SHEIKH NDUNGO ASHINDWA KUMZIKA BABA YAKE MZAZI

Na Kombo Hassan

Ijumaa,30/09/2016

Mtihani juu ya mtihani imeendelea kuwafika ndugu zetu katika imani ya Dini ya Uislamu, wanaotuhumiwa kwa tuhuma mbalimbali za Kesi za Ugaidi, kwa mtu mmoja baada ya mwingine ndani na nje ya magereza wanayoendelea kushikiliwa. Sheikh, Ndungo Nasir, ambaye ni baba wa familia, anayeendelea kusota mahabusu kwenye Gereza la Maweni, Tanga, akikabiliwa na tuhuma za “Ugaidi” na kufunguliwa kesi ya uchochezi, mapema wiki iliyopita, ameshindwa kuhudhuria mazishi ya baba yake mzazi Mzee Nasir, aliyefariki nyumbani kwa mtoto huyo wa pekee aliyekuwa akimuuguza kwa muda mrefu, Mjini Tanga, kabla ya kukamatwa kwake. Na mwili wake ulisafirishwa kwenda kuzikwa kwenye Maziara yao kwenye Kijiji cha Tawalani, Wilaya ya Mkinga, Tanga. Sheikh Ndungo, ambaye ni Imamu wa Msikiti na “Daiyah” alikamatwa mapema mwaka huu mnamo Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, wakati wa Magharibi akifuturu yeye na familia yake nyumbani kwake katika Maeneo ya Sahare, Tanga. Kuendelea kushikiliwa kwa Sheikh, Ndungo, kwenye mazishi ya baba yake mzazi kulidhihirisha ni jinsi gani familia yake ilivyopatwa na pigo au msiba mzito wa yeye kuendelea kushikiliwa mahabusu, kwani watu wengi walidhihirika kumlilia na kumsikitikia yeye zaidi kuliko hata baba yake aliyefariki, kwani yeye kabla ya kukamatwa kwake alikuwa ni muhimili mkubwa mno wa familia yake kiuchumi, kimalezi, kielimu, kidini, n.k. Na baadhi ya ndugu wa Familia ya Sheikh Ndungo, katika kuonyesha huzuni yaliyonayo juu yake, mnamo Jumapili ya wiki iliyopita waliongozana kwenda katika Gereza la Maweni, kwa ajili ya kwenda kumjulia hali na kumpa “Mkono wa Tanzia” kwa ajili ya kumtakia subira na kumuombea kila la kheri kwa Fitina ya Mtihani aliyokadiriwa na Allah (Aliye Mtukufu) kumfika kwa hekima yake. Wakati, huo huo katika kadhia inayoendelea ya kamatakama ya Waislamu, mjini Tanga, wanaotuhumiwa kwa tuhuma za “Uchochezi na Ugaidi”, miongoni mwao ambao waliopatwa na fitina ya mtihani huo ni Sheikh Ali Kiroboto, Mudir wa Maahad Daarul-Ulum, Waalimu wawili wa Somo la Maarifa ya Uislamu, katika mashule mbalimbali ya sekondari na Wahadhiri wa Dini ya Uislamu, ndani ya Jiji la Tanga, Masheikh, hao pia wamesema wamepewa namba za kuripoti, na ni Sheikh Chambuso Ramadhani, na Sheikh Hamad Ayubu Kidege, na waliripoti Ijumaa iliyopita ikiwa ni mara yao ya nne tangu kukamatwa kwao na kutakiwa kusaini kila siku ya Ijumaa, kwenye idara ya Polisi ya Upelelezi, Mjini Tanga, wakitokea majumbani mwao baada ya kuachiwa kwa dhamana. Na ni kwamba simu zao mpaka ikiandikwa makala hii, bado zilikuwa zipo mikononi mwa Polisi zikifanyiwa uchunguzi wa kipelelezi, kwa nyakati tofauti walisema Masheikh hao. Pia alihoji Sheikh, Kidege: “Mbona inaonekana tunaoripoti ni Waislamu pekee yetu tu? Je, wenye tuhuma za Ugaidi na Uchochezi Hapa nchini ni Waislamu tu?” alisema Sheikh Kidege. Hii ndio hali inayoendelea na kuwakabili Waislamu kwa sasa Tanzania hususani Tanga. Wabillah Tawfiq.

Vijana 20 wapatiwa Mafunzo ya Nishati ya Jua

Na Ahmed Lukinga, Azadi Mpango MSJ
Alkhamis,28 Mei 2015
Jumla ya Vijana 20 wa  taasisi mbalimbali katika Wilaya za  Kilombero  na Ulanga, Mkoani Morogoro, wamepatiwa mafunzo ya Nishati ya Jua ili waweze kuipeleka teknolojia hiyo Vijijini.
 
