×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

Kwa nini Wanasayansi wanashindwa kumuona Mungu?

More
3 years 5 months ago #2022 by Oyo
Na Dkt. Kamumpuri, Mfasiri S. Hussein

“Tutawaonesha Ishara Zetu katika ulimwengu na katika nafsi zao hadi waone wazi kuwa huu ni ukweli. Je, haitoshi kuwa Mola wako anaona vitu vyote?’ (41:53).

Profesa Sharon Bagley alichapisha makala moja ya kuvutia katika Jarida la Newsweek International la Julai 27, 1998. Makala hii ilikuwa na kichwa hiki, “Science finds God” (“Sayansi yamuona Mungu”).

Katika makala yake hiyo ndefu, Prof. Bagley amewapambanulia wasomaji wake wengi wa Magharibi kuwa Sayansi, kwa muundo wake, inakiri na kutambua kuwa yupo Mungu Muweza wa Yote.

Profesa huyu kamnukuu Allan Sandage, mwanasayansi mashuhuri ambaye, kwa kinywa kipana, anadai kuwa mafanikio ya sayansi ya leo yanaonekana kupingana na dini na kudhoofisha imani juu ya Mungu.

Lakini kwa upande wa Wanasayansi ambao idadi yao inazidi kuongezeka, vumbuzi hizo hizo zinatoa uthibitisho wa jambo la kiakili la kumtambua Mungu.

Prof. Sandage anazidi kusema, “it was my science that drove to a conclusion that the world is much more complicated than can be explained by science. It is only through the supernatural that we can understand the mystery of existence

Yaani, ‘Ni elimu yangu ya sayansi iliyonisukuma kufikia hitimisho kuwa ulimwengu ni mkubwa zaidi kuliko vile unavyoweza kuelezewa na Sayansi. Ni kwa njia ya Nguvu za Maumbile tu ndipo tunapoweza kukielewa kitendawili cha uhai.” Labda kwenye mabano tuongeze maneno kuwa (hiyo Nguvu anayoihitaji mwanasayansi huyu ni mafundisho ya Mitume kwa njia ya ufunuo).

Kukubali ukamilifu wa Kazi ya Mungu

Almarhum Prof. Muhammad Abdus Salaam alikuwa mwanasayansi mashuhuri katika jamii ya Kimataifa. Alipata nishani ya Nobeli kwa kazi yake ya fizikia mwaka 1979.
Alikuwa Rais wa Taasisi ya Sayansi Ulimwenguni na alikuwa Mwasisi na Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Nadharia ya Fizikia mjini Trieste, Italia. Alikuwa Mjumbe mtendaji wa Vyuo Vikubwa vya Taaluma Ulaya ikiwemo Academia Nazionale dei Lincei.

Katika dhifa moja adhimu iliyoandaliwa na Nobel Foundation na Royal Academy of Science kwa heshima ya watunukiwa wa nishani ya Nobeli, Prof Abdus Salaam ambaye pia alikuwa akipokea Nishani ya Nobeli katika fani ya fizikia, alisoma aya ifuatayo kutoka Surati Mulk ya Qur’an mbele ya hadhara ya wanasayansi 12,000 mashuhuri duniani.

“Ambaye ameumba mbingu saba zilizo tabakatabaka (moja juu ya nyingine); huoni tofauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema. Hebu rudisha macho yako (uzidi kutazama), je unaona kosa? Tena rudisha macho yako mara nyingi zaidi, jicho lako litarudia kuwa limehizika na kuchoka.” (67:3-4).

Baada ya kusoma aya hiyo ya Qur’an, Prof. Salaam alisema hivi;

“Hii hasa ndiyo imani ya wanafizikia wote: Kadri tunavyotafiti zaidi ndivyo mshangao wetu unavyozidi kuwa mkubwa na ndivyo uoni wetu unavyopigwa na mwanga mkali wa kuchoma macho na kufifiliza nuru ya macho.

Mpangilio na uwiano madhubuti katika maumbile makubwa ya angani, yaonekanayo na yasiyoonekana, yanayofuata kanuni sahihi za fizikia unathibitisha Upweke na Mamlaka Kuu ya Muumba Mmoja.

Hakuna mwanya wa kukwepea wala hakuna kizuizi. Hii ndiyo Tauhiid iliyokubaliwa na wanasayansi wote mashuhuri duniani.

Wanasayansi huona vitu visivyoonekana lakini wanashindwa kumuona Mungu!


Mungu haonekani kabisa lakini anaonekana waziwazi kabisa kwa wale wanaojua kuwa Mungu anajidhihirisha katika Ishara Zake na Maajabu Yake. Kila kiumbe duniani ni darubini ya kumuonea Mungu. Kila jambo katika maisha yetu ni kichocheo cha akili ambacho kwacho twaweza kumuona Mungu.

