×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

Maumbile wanayoweza kujitokeza nayo Majini

More
4 years 2 months ago #1746 by Al-Jabri
 Na Sheikh. Prof. Umar al-Ashqar ·        ‘Jini upepo’ ndiye anayemrusha juu ‘Mwanga’ na Ungo!  Wakati mwingine Shetani huwa hawaendei wanadamu kwa njia ya uchochezi wa ndani ya nafsi. Badala yake, hujitokeza kwao kwa umbile la binadamu; sauti yake yaweza kusikika bila mwili wake kuonekana. Au wakati mwingine huweza kujitokeza kwa umbile la ajabu-ajabu. Wakati mwingine Majini hujitokeza mbele ya binadamu na kuwafahamisha kuwa wao ni Majini. Wakati mwingine hudanganya kuwa wao ni malaika. Na wakati mwingine hujiita “watu wasioonekana”  ambapo nyakati nyingine hudai kuwa wao wanatoka katika ulimwengu wa mizimu. Mambo yote haya yamesimuliwa na watu katika zama zote. Wakati mwingine Majini huzungumza moja kwa moja na mtu, na wakati mwingine huzungumza kupitia mtu wa kati au mtabiri, wakitumia ulimi wa mtu huyo kwa muda. Na wakati mwingine Majini huweza kuwajibu binadamu kwa  kuandika. Mashetani wa kijini huweza kufanya mengi zaidi ya hayo. Wamefahamika kuwa wao ndio wanaowarusha watu kwa njia ya upepo kutoka sehemu moja hadi nyingine. Watu wanaposikia Mwanga huruka na ungo,  basi ni Shetani wa kijini anayewarusha. Au Mashetani wa kijini wanaweza kumletea mtu kitu anachokitaka. Lakini mambo haya hufanywa na waovu wasiomwamini Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola wa Mbingu na Ardhi au watu wanaotenda dhambi. Mara nyingi, watu hao hujitokeza kama wacha Mungu kabisa lakini kumbe ni watu wapotevu na mafisadi. Watu wengi wa zamani na wa sasa wamesimulia mikasa ya aina hiyo na hawawezi kupingwa kwani taarifa za matukio hayo zinatoka sehemu nyingi na ni mutawaatir (za mwendelezo wa kizazi hadi kizazi). Miongoni mwa matukio yaliyosimuliwa ni lile aliloliandika ibn Taimiya kuhusiana na Bwana mmoja aliyeitwa al-Hallaaj: “Bwana huyu alikuwa mchawi, na wakati mwingine mashetani wa kijini walikuwa wakimtumikia. Alikuwa na wafuasi wake fulani juu ya mlima wa Abu Qabis. Wafuasi wake walimuomba awaletee sahani ya peremende. Akaenda mahali fulani jirani na mlima  na kuleta sahani hiyo ya peremende. Baadae ikabainika kuwa peremende hizo ziliibwa dukani nchini Yemen ambapo Shetani wa kijini ndiye aliyezichukua na kuzipeleka mahali hapo.” Na ibn Taimiya kaandika hivi: Mbali ya al-Hallaj, mambo kama hayo yamewatokea wengi wanaoishi maisha ya uovu.Tunawajua watu wengi tu wa zama zetu na wa zama nyinginezo. Mfano yule mtu ambaye hivi sasa anaishi Damascus (yaani mtu huyo aliishi Damascus enzi za akina ibn Taimiya). Shetani alikuwa akimbeba mtu huyo kutoka milima ya Salihiya hadi kwenye vijiji vya Damascus. Mtu huyo alikuwa akibebwa hewani hadi kwenye madirisha ya majumba na kuingia ndani huku watu wakimuona.   