×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

Liwati kwa Sura ya Ushoga na Unyumba: Suni wanasemaje? Mashia wanasemaje?

More
3 years 6 months ago #1979 by Al-Jabri
Hakuna “Sunna” ya Liwati
Vigodoro ni kama Mikusanyiko ya Mdumange enzi za Sodoma, Gomora!
Adhabu ya wasagaji katika Uislamu

Na Wanazuoni wetu

Hii ni mada ya ndani sana lakini kutokana na sababu za kimazingira, inabidi iwekwe hadharani ili kila mmoja ajue Mtazamo sahihi wa Uislamu juu ya kadhia ya maendeano ya unyumba kwa njia tofauti na ile ya kawaida.

Kumekuwa na taarifa za kushitusha kutoka kwa baadhi ya watu kuwa jambo hilo hutendeka kwa kutumia hoja kuwa dini imeruhusu! Cha kukera zaidi ni pale neno “Sunna” linapotumika vibaya kuitaja na kuihalalisha kadhia husika!

Haijuzu wala haipendezi kuingia ndani ya majumba ya watu. Wanandoa ni nguo kwa kila mmoja wao, nasi hatuwezi kuwavua nguo zao. Mwenyezi Mungu kaweka stara ya ndoa, nasi hatuna haki ya kudadisi siri za ndoa za watu.

Lakini pale jambo hilo linapoonekana kuhalalishwa kwa sura ya dini, si vema kulikalia kimya bila maelezo. Faragha za watu zitabaki kuwa faragha zao na dini pia ibakie na usahihi wa mafundisho yake bila kutumiwa visivyo.


Kitabu cha Mwongozo wa Maisha cha Waislamu ni Qur’an. Hiki ni Kitabu cha ufunuo alichoteremshiwa Mtume Muhammad, swallallahu alayhi wa sallam.

Kwa kuzingatia aya kadhaa za Kitabu hiki Kitukufu, tendo la kuingiliana kimwili baina ya watu wa jinsia moja, Liwati, au Ushoga, limeharamishwa moja kwa moja wakati tendo la kuingiliana kimwili kinyume na maumbile baina ya watu wa jinsia tofauti, mume na mke, makatazo yake yanajitokeza zaidi katika Hadith za Mtume, swallallahu alayhi wa sallam.

Aidha maelekezo ya kuwaadhibu wanaume wanaofanya uchafu wa wao kwa wao, na wanawake wanaofanya uchafu wa wao kwa wao yanaonekana moja kwa moja katika Qur’an.

Lakini maelekezo ya kuwaadhibu mume na mke wanaoingiliana kwa utupu wa nyuma hayaonekani katika Qur’an bali yanadhihiri katika Hadiyth. Hapa ndipo panapowasukuma watu kutafuta hukumu sahihi. Je, jambo hili lina uharamu wa moja kwa moja ikizingatiwa kuwa Mwenyezi Mungu hana sifa ya kughafilika, au ni makuruhu kama vile kuvuta sigara?

Na katika hili tumefanya uadilifu wa kushirikisha wanazuoni wa pande zote mbili; Sunni wanaokataza jambo hili na Shia wanaosemekana kuruhusu jambo hili japo nao pia Maulamaa wao wanakhitilafiana.

Liwati kwa Watu wa Jinsia Moja

Kwa upande wa watu wa jinsia moja, Qur’an imetaja maangamizi yaliyowafika watu wa Lut katika Miji ya Sodoma na Gomora kwa sababu ya tendo hilo. Neno Liwat la Kiarabu maana yake ni “Dhambi ya Watu wa Lut.”

Lut alitumwa kuwa Nabii katika Miji hiyo ya Sodoma na Gomora. Kisa chake ndani ya Qur’an ndicho kinachotumika kubainisha makatazo ya tendo la liwati. Aliamrishwa kuwalingania watu wake kumwamini Mwenyezi Mungu na kuacha mambo machafu na matendo ya uharamia na ujambazi.

