×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

Historia, Baiolojia, Jiografia, Jiolojia ndani ya Qur’an Tukufu

More
3 years 11 months ago #1790 by Oyo
·   Qur’an inavyozungumzia miji ya kale, nyuki, milima ·        Wanasayansi wastaajabishwa na usahihi wake!   Na  S. Hussein na Wanasayansi Kosa kubwa wanalofanya binadamu wengi ni lile la kukosa udadisi kuhusu Maandiko Matakatifu ili kubaini ukweli wa maudhui yake. Kwa mfano, tayari kila mtu anazo habari kuwa Qur’an inajinadi kuwa ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu.   Kwa kuwa Mungu anatuhusu sote, ulikuwa ni wajibu wa kila mwanadamu, bila kujali, itikadi yake kuutafuta ukweli wa Kitabu hiki. Nakala nyingi za Qur’an zikiwemo za tafsiri za Kiswahili na Kiingereza zinapatikana kwa bei nafuu, na wakati mwingine kwa hidaya au bure. Kazi ilikuwa ndogo tu ya kutenga muda na kusoma.   Wajibu huu upo kwa Waislamu wenyewe ambao wameitupa Qur’an au hawaizingatii, Wakristo ambao wanaona Qur’an haiwahusu, Wahindu, Wapagani na wengineo.   Udadisi ndilo jambo lililowasukuma Wanasayansi Wakristo kama akina Moris Bucaille kuisoma Qur’an na kuuona ukweli wake, na hatimaye kuiona dini ya haki.   Wale ambao hawataki kuuona ukweli kwa sababu ya kukosa tabia ya udadisi huenda wakaja kushindwa kujibu swali Siku ya Siku; kwa nini wewe hawakuuona ukweli kuhusu Maandiko sahihi ya Mwenyezi Mungu. Kwa nini hawakudadisi?   Katika makala hii, mwandishi anasafiri pamoja na Wanahistoria, Wanajiografia, Wanajiolojia, Wanabaiolojia na kadhalika katika kuyasawiri maudhui ya Qur’an yenye uhusiano wa moja kwa moja na matokeo ya tafiti za kisayansi.                                       Historia     Mji ulioangamizwa wa Iram Katika surat al-Fajir kuna aya hii:                           ‘Iramadhaat l-‘imaad’               Wa Iram wenye majumba marefu.” (89:7)   Hakuna mwanahistoria yeyote aliyejua kuwa kulikuwa na mji wa Iram duniani kabla ya chimbachimba (ya mwaka 1973) kwenye eneo la mji wa Ebla ambako mbao za maandishi za udongo mfinyanzi zilizokutwa huko, zilithibitisha kuwa watu wa Ebla walikuwa na mahusiano ya kibiashara na watu wa Iram.  Maelezo juu ya hili yaweza kupatika katika jarida la National Geographic la Mwezi Desemba 1978 ambalo pia linasema kuwa maelezo pekee ya Iram ambayo wataalamu wa mambo ya kale na wanahistoria wamewahi kukutana nayo yamo katika Qur an Tukufu. Hivyo,  mji wa Iram haukuwa ukijulikana hadi hivi karibuni ambapo hata baadhi ya wafasiri wa Kiislamu, kwa kutojua, wameuelezea utajo wa Iram katika Qur an kuwa labda ni wa kitamathali wakidai kuwa yawezekana Iram yalikuwa ni majitu marefu na si mji! Je, laiti mwandishi wa Qur an angelikuwa binadamu, angejuaje uwepo wa mji huo wa Iram (89:7) ilihali hukuna mtu mwingine aliyejua? Hapana shaka Qur’an ni Kitabu cha Mjuzi wa mambo yote yaliyopita, yaliyopo na yajayo.                  Baiolojia Makuzi ya Mimba  Qur an (23:12-13) inaelezea makuzi ya mimba katika ile hatua isiyoonekana kwa macho matupu ndani ya tumbo la uzazi kwa maneno ya fuatayo;    ‘Na kwa yakini tulimuumba mtu kwa udongo safi kisha tukamuumba kwa tone la manii (mbegu ya uzazi) lililowekwa katika makao yaliyohifadhika, kisha tukalifanya tone hilo kuwa pande la damu, kisha tukalifanya pande hilo la damu kuwa pande la nyama, kisha tukalifanya pande la nyama hilo kuwa mifupa na mifupa tukaivika nyama kisha tukamfanya kiumbe kingine basi ametukuka Mwenyezi Mungu mbora wa waumbaji’.   