×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

Maajabu ya Uhandisi usio na kasoro: Nini kinachofanya Miti iwe imara?

More
3 years 10 months ago #1836 by Al-Jabri
Miti huwezaje kuhimili upepo mkali na kubaki wima kwa mamia ya miaka? Ni Sifa gani za kimaumbile zinazofanya miti iwe imara? Je, mizizi, kigogo na majani ya miti ndiyo yanayofanya mti uwe mgumu?

Miti, ambayo ni moja ya maeneo muhimu ya utafiti katika ulimwengu wa sayansi, hufanya kazi ya kuwapa mwongozo wanasayansi katika mambo mengi ambapo vipengele vya maumbile yake vingali bado vinavumbuliwa.

Mojawapo ya sifa za kuvutia mno za miti ambazo zimevuta zaidi mazingatio ya wanasayansi ni magome yao ambayo ni uhandisi wa kustaajabisha. Gome ambalo huunda sehemu kubwa ya mti bado halijafahamika kikamilifu licha ya teknolojia ya hali ya juu iliyotumika na utafiti mkubwa uliofanyika.

Umbile hili ambalo linaupa mti nguvu na mwonekano wa urembo sio tu linasaidia kubeba uzito wa majani na matawi yote bali pia huukinga mti na hali za hewa mbalimbali kama vile pepo na vimbunga na husaidia miti kusimama wima kwa mamia ya miaka. Kinacholeta ugumu-gumu katika magome ya miti ni mpangilio wa seli zao na sifa za maumbile yao.

Seli katika Magome ya Miti hupangiliwa kuleta Ukakamavu

Zaidi ya asilimia 90 (90%) ya seli za miti hujengeka kwa virija vidogo-vidogo ambavyo hugandamana kimoja juu ya kingine kwa kubanana sana na hukitambaa kigogo cha mti na kuyatambaa matawi.

Hii husaidia maji kusafirishwa hadi kwenye majani na wakati huo huo huitia ugumu miti. Kama inavyofahamika, miti, kwa ujumla, hupinzana na nguvu za nje kama vile upepo. Upinzani huu kwa ujumla, huonekana kwa jinsi mti unavyopinda (unavyonesa) kukabiliana na upepo.

Hata hivyo, bila kujali mti unapindia upande gani, bado hunesa pamoja na seli na magamba ya mti. Kadri sehemu iliyobonyea ya chembechembe ndefu na nyembamba za seli zilizopangiliwa sanjari zinavyozuia shinikizo kama mhimili ndivyo sehemu iliyobinuka ya seli inavyonyooka kama kamba na kuhakikisha kuwa mti unasimama imara katika kukabiliana na upepo kwa kuufanya upinde na kunyooka dhidi ya nguvu za nje.

Isitoshe, maumbile yake yanayofanana na mrija ni magumu zaidi kulinganisha na maumbile yaliyokaa sawa. Wahandisi wanaweza kuongeza uimara wa majenzi kwa kutumia sifa hizi za kimaumbile, ambazo ni ishara ya Ujuzi uliotukuka wa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu.

Safu zilizofungamana za Seli ndizo zinazoongeza Uimara

Kuna maduara yaliyofunganafungana ndani ya kigogo cha mti, ili kuongeza uimara wa seli zilizopangika sanjari na mti ili huulinda mti usikatike. Haya huhakikisha kuwa mti unasimama pamoja na seli zilizo sambamba, kwa sababu kama kungelikuwa na athari katika seli zilizo sanjari na mti, basi maduara hayo yangeonesha upinzani kwa upande mwingine wa nguvu ya nje. Matabaka haya ndiyo yanayounda asilimia 80 ya uzito wa utando wa seli, na huu ndio upande hasa unaovuta uzito halisi.

Pale kunapokuwa na athari, upande huu hupasuka kutoka kwenye seli zinazouzingira na kuvunjikia ndani na kunyonya nishati ya athari hiyo. Kwa njia hii hata kama miti huwa na mpasuko mrefu, bado umbile la mti hubakia imara.

Hivyo, hata kama kuna mpasuko, bado mti una nguvu za kubeba kiasi fulani cha uzito. Umbile hili la mti ndilo linalouzuia mti usidondoshwe chini kwa uzito wake wenyewe. Hii hujenga umbo maalum ambalo huufanya mti uwe imara na uweze kuinama na kunyooka.