“Na (wakumbushe Nabii) Lut alipowaambia watu wake: “Bila shaka mnafanya uovu ambao hakuna yoyote aliyekutangulieni kwa uovu huo katika walimwengu. Je, mnawaendea wanaume, na mnawakatizia njia njiani watu (kwa kuwaua na kuwanyang’anya) na mnafanya maovu katika mikusanyiko yenu? Basi halikuwa jawabu la watu wake ila kusema, ‘Tuletee adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli!” (29:28-29)

Majibu hayo ya kiburi, jeuri na kejeli yakamlazimu Nabii Lut kuomba nusura ya Mwenyezi Mungu. “Mola wangu! Ninusuru na watu hawa mafisadi.” (29:30)

Kauli hiyo ya Lut kuomba nusura ya Mwenyezi Mungu ilikuwa na maana ya kunawa mikono kwamba watu wake wameshindikana baada ya kuzama na kubobea au kutopea katika maovu.

Hawakuonesha dalili yoyote ya kurudi nyuma. Shetani aliwasimamia na nafsi zao zikastaabu uovu ambao ndio kwanza wao waliuasisi katika historia ya mwanadamu ulimwenguni.

Kauli eti waletewe adhabu haikuwa kauli ya dhati bali ni kauli ya kejeli kuonesha kuwa aliyokuwa akiyasema Lut ni maneno yake tu na hakutumwa na Mungu wala nini. Waliona kama ni jitihada zake binafsi tu za kuwatisha ili waache maovu ya ushoga na midumange katika mikusanyiko (mfano wa vigodoro vya hivi leo).

Kwa hali hiyo, Hatua za kuwarudi za Mwenyezi Mungu zikaja hivi: “Na wajumbe wetu (Malaika) walipomjia Ibrahimu na habari njema (ya kuwa atazaa mtoto), wakasema pia, “Bila shaka tutawaangamiza watu wa Mji huo, hakika watu wake wamekuwa madhalimu.” Akasema (Ibrahimu), “Hakika humo yumo Luti.” (Malaika) wakasema, “Sisi tunawajua sana waliomo humo, kwa yakini tutamuokoa yeye na watu wake ila mkewe aliye miongoni mwa watakaokaa nyuma.” (29:30-33)


Kuathirika Kisaikolojia na Kutotamani tena Wanawake
Uovu wa liwati ya jinsia moja (ushoga) uliwafikisha watu wa Lut mahala pa kutotamani wanawake. Haya ni madhara ya kisaikolojia ambayo yanatokana na usugu wa moyo katika dhambi.
Qur’an inasema kwa kumnukuu Lut, “Je, mnawaingilia wanaume na mnaacha alichokuumbieni Mola wenu katika wake zenu? Kweli nyinyi ni watu mnaoruka mipaka.” (26:165)
Hali ilikuwa mbaya sana, uovu wa liwati uliwanogea, hawakutaka kusikia neno lolote la Lut. Hawakutaka kuambiwa! Wakawa wakali pale walipoambiwa waache ushoga na kurudi katika utaratibu asilia wa kustarehe na wanawake kwa utaratibu wa ndoa. “Kama usipoacha (kutukataza haya) ewe Luti, bila shaka utakuwa miongoni mwa watu watakaofukuzwa katika nchi hii.” (26:167)
Kama vile walisema, ‘bwana ee, kama wewe hutaki haya tunayoyafanya, si uondoke katika nchi hii, na ukizidi kutufuata-fuata, tutakufukuzilia mbali! Lut akawaambia, “kwa yakini mimi ni katika wale wanaochukia sana kitendo chenu hiki (kichafu). (26:168)

Jaribio la Kuwabaka Wageni (Malaika)
Kuonesha kiwango cha ushenzi walichofikia katika maovu yao, waovu hao hawakuonesha heshima hata kwa wageni. Malaika waliokuja kwa kazi ya kuangamiza kama walivyotangulia kumwambia Ibrahim walijitokeza kwa maumbile ya kuwatamanisha ya kibindamu. Waovu wakafurahi kuona vijana watanashati. Wakaanza kuwamendea.

