Jitihada za kifikra kupambana na kupitukia mipaka

Na Sheikh Mohamed Mahmud Abdulfataah – Al Azhari Sharif
Kwa yakini kupitukia mipaka na uasi ni muonekano mbaya unaoneza mambo yake maovu, kunawiri hatari zake na kukua haraka athari zake mbaya, kwa kuitikisa amani ya jamii na kuyumbisha utulivu wake.
Kutokana na hilo, Uislamu ukaweka jitihada kubwa ya kifikra kupambana na uasi huo wa kidini unaoshadidia misimamo ya kupitukia mipaka na kutaka jamii nzima iburuzike kwenye misimamo hiyo ya kufurutu ada badala ya misingi bora ya ukati na kati.
Basi Dini yetu tukufu inaiwajibisha jamii kung’ang’ania uchache wa madhara ya fikra za aina hiyo kwa kuwahi mapema kukipika kizazi kichanga cha watoto na vijana wetu wasiangukie kwenye mikono isiyo salama na kukosa mafundisho sahihi ya Uislamu.
Bali Mfumo wetu kamilifu wa Maisha (Dini) ya Kunyenyekea na kujisalimisha kwa Mola wetu Muumba (Uislamu) unakokoteza kufuta athari za misimamo ya kupitukia mipaka na kukausha vyanzo vyake.
Vi vema Waislamu wakapeana majukumu ya ushirika (baina ya mtu mmoja na jamii) katika malezi bora kwa watoto na vijana wetu ili wawe ‘barua inayosomeka’ kwa wengine na kujenga taswira nzuri na mitizamo chanya ya Waislamu na Uislamu kwa wasio Waislamu; na hapa ndipo panapokuja nafasi ya taasisi za Dini kurithisha kizazi kichanga chenye akili nyembamba mafunzo sahihi ya Uislamu, ambayo hubeba juu ya shingo yake majukumu ya kuanzisha na kutoa kizazi chenye ufahamu halisi chini ya mapokezi kamili na mazingatio yaliyotimia ya utekelezaji wa sharia za Uislamu.
Kwa hiyo Waislamu kama umma hatuna budi kufanya uteuzi mzuri wa mwongozo wa masomo (mitalaa) unaoshikana na uwastani na msamaha kwa kuakisi matukio, wakati na hali, ili kuiweka mbali jamii yetu na janga la kupitukia mipaka na uasi wa kidini.
Tusalimike na kuzidisha visivyozidishwa, lakini pia tusalimike na kupunguza visivyopunguzwa katika Dini, halkadhalika tusalimike na kupuuzia visivyotakiwa kupuuzwa ili tusizame kwenye msimamo ya kupitukia mipaka.
Kwa hiyo ni jukumu letu kuisomesha jamii yetu ya leo na kesho katika vitengo vyote vya elimu kwa kuchunga muda, mazingira na hali.
Pia hatuna budi kuufundisha utamaduni wa kuishi kwa amani baina ya watu wa mitazamo na Dini tofauti, na kupalilia maisha ya kushirikiana baina ya jamii tofauti bila ya kusukumwa na udini, ukabila, utaifa, urangi, utabaka (masikini au tajiri) na imani za kisiasa, maumbile (ulemavu, ugonjwa au uzima), jinsia (mwanamke au mwanaume), umri na rika (mtoto au mkubwa, kijana au mzee) n.k kwani wote ni washirika katika haki, mali na uhai bila kuruka mipaka aliyoweka Mwenyezi Mungu (S.W).
Jambo linguine ni kuwa na ulazima wa kuwalea watoto juu ya misingi ya msamaha wa Uislam na kukokoteza uwepesi wa sheria zake, na kurithisha historia kutengamaa kwa kwa Uislamu kwa kila sekta na kila zama chini ya mifano hai yenye mwangaza toka katika Qur’ani Tukufu na Sunna.
Mafundisho sahihi na na Historia halisi ya Uislamu vinaonesha uzuri wa muamala wa Kiislam hata na wale maadui wa Dini hii!
Lingine la kusaidia kuiepusha jamii yetu hasa kizazi kichanga na fikra za uwasi wa kidini na kupitukia mipaka ni kujibebesha jukumu muhimu la kufundisha kanuni sahihi za kulingania Dini ya Allah (S.W) yaani kwa njia za hekima, busara na mawaidha mazuri; na iwapo kuna mjadala au mdahalo na wasio Waislamu basi uwendeshwe kwa njia nzuri.
Jambo linguine la kuzingatia ni kubainisha na kukiri kuwa Dini inatangazwa na wala hailazimishwi, hapana kulazimisha katika kujiunga na kuingia katika Dini na kuchagua, wala kuteza nguvu juu ya Dini na kuingia katika imani kama navyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu; “Hakuna kulazimishwa (mtu kuingia) katika Dini. Uongofu umekwishapambanuka na upotofu. Basi anayemkataa shetani na Akamwamini Mwenyezi Mungu, bila shaka yeye ameshika kishiko chenye nguvu kisichokuwa na kuvunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kujuwa” Aya ya 256 ya Suurat Al Bakarat.
Kwa hakika zama zinabadilika na nahali hugeuka, hapo kale palikuwa vita hupiganwa kwa silaha pekee, lakini katika zama zetu hizi vita hupiganwa kwa silaha na kwa fikra; basi hakuna vita mbaya kama vita ya fikra.
Kwa yakini unapigwa vita Uislam na kuwateka watu wake kwa kutumia fikra, pia kuwadhalilisha watu wake, na kuwapaka matope kutokana na kulegea misingi ya mafundisho sahihi ya Dini yao, hivyo kuliachia kundi kubwa la wafuasi wake hasa vijana kutekwa na maadui kwa kujibebesha misimamo ya kufurutu ada bila kufahamu.
Nikamilishe waadhi wa leo kwa kusisitiza kuwa, Mtoto katika Uislamu ni wa jamii nzima, kila mtu anawajibika naye; hivyo kuanzia ngazi ya familia (baba na mama), kisha ukoo, jamii, waalimu, Maimamu (viongozi) na yeyote mwingine wana wajibu wa kuwafunza na kuwarithisha watoto na vijana wetu fikra sahihi za ukati na kati wa Dini yetu na kuwaweka mbali mno na fikra za uwasi wa Kidini kwa kupitukia mipaka kimisimamo.
Tunamuomba Allah (S.W) Atuhifadhi sisi na kizazi chetu pamoja na Dini yetu na kila chenye madhara kwetu, na kutuongoza kufanya Da’awa kwa usahihi wake badala ya kuvuruga na kuvunja, halkadhalika Atuweke katika amani na kusalimika kupitukia mipaka kiimani, Aamin.
Wabillah Tawfiiq,
Kama una maoni, Maswali au ushauri, usisite kuwasiliana na Mudir, Egyptian Islamic Center kwa Email:This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. .Pia unaweza kutoa maoni KUNENA