Soma kwa Jina la Mola wako aliyeumba, amemuumba mtu kutoka na kitu kinachodedereka (pande la damu) (96:1-2)   ‘Kwa hakika tulikuumbeni kwa udongo kisha kwa  maniii kisha kwa kitu kinachoderereka (kipande cha damu) kisha kuwa kipande cha nyama kinachoumbika na  kisichoumbika (22:5)   Upambanuzi na ufasaha wa ajabu wa maelezo hayo ya hatua mbalimbali za makuzi ya mimba yanathibitika katika kitabu hiki mashuhuri ‘The Developing Human’cha K. Moore na T.V.N. Persaud.   Wanasayansi wengi mashuhuri wamethibitisha kuwa elimu hiyo sahihi ya hatua za mimba imepatikana kwa jamii ya Wanasayansi katika miaka arobaini tu iliyopita!    Hizo zilizonukuliwa ni aya chache tu miongoni mwa aya chungu tele za kisayansi katika Qur an. Wasomaji wanaotaka vielelezo zaidi warejee kitabu cha Maurice Bucaille ‘The Bible, the Qur an and science’, ‘Struggling to surrender’ uk 33-38 cha Jeffrey Lang na The Qur an Phenomenon cha Malik Bennabi   Vingine ni ‘The developing human’ toleo la 3 cha Keith L Moore,  ‘A brief illustrated guide to understanding Islam’ cha I.A Ibrahim, ‘The source of the Qur an’ cha Hamza Mustafa  Njozi, ‘This is the Truth’ cha Abdullah M.Al Rehail na ‘The basis of Muslim belief’ na ‘The Amazing Qur an’ vya Gary Miller na vinginevyo.   Nyuki   Katika usahihi usio wa kawaida, Qur’an imemtaja ‘Nyuki wa kazi’ kuwa ni nyuki jike. Usahihi huu wa Qur’an katika kueleza jambo hili la kimaumbile unaonekana katika aya (16:68)    ‘Na Mola wako alipomfunulia nyuki ya kwamba jitengenezee  majumba (yako) katika milima na katika miti na katika yale (majumba) wanayojenga (watu).”    Tamko la Kiarabu ‘ittakhidhi’ katika Aya hiyo ni la jinsia ya kike (maneno ya Kiarabu hutofautisha jinsia). Katika Kiarabu, sifa ya uke hutumika pale ambapo watu wote ambao neno linawazungumzia ni wanawake wakati ambapo sifa ya ume hutumika pale ambapo angalau kuna mwanaume mmoja katika kundi. Hivyo, hapa Qur an ina maana, ‘jichukulieni makazi enyi nyuki wa kike.’   Kidogo-kidogo, Sayansi ikagundua kuwa kundi  la nyuki linajumuisha  aina tatu za nyuki; Malkia wa nyuki, Nyuki wa kazi ambao hukusanya chavua kutengeneza asali na kujenga mzinga, na Nyuki dume ambao kazi yao pekee ni kumpa mimba Malkia na kisha wanauawa na nyuki wa kazi. Nyuki hawa wa kazi  wote ni majike wakiwa na viungo vya uke visivyopevuka.   Kwa hiyo, tamko hilo la kijinsia katika Qur an linaoana na ukweli kuwa nyuki dume huwa hawashiriki katika ujenzi wa mzinga au makazi ya nyuki ambayo ni kazi  ya nyuki wa kazi tu ambao ni majike.   Huo ni mfano wa usahihi wa Qur an ambao unapingana kabisa na dhana kuwa imetungwa kwa kubahatisha tu kwani, vingenevyo, kama Qur’an isingetoka kwa Mjuzi wa yote, basi palikuwa na uwezekano kuwa jinsia ya kiume ingetumika katika kuwataja nyuki wa kazi.                                   