“Basi wageni walipofika kwa watu wa Luti (kwa sura za kibinadamu), (Luti) akasema, “Hakika nyinyi ni wageni (na mimi sikujueni). (15:61-62)
Hapa Lut alikuwa kama mtu anayestaajabu kufikiwa na wageni wale. Kana kwamba aseme, vijana wangu, mji mbaya huu, sijui mnatokea wapi? Kile alichokichelea ndicho kilichotokea kwamba watu wake wasingechunga heshima kwa wageni hao.
“Na wakaja (kwa Lut) watu wa mji hali ya kuwa wamefurahi kuona wamekuja wageni wanaopendeza ili wawafanyie machafu).” (15:67)
Baada ya kuona wahuni wanakusanyika nyumbani kwake, Luti akajaribu kuwahami wagewni wake. “Akasema Nabii Luti, “Hakika hawa ni wageni wangu, msinifedheheshe. Na muogopeni Mwenyezi Mungu, wala msinidhalilishe (mbele yao).” (15:68-69)
Wahuni hawakutaka kusikia. Kumbe walishamuwekea Nabii zuio la kutoleta wageni! Wakasema, “Je! Sisis hatukukataza (kukaribisha) watu (wa nje)?” (15:70)

Wahuni walifikia hatua ya kupangia maisha watu kwamba wasikaribishe wageni! Hii ilikuwa ni kauli ya kutafuta shari. Lut akatoa kauli nyingine ya kujaribu kuwahami wageni wake, “Akasema, “Hawa ni binti zangu ikiwa nyinyi ni wafanyao yaliyoamrishwa.” (15:71)
Hapo kama vile aliwaambia, jamani mbona wanawake wapo, kwa nini msiwatamani na kuwaoa hawa ili kuendana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu.
Hatima ya Mashoga na Mabaradhuli
Kuhusu hatima ya watu hawa wabaya, Mwenyezi Mungu anatufahamisha hivi: “Naapa kwa umri wako! Hakika wao walikuwa katika ulevi wao (wa maovu); wanahangaika ovyo. Mara adhabu ikwakamata lilipotoka jua (tu). Basi Tukaifanya (miji ile chini juu) juu yake kuwa chini yake: Na Tukawamiminia mvua ya mawe ya udongo wa Motoni.” (15:72-74)

Mazingatio
Kilichowafika watu wa Luti kwa sababu ya uovu wao hakikuishia kwao tu. Mwenyezi Mungu anatutanabahisha: “Hakika katika (masimulizi) haya yamo mazingatio kwa watu wenye kupima mambo. Na miji hii (Tuliyoiangamiza) iko katika njia zipitwazo. Bila shaka katika haya yamo mazingatio kwa wanaoamini.” (15:75-77)


Liwati kwa Watu wa Jinsia tofauti

Si jambo la kuficha kuwa watu wa jinsi tofauti nao wamekuwa na maemdeano tofauti na ya kimaumbile. Jambo hili limezidi kushamiri hivi leo huku baadhi ya watu wakitafuta hukumu sahihi ya Uislamu juu ya mume na mke wanaoendana isivyo kawaida.

Hakuna makatazo na makemeo ya moja kwa moja katika Qur’an juu ya jambo hili bali makatazo yake yanaonekana katika Hadiyth za Mtume, swallallahu alayhi wa sallam.

Kwa kuwa Uislamu hauridhii mahusiano ya kishoga baina ya watu wa jinsia moja, pia unakataa mwendeano tofauti wa kimwili baina ya wanandoa. Sio njia mbadala ya maingiliano ya unyumba pale mke anapokuwa katika siku zake. Watu wanapooana, wanakuwa na haki na wajibu wa kutimiziana mahitaji yao ya kimwili lakini hiyo ni kwa kufuata mwongozo wa Qur’an na Sunna (Hadith).

Qur’an inasema: “Na wanakuuliza juu ya hedhi; waambie huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi (zao). Wala msiwakaribie mpaka watwaharike. Wakishatwaharika basi waendeeni katika pale alipowaamrisheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezin Mungu huwapenda wanaotubu. Huwapenda wanaojitakasa.” (2:22)

Ngono ya liwati inakatazwa hata kama mume na mke wanaridhiana kwani maridhiano hayawezi kuvunja hukumu ya jambo ambalo limeharamishwa. Mwanazuoni wa Sunni wa zama hizi, Yusuf Qaradhawi, yeye anasema kuwa ngono ya liwati inakatazwa ambapo mke ajitenge kama mume anayetaka jambo hilo atamlazimisha.