Alikuwa akija nyakati za usiku kwenye lango la Small Gate (moja ya malango sita ya Damascus enzi hizo) ambapo yeye na wafuasi wake walikuwa wakionekana hapo. Bwana huyo alikuwa ni mmoja wa watu waovu kabisa. Mmoja wao alikuwa katika gereza lenye ngome katika mji mmoja ulioitwa Al-Shahida. Mtu huyu alikuwa akienda kwa upepo hadi kwenye kilele cha mlima na watu walikuwa wakimuona. Shetani ndiye aliyekuwa akimbeba. Mtu huyu alikuwa  mwizi wa kupora barabarani Watu wengi wa aina hiyo huwa ni vinara wa uovu. Mmoja wao alikuwa anaitwa al-Barsha Abu al-Majib. Hema lake lilikuwa likikitwa kwa muda kwa ajili yake usiku wa giza nene. Chakula kilitayarishwa kwa utaratibu wa kafara. Hawakutaja jina la Allah wala hawakuwa na kitabu chochote chenye jina la Allah. Kisha al-Barsha akawa anapaa juu hewani. Wenziwe wakamtazama na kumsikia akizungumza na shetani, na wakamsikia shetani akizungumza naye. Mtu yeyote aliyecheka-cheka au yeyote aliyedokoa chakula, alipigwa bila kujua nani aliyempiga. Kisha Shetani akawa anawafahamisha mambo waliyokuwa wakiuliza. Kisha akawaamuru watoe kafara ya ng’ombe, farasi au mnyama aliye sawa na hao. Akawaambia wamnyonge mnyama huyo na wasitaje jina la Mwenyezi Mungu juu yake. Walipofanya hivyo, basi na yeye akawatimizia mahitaji yao.” Ibn Taimiya pia alimtaja Sheikh mmoja wa Kisufi. Sheikh huyo alisema yeye mwenyewe kwamba alikuwa na tabia ya kuzini na kuwalawiti watoto wa kiume. Akasema, “mbwa mweusi mwenye mabaka mawili meupe baina ya macho yake alikuwa akinisemesha, ‘fulani bin fulani atakuja kwako kuhusiana na kiapo alichokula kwa jina lako na nimetimiza haja zake kwa niaba yako.’  Kisha huyo fulani bin fulani akaenda kwa Sheikh kukizungumzia kiapo hicho ambapo sheikh huyo kafiri  tayari alishakuwa anajua jambo hilo na akamfahamisha mtu huyo hata kabla mwenyewe hajalisema. Na ibn Taimiya pia akasimulia kutoka kwa mtu huyo, “kama mtu yeyote ananitaka nimbadilishie kitu chochote kama vile gundi, basi nitapayuka hadi nipagawe na baada ya hapo, nitaiona gundi mkononi mwangu au mdomoni mwangu na nisijuwe nani aliyeiweka.” Na akasema, “Nilipotembea nyakati za usiku, nilikuwa na bakora nyeusi iliyoniangazia mwanga mbele yangu.” Ibn Taimiya akasema kuwa Sheikh huyo alipotubu na kuanza kuswali, kufunga na kuepuka mambo ya haramu, mbwa huyo mweusi akamkimbia, na hakuweza tena kutengeneza gundi wala kitu kingine chochote kile.” Ibn Taimiya pia kamtaja sheikh mwingine ambaye alikuwa akituma mashetani yake kwenda kuwakumba watu fulani. Familia za watu hao zikawa zinakwenda kwa sheikh huyo kumuomba awaague ndugu zao. Ndipo sheikh huyo alipowaambia mashetani wamwachie mtu huyo. Kisha familia ikamlipa sheikh huyo pesa nyingi kwa kazi hiyo. Wakati mwingine majini walikuwa wanamletea sheikh huyo pesa na chakula walichowaibia watu.  Baadhi ya watu walikuwa na tini zao. Sheikh akawaomba mashetani wampatie tini, nao wakamletea tini hizo. Pale wenye tini zao walipotazama mabakuli yao, wakakuta tini hazipo.

Ukinyoa upara usiokote madoriani

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.435 seconds