Jiografia   Milima kama ‘Vigingi’ na Vizuizi   Katika kitabu chake kiitwacho ‘Earth’, Profesa Emiritus Frank anasema kuwa milima haipo juu-juu ya ardhi bali ina vishina chini yake. Mashina haya ya chini kabisa yamekamatana na ardhi. Hivyo milima imeumbwa kama vigingi.’   Anavyosema Profesa huyo ndivyo inavyosema Qur’an kuhusu milima. Mola Muumba anasema katika Qur an ‘Je, Hatukuifanya ardhi kuwa tandiko na milima kuwa kama vigingi (vya ardhi]? [78:6-7] Kwa msingi wa maelezo hayo, neno linalofaa zaidi kuelezea milima ni neno ‘pegs’ (‘vigingi’) kwani kigingi imara zaidi cha hema ni kile kinachopigiliwa [shindiliwa] chini kabisa na neno hili ndilo lenye kufahamika zaidi na jamii ya jangwani ya karne saba iliyopokea wahyi huo.   Mwandishi wa Qur an alitoaje maelezo sahihi namna  hiyo ilahli nadharia ya ya milima kuwa na  mashina ya chini imefahamika katika ngwe ya mwisho wa karne ya kumi na tisa?   Aidha, milima inaelezwa katika Qur an kuwa inafanya kazi muhimu ya kuzuia ‘msukosuko’wa ardhi (kuyumbayumba kwa ardhi). Mwenyezi Mungu anasema, ‘Na akaweka katika ardhi milima ili (ardhi) isiyumbeyumbe nanyi (16:15).   Halikadhalika, nadharia ya sasa ya ‘plate tectonics’ inasema kuwa milima inafanya kazi kama vizuizi vya matabaka ya mgongo wa ardhi ya sayari yetu inayokuwa mwendoni wakati wote kutokana na sayari hii kujizunguusha kwa kasi. Vizuizi hivyo ni muhimu kwa ajili ya kupunguza athari za  mitetemeko ya ardhi ambapo matabaka hayo hogongana. Elimu hii juu ya kazi ya milima ilianza kufahamika mwishoni mwa miaka ya 1960 Umbile duara la Dunia Katika aya kadhaa [7:54 36:37 31:29], Qur an inatutaka tutafakari mabadiliko ya usiku na mchana kama ishara itokanayo na Mola Muweza wa yote. Kwa mfano, aya hii inasema huufunika usiku juu ya mchana na huufunika mchana juu ya usiku (39:5). Kitenzi cha Kiarabu ‘kawwara’ maana yake  ni kuviringisha au kufungiliza  na hapa kina maana ya kuviringisha kitu katika kitumviringo (duara) kama vile kuviringisha kamba ya katani kwenye burungutu lake au kuviringisha kitambaa cha nguo kichwani.   Kutokana na umbile la sayari ya dunia hivyo ndivyo inavyotokea ambapo upande wa tufe ulio usiku hufuatiwa na upande wa tufe ulio mchana. Daima huviringana katika sehemu yake ya juu. Mtu atazamaye kutoka angani, akiiangalia dunia kutoka mbali, ataona ule uonekano wa mviringano wa usiku na mchana katika kuizunguuka sayari kwa mwendo wa kubiringita pale atazamapo kutoka pembe ambayo mwanga wa mchana hutokeza ndani ya usiku na halafu usiku kutokeza ndani ya mwanga wa mchana.   Hii ni kutokana na mzunguuko wa dunia na mahali linapotua jua kwa usawa na dunia. Hivyo, matumizi ya maneno katika Qur an kuhusiana na jiografia hili ni barabara kabisa. Kutanuka kwa ulimwengu   Kutokana na utafiti wa mpangilio wa magimbo (galastic spectrum),  Wanasayansi wamethibisha hivi karibuni tu kuwa ulimwengu unatanuka. KatikaQur’an (51:47), tunasoma hivi; ‘Na mbingu tumezifanya kwa kudra (yetu) kwa hakika Sisi ndio wenye Uweza’    Neno ‘samaa’ la Kiarabu lina maana ya mbingu yaani maumbile makubwa ya ulimwengu na neno ‘musi’un’ ni kitenzi cha wingi cha wakati uliopo kitokanacho na kitenzi ‘awsa’a’ ambacho kina maana ya kupanuka (kujitandaza, kutanuka). Ukweli huu unathibitika katika andiko la ‘Stephen Hawking’ ‘A brief history of time’                                             Mripuko mkubwa   Katika Qur an (21:30) na (21:30), tunasoma “Je hawakuona wale waliokufuru ya kwamba mbingu na ardhi vilikuwa vimeambatana kisha tukaviambua na tukafanya kwa maji kila kitu kilicho hai. Je, hawaamini?   