Matangazo maalum ya kibiashara (nafasi hii inalipiwa)

زيت ارغان    Mafuta ya Arghani mafutayaarghani

Matoleo mapya ya kitabu kipendwacho cha Mkweli Mwaminifu yako tayari.Agizia mapema kutoka kwetu.

mkweli mwaminifu 

Suruali za kuvalia kanzu za kiume. na za kike

Zipo za ukubwa na rangi mbali mbali .Ni mali kutoka nchini Morocco.

Zinapatikana Kwa reja reja na kwa jumla .Ili Kujua zaidi wasiliana nasi hapa.

 

  SURUALI MOROCO      SURUALI MOROCCO

MWANGAZA KWA UMMA

Tofauti kati ya Tohara na kukeketa
Na Skh Mussa Kileo

Kila inapofika tarehe 6 Februari, Umoja wa Mataifa huadhimsha siku ya kupinga ukeketaji wa wanawake Duniani . Kwa wanaharakati wa Haki za binaadam na jinsia huiadhimisha siku hii kwa kauli mbiu mbalimbali na maazimio ya kushinikisha jamii ibadilike ili iachane na kuwakeketa wanawake.

Ukeketaji ni jambo lilioenea katika vinywa vya watu na kuandikwa na asasi mbali mbali za kijamii,na ipo haja kubwa kwa jamii ya kiislaam kulichambua jambo hili kwa kina,na ufafanuzi kama ifuatavyo:

Endelea