Kuna akili yenye ubora wa hali ya juu ambayo ndiyo inayoipa miti sifa zote ilizonazo. Akili hiyo ni Mwenyezi Mungu ambaye ni Mfalme wa walimwengu na ambaye anamiliki vitu vyote. Hii inabainishwa katika aya hii: “Vyote) vilivyomo mbinguni na ardhini ni Vyake, na vyote humtii Yeye.” (30:26)

Umbile la Utando wa seli ndilo linaloleta Nguvu na Uimara wa Mti

Kila kipengele katika umbile la mti-kuanzia wembamba wa matabaka yao, msongamano wao, idadi na mpangilio wa chelewa zake, vitu vilivyomo ndani-huumbwa ili kuhakikisha uimara.

Utando wa seli nao pia umeumbwa kutokana na dutu imara ambayo huongeza sifa ya uimara wa mti. Hii hujumuisha nyuzi ndogondogo za seli. Hizi hufanya gome liwe imara zaidi na kulikinga lisikatike-katike.

Umbile hili huufanya mti uwe mgumu zaidi kuliko hata kioo cha utembo (fiberglass). Kwa hali hiyo, maboti yanayotengenezwa kwa mbao ndiyo yenye nguvu ya kuzuia mawimbi makubwa kuliko utembo.

Kigogo cha Mti kina umbile kamili la mti

Haiba ya jumla ya mti ni ile ya matawi na majani yanayotokea katika kigogo kimoja. Mwenyezi Mungu ndiye aliyekiumba kigogo kama mhimili mmoja wenye nguvu ili kuzuia usiinamie chini. Kutokana na usanifu huu bora kabisa wa maumbile, mti unaweza kubeba majani na matawi yanayoujazia uzito juu yake.

Zaidi ya hivyo, kigogo huhitaji kigogo kiwe kimoja na imara ili kuhimili mneso wa kuyumba unaotokea wakati wa upepo mkali. Hii ni kwa sababu kigogo kimoja kipana ndicho imara na chenye nguvu zaidi ya kuhimili misukosuko kuliko vigogo vingi vyembamba.

Mola wetu ndiye aliyeupa mti uimara kupitia umbile la kigogo. Sehemu ya kigogo ambayo iko jirani zaidi na ardhi ndiyo kubwa zaidi. Kwa namna hii, sehemu ya mti ambayo ndiyo yenye nguvu zaidi za kuzuia misukosukuso ya nje huwa imara zaidi kadri mti unavyotanuka.

Mwenyezi Mungu ni Yule anayeumba Gome la Mti na kulipa sifa isiyo na mfano

Moja ya dutu kuu za kemikali zinazounda umbile la mti ni “Lignocellulosex.” Dutu hii inajumuisha mseto wa “lignin” na “cellulose” ambayo ndiyo inayofanya mti uwe mgumu.

Pale umbile la kemikali la mti linapotafitiwa, ndipo inapoonekana kuwa lina asilimia 50 ya cellulose, asilimia 25 ya hemicellulose na asilimia 25 ya lignin. Pale mifumo ya kemikali ya dutu hizi inapochunguzwa, viasili vitatu vya kikemikali hukutwa katika muundo wao: navyo ni haidrojeni, oksijeni na Kaboni.

Viasili hivi vya Haidrojrni, oksijeni na kaboni ndiyo matofali ya kujengea mamilioni ya dutu katika maumbile. Hata hivyo, vitu hivi vitatu hujumuika pamoja na kuunda “lignocellulosex” katika umbile la mimea ikiwa ni maajabu ya Mwenyezi Mungu.

Hata kama wanasayansi wanazo ghafi hizi, bado hawawezi kutengeneza dutu hii maalum kwa njia za bandia katika maumbile ya mimea. Ijapokuwa wanaweza kirahisi kupata viasili hivi vitatu ambavyo, kwa kawaida, hupatikana katika maumbile na mbele yao ipo sampuli ya mti, bado wanasayansi hawawezi kuunda hata kipande cha mti kwa njia za bandia

Hata hivyo, miti yote ambayo tunaiona huku na kule hujumuisha oksijeni na kaboni katika hewa, maji na mwanga wa jua, na imekuwa ikitengeneza mseto huu kwa mamilioni ya miaka tangu ilipoanza kuwepo duniani. Vipengele katika gome la mti vyatukumbusha sifa bora za maumbile ya miti kama Mwenyezi Mungu anavyotudokeza katika Surat Al-Waqia:

“Je! Mnauona moto ambao mnauwasha? Je! Mti wake mmeuumba nyinyi au Sisi ndio tuliouumba? Sisi Tumeufanya kuwa ukumbusho na manufaa kwa viumbe. Basi litukuze jina la Mola wako aliye mkuu.” (56:71-74)

Sifa hii ambayo Mola wetu kaiumba ndani ya magome ya miti, bado haijaweza kusanisiwa kwa mchakato wowote unaofahamika wa kisayansi. Gome ni laini kiasi cha kuweza kubeba majani yake, lina nguvu ya kutosha kuzuia miti kuanguka kutokana na uzito wao, kukatika au kung’olewa na upepo mkali, na ni jepesi na gumu kiasi cha kuweza kuzuia mti usishindwe kukabiliana na nguvu za nje.