Hayo yalibainishwa  na  Meneja wa Nishati ya Jua Wilayani Kilombero, Bw. Adolf  Richard ambaye alisema kuwa kutolewa kwa elimu ya nishati hiyo kutawawezesha vijana hao kuwa na maarifa ya kutosha yatakayowawezesha kujiajiri wenyewe.
 
Alisema kuwa Tanzania inakabiliwa na changamoto ya ajira kwa vijana hali inayopelekea vijana wengi kujiingiza katika vitendo vya uhalifu vinavyotishia amani ya nchi.
“Lengo la kutoa mafunzo haya kwa vijana hawa ni kuwajengea uwezo kuhusu teknolojia hii ya umeme wa Jua ili kuwawezesha kujiajiri  wenyewe na  ninaamini kama watatumia vizuri elimu hii itaweza kuwasaidia kiuchumi’’alisema Richard.
 
Hata hivyo aliwataka vijana hao waliopata mafunzo hayo kutokuwa wabinafsi katika kutoa elimu kwa vijana wenzao ili mafunzo yaliyotolewa yaweze kuwa na faida kubwa zaidi kwa jamii inayowazunguuka.

Wawili wafa kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba,11 waokoka baada ya kuzama baharini

Na mwandishi wetu,

Jumamosi,25/04/2015.

Watu wawili,,mtoto mchanga na kaka yake anayemfuatia wamepoteza maisha baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba alfajiri ya leo wakiwa wamelala.Majeruhi wengine wanne wamelazwa kwenye hospitali ya Bombo wakipatiwa matibabu akiwemo mama wa watoto hao.

Ajali hiyo imetokea maeneo ya barabara ya 19 jirani kabisa na nyumba ya marehemu sheikh Mohammed Mkanga,aliyekuwa sheikh mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Wakati ukuta huo ulipoanguka ilikuwa mvua ikinyesha iliyokuwa imeambatana na upepo mkali..

Kwa mujibu wa shuhuda wa mkasa huo aliyesaidia katika kufukua kifusi kuwapata waathiriwa.Wakati mvua ikiendelea muda huo wa alfajiri ghafla walisikia kishindo kikubwa na kuona ukutta huo ukiwa umeanguka.Kwanza walimpigia simu mwenyekiti wa mtaa,bwana Rajab ambaye haraka alifika na wenzake akiwa na gari.Ndipo walipofanikiwa kuzipata maiti za watoto hao wawili na kuwakimbiza majeruhi hospitali.

Watoto waliofariki ni Hassan mwenye umri wa miaka 7 na nduguye Bakari mwenye umri wa miezi 6.Majeruhi wawili kati ya walionusurika inasemekana wako katika hali ambayo si nzuri

Wakati huo huo wavuvi 11 wa kijiji cha Maboza wamenusurika kufa baada ya boti yao kuzama hapo juzi usiku.Kwa mujibu wa matangazo   ya Redio Nuur 94.5 ya jijini hapa nahodha wa ngarawa hiyo alifanikiwa kupiga simu kwa ndugu zake kwamba walikuwa wanazama.Muda mfupi baada ya mawasiliano hayo hakuweza kupatikana tena.

Ndugu hao walifanya mawasiliano na serikali ya kijjiji iliyotoa taarifa kwa polisi ambao nao walifanya mawasiliano na wenzao wa Kenya ili kusaidiana katika kuwatafuta wavuvi hao.Katika hali isiyotarajiwa wavuvi hao wote wamepatikana wakiwa hai kwenye maeneo matatu tofauti ya bahari kwenye pwani ya Kenya

 

 

 

Meya wa Tanga asisitiza usafi wa mazingira.

Na Salim Mohammed,Tanga

Jumatano,28/01/2015

Tanga, MEYA wa jiji la Tanga, Omar Guledi, ametoa agizo kwa mabalozi wa nyumba  kumi na wenyeviti wa Serikali za mitaa kuwahamasisha wananchi kuweka mazingira ya usafi maeneo yao na atakaekaidi achukuliwe hatua za kisheria.

Akizindua mradi wa utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa kata ya Nguvumali na kushirikisha viongozi wa kata, Serikali za mitaa na viongozi wa dini jan, Gulledi alisema magonjwa ya miripuko na homa za mara kwa mara hazitoisha hadi jamii yenyewe itakapobadilika juu ya usafi wa  mazingira.