Na anaweza hata kudai talaka iwapo mume ataendelea kumlazimisha jambo hilo kwani tendo hilo limekatazwa. Hata hivyo, jambo hilo halitengui ndoa ila mpaka mwanamke adai talaka.


Kuna tafsiri ya upotoshaji na inayotoka nje ya muktadha wa aya hii ya Qur’an kuhusiana na kadhia ya kumuendea mke katika njia nyingine. “Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Na zitangulizieni (wema) nafsi zenu; na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba mtakutana naye, na wapashe habari njema walioamini.” (2:223)
Aya hii inaashiria mikao mbalimbali ambayo wanandoa wanaweza kuendeana kwayo wakati wa kukutana kiunyumba ambapo inaruhusiwa kwao kukaa vyovyote maadam tu jimai ifanyikie ukeni na si kwenye njia nyingine.

Mafuqaha wengi wametafsiri maneno ‘kuliendea konde’ kama ni kupanda mbegu za uzazi kwa mwanamke kama mkulima anavyopanda mbegu shambani.

Hivyo, kuliendea konde mtu apendavyo hakuna maana ya kutupa mbegu sehemu nyingine nje ya shamba. Njia nyingine ya maumbile haiwezi kuwa konde kwa sababu yenyewe haioteshi au haileti mazao.


Makatazo ya Liwati ya Unyumba katika Hadiyth

Hadiyth ni maneno na Matendo ya Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, yaliyoripotiwa na watu waliokuwa karibu naye katika maisha yake. Hadiyth zinazohusu Liwati ya Unyumba zinabainisha wazi kuwa jambo hilo linakatazwa kabisa. Madh-hab nne za Sunni kwa pamoja zinakataa maendeano ya liwati kwa wanandoa. Baadhi ya Hadiyth hizo zinasema:


· Yeyote kati yenu akienda kwa mtabiri na kuamini kile anachokisema au akifanya tendo la ndoa na mkewe wakati akiwa katika hedhi, au akimwingilia mkewe kwenye utupu wa nyuma, huyo hayumo katika kile alichoteremshiwa Muhammad.” Imesimuliwa na Abu Hurairah katika Sunan Abu Dawud, 3895.

· “Mwenyezi Mungu hakuoneeni haya kukwambieni ukweli: msiingiliane na wake zenu katika utupu wa nyuma.” Imesimuliwa na Ahmad, 5/213

· Siku ya Kufufuliwa, Mwenyezi Mungu hatamtazama mtu aliyemwingilia mkewe katika utupu wa nyuma.” Imesimuliwa na Ibn Abi Shayba, 3/529. Imesimuliwa na kudarajishwa kama Sahihi na Sunan al-Tirmidh, 1165.

· (Fanya mapenzi na mke) kichali au kimgongo lakini epuka utupu wa nyuma na katika kipindi cha hedhi.” Imesimuliwa na Ahmad na Sunan al-Tirmidh.

· “Yule anayeingiliana na mkewe katika utupu wa nyuma hulaaniwa”-Imesimuliwa na Abu Hurairah, Kitabu cha Ndoa, Sunan Abu Dawud 2157.

· Mkimfuma mtu anafanya tendo la Kaumu Luti, basi muueni mfanyaji na yule anayefanyiwa.” Imesimuliwa na Ibn Abbas. Kitabu cha Adhabu za Kisheria, Sunan al-Tirmidh, Kitabu 17, Hadith 40 (Namba 1456). Imedarajishwa kama Hasan.

· “Kwa hakika ninachokichelea zaidi kwa Umma wangu ni tendo la Kaumuluti.” Imesimuliwa na Jabir, Kitabu cha Adhabu za kisheria, Sunan al-Tirmidhi, Namba 1374, imedarajishwa kama Hasan.