Kwa muda mrefu sasa Wanasayansi wamekuwa wakisema kuwa ulimwengu mwanzoni ulikuwa fungamo moja lenye ukubwa  usiokadirika ambalo baadae ukapasuka katika vipande vingi baada ya mripuko mkubwa mno ulioitwa ‘big bang’.   Aidha, imethibika kuwa seli za uhai zaidi hujengeka kwa maji ambayo ndiyo kiini muhimu cha uhai kama tujuavyo. neno ‘maa’a’ kwa kawaida hutafsiriwa kama ‘maji’ lakini lenyewe lina maana ya angani , baharini na kwa jumla aina yoyote ile ya maji. Kwa hiyo, aya iliyonukuliwa hapo juu inakubaliana kabisa na tafiti za kisayansi.   Jeffrey Lang naye anasema kuwa jambo la kusisimua zaidi ni kuwa changomoto hii kwa wasioamini ilitolewa katika karne ya saba. Twaweza kujiuliza ni watu gani wasioamini wanaozungumziwa hapa?   Kwa hakika, kwa watu wa zama za Muhammad wahyi huu ulikuwa na mambo mengi yenye mvuto lakini swali lililoulizwa lisingekuwa na maana sana kwao isipokuwa labda kama pangelikuwa na elimu ya mithiolojia kule Arabuni mbayo wangelihusisha na swali hilo.   Elimu hiyo haikuwepo. Sasa, je, swali hilo la Qur’an lilikusudiwa kwa watu wa baadae kabisa ambao ndio wangekuwa na maarifa ya tafiti za kisayansi?   Kwamba, wakati fulani, huu ulimwengu haukuwa chochote ila wingu tu la moshi (Qur an 41:11). Ufafanuzi juu ya ulimwengu kuumbika kwa wingu la moshi ndiyo kanuni ambayo haipingani na elimu ya sasa ya maumbile.    ‘Kisha Akazielekea mbingu na zilikuwa moshi (dukhaan) [41:11].’ Neno ‘moshi’ ndilo lifaalo zaidi kuelezea mseto wa gesi nzito mno ya moto-moto usiopitisha mwanga ambao ulikuwepo kabla ya ulimwengu kupasuka.   Nyota mpya ambazo hadi sasa bado zinajiunda, kama wasemavyo wataalamu wa mambo ya anga, zinatokana na mapande ya huo ‘moshi’ wa awali. Haiingii akilini kabisa kuwa mtu wa karne ya saba kule Arabuni angeliweza kujua habari kuhusu mwanzo huu wa ulimwengu!   Ni wanasayansi wangapi bora na mahiri wa hivi leo waliolazimika kuvumbua hakika hizo kwa msaada  wa vifaa vya teknolojia ya hali ya juu, setilaiti, darubini,viona mbali na kompyuta na kwa muda gani wamefanya kazi hiyo?   Je, kweli inaingia akilini kuwa mwanadamu yoyote wa zaidi ya miaka 1400 iliyopita angeweza kuandika kitabu chenye maelezo hayo seuze mtu ambaye hakuwa na elimu yoyote? Muhammad ambaye hakujua kusoma wala kuandika angewezaje kujua mambo ya kisayansi ambayo ulimwengu umeyajua katika karne za karibuni tu tena kwa msaada wa vifaa vya kisasa?    Ingawaje udhaifu wa mwanadamu kuyajua maajabu na mchangamano wa maumbile unaelezwa katika Qur an (67:3-4), hata hivyo, wahyi unataja mambo mbalimbali ya kimaumbile kwa namna ya kuwachagiza wanadamu kutafiti na kuthibisha kisemwacho na Mwenyezi Mungu.   Dkt Maurice Bucaille alihitimisha utafiti kwa maneno haya: Kwa kuzingatia hatua  ya elimu katika zama za Muhammad, haiingii akilini eti maelezo mengi namna hiyo ya Qur an ambayo yanashabihiana na sayansi yawe yameandikwa na mtu!

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.398 seconds