic Developement  Foundation iliyopata usajili mwaka  2010 kwa  hati  nambari  16836.

sheikh Ayoub Ngando akitoa nasaha
Sh.Ayoub Ngando

Kwa kuzingatia  hilo taasisi hiyo kwa makusudi  iliasisi  wazo la kujenga hospitali  ya kiislamu  ili kutoa huduma za afya za nafuu na kwa  kufuata maadili mema kwa akinama na watoto kwa kuanzia.

Ili kufanikisha  mpango huo taasisi  imekuwa ikifanya vikao vingi kwenye misikiti ya Masjid Quba eneo la Masiwani,masjid Aqswa eneo la Mabawa na masjid  Ngazija eneo la katikati ya jiji.

Jitihada hizo hatimaye zilifanikisha kupatikana kwa eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 3642 kwenye  kiwanja nambari  Plot 316 Block A eneo la Neema.

Kupitia michango mbali mbali ya waumini,TIDF mpaka sasa imekamilisha mchoro wa ujenzi wa hospitali hiyo na kupata kibali cha ujenzi kutoka Halmashauri ya jiji la Tanga chenye nambari  0179.Tayari eneo lote  limezungushiwa uzio  kusubiri hatua za mwanzo za ujenzi.

                Vitengo vya mwanzo vinavyokusudiwa kujengwa katika mradi huu ni pamoja  jengo la  utawala na ,chumba cha upasuaji  pamoja na wadi ya kujifungulia ya akinamama.Mbali na hivyo vipo  vitengo vyengine 7 kwa ajili ya wagonjwa wengine wa jinsia zote.Jengo kuu la utawala linatarajiwa kuwa la ghorofa 2.

Ili kufanikisha hatua hizo za ujenzi,  makadirio yanaonesha zitahitajika jumla ya shilingi Bilioni moja,milioni mia tano na thelathini ,laki tano na thelathini na nane na mia saba na ishiri na sita.(1,530,538,726/-).

Ukumbi wa Simba mtoto umefurika
waislamu wakiahidi kuchangia na kufanikisha ujenzi
Masheikh kadhaa wenyeji wa Tanga walishiriki katika uhamasishaji  kwenye kongamano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Simba Mtoto uliojulikana zamani kama Ridoch Motors.
Kwa upande wake sheikh Muhammad  Juma Mdharuba ambaye ni mwenyekiti wa mradi wa hospitali alisema, kwa idadi yoyote waumini waliofika kwenye kongamano hilo si wengi kuliko walioalikwa na wahitaji wa huduma hizo.Hata hivyo akakumbusha kauli iliyo katika Qur’an kwamba uchache wa watu walio kwenye jambao la haki si kigezo cha kushindwa kwa lile wanalolipigania.

كَم مِّن فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةًبِإِذْنِ اللّهِ وَاللّهُ مَعَ الصَّابِرِين

Makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.(Qur 2;49).

Katika nukta hiyo hiyo,sheikh Kassim Rashid Mohammed alikumbusha tukio katika seera ya Mtume swalaLlaahu alayhi wassalaam,ambapo katika vita vya Hunayn waislamu walijifakharisha kwa wingi wao na kujiamini  kupata ushindi.Kinyume na matarajio yao waislamu katika vita hivyo walishindwa hata ikawalazimu kutimua mbio kuwakimbia maadui zao.

Tukio muhimu katika kongamano hilo ambalo lilielekea kuhitimisha ratiba nzima ilikuwa ni kuchangia gharama za ujenzi.Njia  mojawapo iliyotoa mchango mkubwa wa fedha taslimu ilikuwa katika kumnadi mbuzi aliyefikishwa ukumbini hapo ambapo alinunuliwa kwa jumla sh,600,000.

Katibu wa mradi huo wa hospitali,ustadhi Ahmad Ayoub Kidege alifafanua kwamba kaika kongamano kama hilo la mwaka jana jumla ya shilingi milioni nne zilipatikana ambazo ndizo zilizosaidia pakubwa katika maandalizi ya eneo hilo.Fedha hizo nyingi zilipatikana kwa njia ya kugawa bahasha maalum ambazo zilirejeshwa zikiwa na kiasi tofauti cha pesa

Akinamama katika kongamano la uchangiaji hospitali ya kiislamuHivyo mbali na  michango ya papo kwa papo na ahadi,bahasha 5000 zilikuwa tayari kwa kugawiwa ambapo waumini waliondoka na idadi tofauti ili kuzisambaza kwa wenzao ambao hawakuwepo ukumbini hapo.

Muhtasari wa michango iliyopatikana ni kama ifuatavyo.Michango ndani ya ukumbi 2,074,050.Ahadi 5,150,000.Kupitia mitandao ya simu ni 287,000.Ahadi ya vifaa ni mifuko ya saruji 67,mawe gari 1,mchanga gari 1na kwenye tamasha la Idi ni 445,000/.Michango hii ni kabla ya kufunguliwa kwa bahasha  zinazoendelea kukushanywa ofisini.

Njia nyengine mbadala za kuchangia ziliongezwa kwenye kongamano la mwaka huu jambo ambalo linatarajiwa kuongeza mapato yatakayofanikisha kuanza kwa ujenzi mapema kadri iwezekanavyo.

 

Kwa wale ambao hawakubahatika kufika kwenye kongamano hilo milango ya kuchangia bado iko waziCHANGIA UJENZI WA HOSPITALI YA KIISLAMU TANGA.Na Kama una mchango bora wa mawazo kufanikisha mradi huu tafadhali TOA HAPA

Matangazo maalum ya kibiashara (nafasi hii inalipiwa)

زيت ارغان    Mafuta ya Arghani mafutayaarghani

Matoleo mapya ya kitabu kipendwacho cha Mkweli Mwaminifu yako tayari.Agizia mapema kutoka kwetu.

mkweli mwaminifu 

Suruali za kuvalia kanzu za kiume. na za kike

Zipo za ukubwa na rangi mbali mbali .Ni mali kutoka nchini Morocco.

Zinapatikana Kwa reja reja na kwa jumla .Ili Kujua zaidi wasiliana nasi hapa.

 

  SURUALI MOROCO      SURUALI MOROCCO

MWANGAZA KWA UMMA

Tofauti kati ya Tohara na kukeketa
Na Skh Mussa Kileo

Kila inapofika tarehe 6 Februari, Umoja wa Mataifa huadhimsha siku ya kupinga ukeketaji wa wanawake Duniani . Kwa wanaharakati wa Haki za binaadam na jinsia huiadhimisha siku hii kwa kauli mbiu mbalimbali na maazimio ya kushinikisha jamii ibadilike ili iachane na kuwakeketa wanawake.

Ukeketaji ni jambo lilioenea katika vinywa vya watu na kuandikwa na asasi mbali mbali za kijamii,na ipo haja kubwa kwa jamii ya kiislaam kulichambua jambo hili kwa kina,na ufafanuzi kama ifuatavyo:

Endelea