Alisema kufuatia kukaribia kwa msimu wa mvua ni wajibu wa kila kaya kuweka mazingira ya usafi katika maeneo yao ikiwa na pamoja na kuifanyia usafi mifereji iliyoziba ili kuwa rahisi mvua inaponyesha maji kutembea.

“Kwanza niipongeze Asasi ya Nguvumali community development of environment kwa kubuni jambo hili ambalo liko na faida ya kila mtu----mazingira yetu bado hayaridhishi na kuna kitisho cha mvua kubwa mbele yetu” alisema na kuongeza

‘Tumesikia kutoka kwa wataalamu wetu kuwa kuna mvua kubwa zinatarajia kunyesha na kama hatutaweka maeneo yetu katika usafi tutajazana mahospitalini kwa kuugua magonjwa ya miripuko” alisema Gulledi

Alisema ili kuweza kulifanikisha zoezi hilo ni wajibu wa viongozi wa dini na Serikali kuielimisha jamii kuweka mazingira ya usafi na yoyote ambaye atakuwa kikwazo awajibishwe kwa mujibu wa taratibu na sheria.

Kwa upande wake, Katibu wa Asasi ya Nguvumali Commity Development of Enviromment (NCDE), Frank Mgunda, alisema kuongezeka  vitendo vya uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji na uchimbaji wa madini katika misitu.

Alisema Asasi hiyo itafanya kampeni ya nyumba kwa nyumba kutoa elimu ya mazingira kwa kuanzia mjini hadi vijijini kabla ya msimu wa mvua kuanza kunyesha ikiwa na pamoja na vijiji vinavyoishi kandokando ya vyanzo vya maji na misitu.

“Sisi tumedhamiria hasa kutoa elimu ya mazingira kwani kama yanavyonekana bado hayaridhishi na tuko katika hatari ya kukumbwa ukame miaka ya mbele na maeneo yetu kuwa jangwa baada ya kukithiri ukataji wa miti na uchimbaji wa madini holela .

Alisema elimu hiyo itakuwa ya kila kaya pamoja na kupita katika shule za msingi na sekondari lengo likiwa ni kuhakikisha mazingira yetu yanakuwa katika hali ya kuridhisha.

Hongera Prof. Assad, Timiza Wajibu kulisaidia Taifa

Na Alhuda,Jumatano 10 Disemba 2014
Hatimaye Taifa limepata Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali-CAG. Ni Profesa Mussa Juma Assad aliyeteuliwa kushika nafasi ya ndugu Ludovick Utto ambaye amestaafu.
 
Uteuzi wa Prof. Assad umekuja baada ya nafasi hiyo kukaimiwa kwa kipindi kifupi. Tunachukua fursa hii kumpongeza mtaalamu huyu wa Mahesabu na tunamuombea kheri na fanaka katika kazi yake.
 
Mtangulizi wa Prof. Assad, Bw. Ludovick Utto, ameondoka ofisini salama. Hata hivyo, nyuma yake Ofisi hiyo imeleta sokomoko la Kitaifa ambapo aliyekuwa akikaimu ofisi hiyo aliliweka Taifa pagumu kwa kauli yake ya shaka juu ya umiliki wa fedha za Akaunti ya Escrow.
 
CAG mpya anakuja kama mkombozi wa kulitoa Taifa katika matope ya shaka ili amani ya hisia ya kila Mtanzania irejee baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma kuchafua hali ya hewa.
 
Tumefurahishwa na kauli ya CAG mpya kuwa shughuli za Ofisi yake zisichanganywe na mambo ya siasa. Ni kweli kabisa kuwa msingi wa sakata la fedha za Akaunti ya Esrow ni tafsiri mbaya iliyotolewa na PAC kuhusiana na kauli ya kaimu CAG.
 
Tunaamini kuwa, kwa sifa na uzoefu mkubwa alionao Prof. Assad, Ofisi yake itakuwa makini na matamko yake ili kuepuka kuleta mkanganyiko wowote unaoweza kuleta tafrani katika nchi.
 
Tunathubutu kusema kuwa Ofisi hii ni nyeti mno kwa usalama wa nchi. Kucheza na hesabu za fedha za nchi ambazo moja kwa moja zinagusa maisha ya wananchi ni hatari kubwa inayoweza kuifikisha nchi pabaya.
 
Hatusemi vibaya lakini laiti nchi yetu ingelikuwa na wananchi wakorofi kama wale wa Mataifa yenye vita, kitendo cha Kamati ya Zitto cha kutoa kauli ya jumla ya wizi wa fedha za Umma kingeiingiza nchi kwenye machafuko makubwa.
 
