×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

UKEKETAJI- BY SHEIKH MUSSA KILEO

More
3 years 4 months ago - 3 years 4 months ago #2052 by Kisalazo
Ukeketaji na Khitaan (Twahara) Kwa Mwanamke
Sh. Mussa Kileo

Kila inapofika tarehe 6 Februari, Umoja wa Mataifa huadhimsha siku ya kupinga ukeketaji wa wanawake Duniani . Kwa wanaharakati wa Haki za binaadam na jinsia huiadhimisha siku hii kwa kauli mbiu mbalimbali na maazimio ya kushinikisha jamii ibadilike ili iachane na kuwakeketa wanawake.
Kuna baadhi ya watu wakiwemo Waislam, na jumuiya za haki za binaadam, haki za wanawake, Umoja wa Mataifa na Nchi za Magharibi wanaopinga kitendo hiki na kukilaani pamoja na kutafuta njia za kila namna za kuzuia na kuharamisha moja kwa moja kwa kigezo kuwa ni 'UKATILI' na kuwa unakiuka haki za wanawake. Lakini kuna tofauti kubwa baina ya kukeketa na tohara kwa wanawake , lakini kwa bahati mbaya bado tafiti zilivyofanywa hazijatenganisha tofauti hizo.Tohara ni zoezi linalofanywa kidini na ukeketaji ambalo ni zoezi la kimila yote mawili yanafanywa katika nyingi duniani ikiwemo Marekani , Afrika , Mashariki ya kati na kwengineko . Kati ya wanawake 125 mil duniani waliopata tohara au kuketwa wanatoka katika nchi 29 za Afrika na mashariki ya kati. Na watafiti wamegundua kua wengi waliofanyiwa ukeketaji hupata madhara ya Saratani , uzazi na mengineyo. Changamoto hii ndiyo inayopelekea wanaharakati wa UN na taasisi zake kukaza kamba kupinga utekelezaji wake.
Amma katika Uislam ambayo ni dini ya kimaumbile na imeelezea na kuelekeza yale yote yanayomhusu mwanaadamu kwa kila nyanja,kuanzia kabla hajazaliwa,na pale atakapozaliwa aishi vipi na atumie mfumo gani wa utawala na hatimaye atapata nini baada ya kufa kwake. Kwa yakini sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (saaw) na Swahaba zake ( r a) na wote wanaofuata mwendo wake na kuyarejesha maisha ya kiislaam kwa kuisimamisha Khilafah.
Ukeketaji ni jambo lilioenea katika vinywa vya watu na kuandikwa na asasi mbali mbali za kijamii,na ipo haja kubwa kwa jamii ya kiislaam kulichambua jambo hili kwa kina,na ufafanuzi kama ifuatavyo:
'Khitaan' (kutahir au Twahaarah ) kwa mwanamke ni jambo lisilokatazwa kwenye Uislam, na ni jambo mtu ana khiyari ya kulifanya au kutolifanya lakini si jambo linalokatazwa kama wengi wanavyodhani!
Uislam umeruhusu kutahiri ,na wala si kukeketa kunakofanywa na baadhi ya makabila na watu wengine, ni tofauti kubwa. Tutazame dalili zifuatazo na maelezo mbalimbali ili tuweze kujua ruhsa ya kufanyika khitani na njia sahihi za kuifanya;
Abu Hurayrah amesimulia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Vitu vitano ni katika fitrah(Maumbile), kutahiri, kunyoa nywele za sehemu za siri, kupunguza masharubu, kukata kucha na kunyofoa nywele za kwapa” [Imepokewa na Al-Bukhaariy, mj. 7, kitabu 72, namba 779]. Baada ya kuona Hadiyth hiyo inayozungumzia 'kutahir au Twahaarah' kwa ujumla, tuangalie Twahaarah kwa mwanamke katika sheria ya Kiislam:
Mtume (saaw) anasema, “Itakapogusa [kitakapokutana] kilichotahiriwa kimoja kugusa kilichotahiriwa kingine, basi yapasa kuoga.” [Al-Bukhaariy]. Na amesema tena Mtume (saaw): “Vitakapokutana viwili vilivyotahiriwa, basi ni wajibu kuoga.” [Ibn Maajah 611].