Sifa hii ya mti inatokana na hikima iliyotukuka ya Mola wetu ambayo inajidhihirisha katika mpangilio wa seli na sifa za utando wa seli zenye kuonekana kwa jicho la darubini.

Hakuna kitu kilichotengenezwa na mwanadamu ambacho kinaweza kuwa na sifa za ugumu, nguvu, ulaini na wepesi ambazo mti unazo zote kwa wakati mmoja. Matofali na maplastiki, chuma ni vigumu lakini vizito sana. Mti ni ajabu ya kweli ya maumbile pale unapolinganishwa na vitu hivi.

Ukweli kwamba hata seli moja inayounda mti haiwezi kuigizika kwa njia za bandia una maana kuwa mwanadamu hawezi kukabiliana na miti licha ya uwezo wake wote.

Kwamba sifa za miti zingeliweza kujaza majuzuu na majuzuu ya vitabu, na kwamba sifa zao za ajabu huwavutia wanasayansi-zote hizi zinadhihirisha ilimu na hikima iliyotukuka katika maumbile ya miti. Ilimu na hikima hii ambayo inadhihiri katika miti ni ya Mwenyezi Mungu ambaye kaumba viumbe vyote na kukimiliki kila kitu.

Mfumo wa Mizizi ya Miti, Matawi na Majani huzidisha Uimara wao

Sifa za Mizizi

Miti huvifikishia ujumbe kigogo na mizizi yao kuhusu athari za upepo mkali na vimbunga. Mola wetu ndiye aliyeumba mifumo ya mizizi ya miti kwa namna ambayo huushikamanisha mti na ardhi barabara.

Kama inavyofahamika, sehemu kubwa ya mizizi huundwa na mzizi mkuu. Huu ndio unaoshikamanisha mti na udongo kama vile nguzo zinavyokamatia hema ardhini.

Mizizi ya pembeni-pembeni inayotokana na mzizi mkubwa yenyewe hufanya kazi kama kamba zinazosaidia kushikilia hema, na mizizi hii ya pembeni ndiyo inayozuia mzizi mkuu usuyumbishwe.

Kadiri mti unavyozeeka, mizizi mikubwa huanza kupoteza nguvu yao. Hata hivyo, Hikima iliyotukuka ya Mola wetu hudhihirika tena hapa. Mizizi ya ziada huanza kuota ili kuutia nguvu zaidi mti.

Mizizi hii ya ziada huenda mbali zaidi chini na huwa mizito na husababisha mizizi kupata matawi na kujenga nyavu-nyavu. Kwa kuwa hakuna mzizi utakaoweza wenyewe kuushikilia mti mahala pake, vizizi vidogo-vidogo vinavyoota kutokana na mizizi ya ziada ndivyo vinavyohakikisha kuwa mti unashikama na udongo barabara.

Nguvu ya Matawi na Majani ambayo hupunguza Nguvu ya Msukosuko ya baridi.

Kwa kuwa matawi na majani ya mti ni membamba zaidi, basi huwa na nguvu ndogo ya kuleta msukosuko juu ya mti kuliko nguvu ya kigogo, na hili ndilo linalofanya mti uweze kujishika kwa usalama ardhini.
Na Harun Yahya, Mfasiri Abu Kawthar
Kutokana na sifa hii ya maumbile, nguvu ya upepo mkali juu ya mti wa msonobari wenye urefu wa mita tano juu huwa ndogo kwa theluthi nzima. Minazi huweza kuhimili upepo mkali zaidi kutokana na sifa hiyo. Miti inayodondosha majani yao hupunguza zaidi nguvu ya upepo kwa kuyumba zaidi dhidi ya vimbunga vyenye upepo mkali.

Na miti isiyodondosha majani yao hupunguza nguvu ya msukusuko kwa kuwa na majani ambayo yanabana matawi. Kama ilivyokwishaelezwa, Mwenyezi Mungu ndiye aliyeumba mifumo hii thabiti kwa ajili ya miti kushikamana na ardhi barabara. Mwenyezi Mungu ndiye anayevilinda viumbe vyote na Mwenye Uweza Mkubwa, ndiye Muumba wa viumbe vyote.

“Je! Hawazioni mbingu zilizo juu yao! Tumezijengaje na Tumezipambaje, wala hazina nyufa. Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna. (Yawe hayo) ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mtu mwelekevu.” (50:6-8)

Ukinyoa upara usiokote madoriani

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.399 seconds