Wananchi walipandwa na hasira kuwa wakati wao wakikabiliwa na matatizo mbalimbali ya kimaisha kumbe viongozi wanaiba fedha zao. Ni dhahiri ingelikuwa Congo DRC, saa hizi hadithi ingelikuwa nyingine.
 
Kwa bahati nzuri Watanzania ni wanadamu wenye tunu ya uvumilivu. Tunawapongeza sana kwa uvumilivu wao. Subira yao imewapa nafasi ya kuchuja ukweli na uongo katika ripoti ya PAC.
 
Wananchi, kwa ujumla, wamepata changamoto ya kutumia bongo zao na kutimiza ule usemi mashuhuri kuwa ‘akili za kuambiwa, changanya na zako.’ Siku zote wanaposikia jambo, wajipe muda wa kulitafakari na kuliendea katika vyanzo mbalimbali ili kuujua undani na ukweli wake halisi.
 
Nidhamu hiyo ya matumizi ya akili ndiyo itakayokomesha tabia ya uzushi ambayo inaweza kuleta madhara kwa Taifa. Wazushi wakifahamu kuwa wananchi wana uwezo wa kufikiri kabla ya kukubali wanachoambiwa, hawatakuwa tena na nafasi ya kutengeneza uongo.
 
Kuteuliwa kwa CAG mpya ni faraja kubwa kwa kila mwananchi anayetaka kujua ukweli kuhusu fedha za nchi. Kwa upande mwingine, CAG mpya ni faraja kwa Wawekezaji ambao wangependa kuwa na uhakika na rasilimali zao.
 
Kwa umakini na uadilifu, Ofisi ya CAG itaweka bayana kila fedha ambayo inalihusu Taifa kwa maana ya fedha ya Umma na itawaweka katika hali ya usalama wa mali zao wale wanaowekeza fedha zao katika sekta binafsi.
Taarifa ya PAC na Azimio la Bunge ni tishio kwa uhai wa sekta binafsi nchini. Wawekezaji wanaweza kuogopa kuwekeza fedha zao katika miradi mbalimbali kama mamlaka za nchi zitashindwa kuainisha zipi ni rasilimali za Umma na zipi ni za binafsi.
 
Taifa lilipoteza imani ya Wawekezaji katika miaka ya nyuma kwa sababu ya hatua ya kutaifisha na kunyang’anya mali za watu binafsi. Nchi bado iko nyuma mno katika eneo la uwekezaji ilihali maendeleo yake yanaihitaji sekta hii.
 
Kutishia rasilimali za watu kwa namna yoyote ile kutadhoofisha jitihada za serikali za kujenga uchumi kupitia sekta binafsi ya uwekezaji. Tayari Mwekezaji Sethi wa IPTL ametoa kauli ya kung’oa mitambo yake baada ya Bunge kutoa kauli za kutaka kuitaifisha mitambo hiyo.
 
Ni matumaini yetu kuwa CAG mpya, Prof. Dkt. Musa Juma Assad, atatimiza wajibu wake kulisaidia Taifa kwa kuainisha fedha za Umma kwa umakini na usahihi wake.

Matangazo maalum ya kibiashara (nafasi hii inalipiwa)

زيت ارغان    Mafuta ya Arghani mafutayaarghani

Matoleo mapya ya kitabu kipendwacho cha Mkweli Mwaminifu yako tayari.Agizia mapema kutoka kwetu.

mkweli mwaminifu 

Suruali za kuvalia kanzu za kiume. na za kike

Zipo za ukubwa na rangi mbali mbali .Ni mali kutoka nchini Morocco.

Zinapatikana Kwa reja reja na kwa jumla .Ili Kujua zaidi wasiliana nasi hapa.

 

  SURUALI MOROCO      SURUALI MOROCCO

MWANGAZA KWA UMMA

Tofauti kati ya Tohara na kukeketa
Na Skh Mussa Kileo

Kila inapofika tarehe 6 Februari, Umoja wa Mataifa huadhimsha siku ya kupinga ukeketaji wa wanawake Duniani . Kwa wanaharakati wa Haki za binaadam na jinsia huiadhimisha siku hii kwa kauli mbiu mbalimbali na maazimio ya kushinikisha jamii ibadilike ili iachane na kuwakeketa wanawake.

Ukeketaji ni jambo lilioenea katika vinywa vya watu na kuandikwa na asasi mbali mbali za kijamii,na ipo haja kubwa kwa jamii ya kiislaam kulichambua jambo hili kwa kina,na ufafanuzi kama ifuatavyo:

Endelea