Kuona vitu kwa macho ya upofu:

“Nyoyo wanazo lakini hawafahamu kwazo, na macho wanayo, lakini hawaoni kwayo, na masikio wanayo lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama; bali wao ni wapotevu zaidi. Hao ndio walioghafilika.” (7:179).

Katika aya hiyo, Qur’an inauelezea wazi mtazamo potofu wa Wanasayansi wanaomkana Mungu ambao wana macho makali yanayoweza kuona vijichembe vya atomu visivyoonekana kwa macho matupu lakini wao hao hao wanapinga kuwepo kwa Mungu.

Yafuatayo ni maajabu ya kazi ya kuumbaji ya Mwenyezi Mungu ambayo wanasayansi wenyewe wameyavumbua. Vumbuzi hizi za ajabu zilizofanywa na wanasayansi wanaomkana Mungu zinabainisha kile kile ambacho Qur’an imekizungumza juu yao, kwamba wana bongo za kujua mambo mengi na macho makali ya kuona vitu vingi lakini hawatafakari wala hawaoni-Hawazingatii.

Wanasayansi wamepima ukubwa wa chembe za elektroni zisizoonekana kwa macho matupu ambazo zinajizunguusha katika chembe ndogo mno ya maada isiyoonekana. Uzito wa elekroni moja ni Gramu 0.0000000000000000000000000009.

Mwili wa binadamu una zaidi ya seli (chembechembe hai) 10, 000,000,000,000 (milioni 10 milioni ). Yaani milioni kumi ziwe milioni. Kila seli (chembe) katika mwili wako iko hai kama ulivyo hai
wewe mwenyewe.

Inapumua, inakula chakula, inafanyiza haja,
inakuwa, inazaa, inafanya kazi mahususi na hatimaye hufa. Mabilioni
ya seli hufa kila baada ya dakika moja na papo hapo nafasi zao hujazwa na seli nyingine mpya.

Kama DNA yote katika mwili wako ingekunjuliwa na kunyooshwa basi ingefika hadi pale lilipo jua kwa takribani mikunjo 3000. (Kwa kuelewa zaidi maana ya mikunjo, angalia ukunjaji wa burungutu la kamba. Unakunja na kurudia)

Wastani wa uzito wa ubongo wa mwanadamu ni kilo 1.4 na una takribani seli (chembe hai) bilioni 100 na kuna idadi kubwa zaidi ya glia. Kazi ya seli hizi ni kusambaza taarifa za neva. Glia nayo hufanya kazi nyingi muhimu. Kila seli ya neva imepangiwa na Mwenyezi Mungu kufanya kazi yake maalum.

Moyo wa binadamu husukuma (hupampu) lita 4.7 za damu mwilini kila dakika. Kwa siku moja, moyo hupampu takribani magaloni 2,000 (sawa na lita 7,600) za damu.

Katika mwaka wa 70 wa uhai wa mtu, moyo unakuwa umepampu magaloni milioni 51 (sawa na lita milioni 193) za damu na moyo huo unakuwa umedunda mara bilioni 2.5. Mtambo huu madhubuti hujengeka kikamilifu baada ya majuma manane tu ya kushika mimba wakati mimba ikiwa na urefu wa nchi moja tu.

Katika mwili wako kuna takribani lita 4.4 za damu ambayo inajumuisha wastani wa seli nyekundu, red blood cells 5000,000 na seli nyeupe white blood cells 5,000 hadi 10,000

Retina ndogo-tabaka la ndani la mboni ya jicho lina takribani vijeledi (rods) milioni 160, 000,000 na koni (cones) 6,000, 000. Zinakadiriwa molikuli 10,000,000 za rhodopsin kuwemo katika kila kijeledi kimoja kati ya hivyo vijeledi 160,000,000 katika jicho lako.

Kipanga anakadiriwa kuwa na koni 600,000,000 zilizosindikwa katikati ya retina, zikimpa ndege huyo uoni mkali wa macho mara nane ya ule wa binadamu.

Mapafu yako yana vifuko vya hewa 300, 000,000. Figo mbili nzima zina jumla ya nephroni 2,000,000 ambazo huchuja lita 190 au galoni 50 za damu kila siku.

Mgofu (Skeletoni) una jumla ya mifupa 208 inayoutia nguvu mwili. Kuna mifupa 27 katika kila mkono mmoja. Ni miyepesi na imara zaidi ya mara tano ya kipande cha chuma chenye uzito wa zaidi ya mara tano ya mfupa. Kuna jumla ya misuli 639 katika mwili wako.

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.511 seconds