Kauli hizo za Mtume zinazungumzia kukutana vilivyotahiriwa viwili hapo makusudio ni sehemu ya ngozi inayokatwa katika utupu wa mwanamme na ile ya utupu wa mwanamke. Na ni ushahidi kuwa wanawake walikuwa wakitahiriwa. [Rejea Swahiyh Fiqhus Sunnah mj.1, uk.99]. Hadiyth hizo mbili ni sahihi kwa itifaki ya wanachuoni. Na vilevile kuna Hadiyth nyinginezo zenye kuweka wazi zaidi Twahaarah kwa mwanamke kama Hadiyth ya Ummu 'Atwiyah isemayo kwamba yeye alikuwa akitahiri na Mtume kusikia akasema, “Ukipunguza usimalize kwani ni pendezo kwa uso na tulizo kwa mume.” Na nyingine iliyopokewa na Imam Ahmad kwenye Musnad yake yenye maneno kama hayo, ingawa wametofautiana wanachuoni kuhusu usahihi na udhaifu wa Hadiyth hizo.
Baada ya kuona Hadiyth zenye kuthibitisha kuwepo na kuthibiti jambo hilo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ni vizuri pia tutazame nao Wanachuoni wamefahamu vipi kuhusu suala hilo:
'Khitaan ni wajibu kwa mwanamme na ni Sunnah kwa mwanamke' [Kitabu 'Mukhtasar al-Fiqhil Islaamiy, uk.381].
''Khitaan ni kukata kigozi kilichozidi hadi kichwa kitokeze kwa mwanamme na kwa mwanamke ni kukata kipande kidogo cha juu kwenye kisimi 'clitoris' .
Ieleweke wazi kuwa jambo la kutahiri kwa mwanamke ni jambo la khiyari sio lazima,na kukeketa hakufai na kumekatazwa kama tulivyoona hapo juu,
Kwa wale ambao wanachanganya tohara ya Kiislam na tohara ya kimila na kikabila inayofanywa na wengineo, yawezekana hawajui au wanafanya makusudi kutaka kuzipinga na kuzikosoa sheria zinazohusiana na Uislam kama wafanyavyo katika suala la Mirathi na Adhabu za kukatwa mkono kwa mwizi na nyenginezo.
Ni jambo ambalo si SAHIHI kulinganisha au kupinga tohara hii ya Kiislam kwa kuwa kuna wanaofanya tohara vibaya na kimakosa.
Kwani wao kigezo chao kikubwa ni baadhi ya nchi zifanyazo 'TOHARA' kimila na si Kiislam, tunasema kimila na si Kiislam, kwa sababu, nchi nyingi haswa za Afrika kaskazini na mashariki, kama vile Somalia, Chad, Sudan, Misr, Tanzania n.k, hizi wao wanachofanya ni KUFYEKA kabisa na sio kupunguza, nako kunaitwa 'UKEKETAJI'!!! Na matokeo yake kumepatikana madhara mengi kama wanawake kupata saratani, kupata taabu wakati wa uzazi, kukosa raha ya tendo la ndoa na hata wengine kufariki kutokana na kupoteza damu nyingi wakati wa kutahiri. Wao huondosha kisimi 'clitoris' chote, 'labia minora' na sehemu ya kati ya 'labia majora', pamoja na sehemu yote ya kiungo cha mwanamke kushonwa na kubakizwa tundu dogo tu. Na utaratibu huu unahitaji kumfunga miguu mtoto kwa kiasi cha wiki tatu. Na hii ndio wengine wakaita kuwa ni tendo au ada ya Ki-Firauni.
Na hivyo wafanyavyo, ni kinyume kabisa na ilivyo katika Uislam, na wala haukubaliani na njia hizo zifanywazo na wafanyao hata kama ni WAISLAM!! Kwani si taratibu zilizofundishwa na Mtukufu Mtume (saaw) .
Hivyo, kama tulivyoona, ni jambo lenye kupendezwa na si jambo la lazima. Mwenye kutaka kufanya ni bora, na asiyetaka ni khiyari yake, lakini asilaumu wala kuponda kwani ni jambo ambalo lililopo na limethibiti katika Dini na Allaah ni mjuzi Zaidi
Last edit: 3 years 4 months ago by Al-Jabri.

Please Log in or Create an account to join the conversation.

  • ABMAS
  • ABMAS's Avatar
  • Visitor
  • Visitor
3 years 2 weeks ago #2123 by ABMAS
Replied by ABMAS on topic UKEKETAJI- BY SHEIKH MUSSA KILEO
Islamic

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.412 seconds