Mtazamo wa Kisheria wa Suni juu ya Liwati ya Unyumba

Sheria ya Kiislamu, Shariah, iliendelezwa katika karne za 8 na 9 katika madh-hab mbalimbali kwa kuzingatia tafsiri mbalimbali za Qur’an na Hadith.

Hadith nyingi za Mtume zinatoa adhabu kali kwa wanaume wanaoingiliana wenyewe kwa wenyewe, na hili ndilo linaloonekana katika sehemu kubwa ya shariah.

Kwa vile mahusiano ya jimai chini ya Shariah huruhusiwa kwa njia ya ndoa, mantiki yake ni kwamba ngono nje ya ndoa ni uzinzi na hivyo yana adhabu ileile ya viboko na kifo. Hata hivyo, kwa mashoga, adhabu zinatofautiana kati ya madh-hab na madha-hab au kati ya Maulamaa na Maulamaa.

Abu Isa At-Tirmidh, yeye anasema, “Maulamaa wamekhitilafiana kuhusiana na adhabu kwa watu wanaotenda matendo ya Sodoma (kaumuluti). Rai ya baadhi yao ni kwamba, anayetenda matendo ya kaumuluti apewe adhabu ya kifo. Hii ndiyo rai ya Malik, Shafi, Ahmad na Ishaq. Wanazuoni miongoni mwa mafuqaha wa Tabiina kama Hasan Al-Basri, Ibrahim An-Nakh’ai, Ata’ ibn Abu Rabah na wengineo wao wamesema kuwa adhabu ya kisheria kwa mtu anayetenda tendo la kaumuluti ni sawa tu na yule anayefanya uzinzi, na hii ndiyo rai ya Sufyan Ath-Tawri na watu wa Kufa.”

Kwa mujibu wa Hadith husika inayoelekeza adhabu ya jambo hilo, adhabu ya kisheria ya tendo la kaumuluti ipo katika tabaka la adhabu za uzinzi.

“Mkimfuma mtu anafanya tendo la kaumuluti, basi muueni mfanyaji na anayefanyiwa.” Imesimuliwa na Ibn Abbas, Kitabu cha Sheria za Adhabu, Sunan al-Tirmidh, Kitabu 17, Hadith 40 (Namba 1456), Hasan.

Aya moja katika Qur’an inachukua msimamo mahususi wa kisheria kwa uzinzi uliothibitika na kwa tendo la liwati lilothibitika kwa mnasaba wa adhabu zilizoptajwa katika Hadith kwani adhabu hutolewa kwa tendo la kuingiliana isivyo halali:

“Na wale wanawake wafanyao machafu (ya wenyewe kwa wenyewe) miongoni mwa wanawake wenu; basi washuhudisheni mashahidi wanne (waliowaona wanafanya hivyo) miongoni mwenu. Na kama wakishuhudia basi wazuieni majumbani mpaka mauti yawafike au Mwenyezio Mungu awafanyie njia nyingine (kama kupata waume kuwaoa, na kama haya).” (4:15)

“Na wanaume wawili wanaofanya uchafu (wa wanaume kwa wanaume) miongoni mwenu, waadhibuni wote wawili. Na wakitubia na wakatengenea waacheni. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye apokeaye toba (na) ndiye mwenye kurehemu.” (4:16)

Licha ya makatazo ya pamoja (Ijma) ya matendo ya kaumuluti katika Uislamu, ada za kiutamaduni katika nchi mbalimbali za Waislamu zinatofautiana katika adhabu ya kifo ambapo ni nchi chache za Kiislamu zinazotekeleza adhabu hiyo.
Mtazamo wa Kisheria wa Mashia juu ya Liwati ya Unyumba
Maulamaa wengi wa Kishia hawaruhusu liwati ya unyumba. Hawa ni wale wanaosema kuwa jambo hilo ni makuruhu kabisa. Kuna dalili nzito kuwa Ayatullah Ruhollah Khomeini aliuchukia upenyezaji wa dhakari katika utupu wa nyuma kama ilivyoainishwa katika Kitabu chake cha juzuu mbili, Tahrir al-Wasilah.
Kwa mujibu wa Ayatullah Sistani, ngono ya utupu wa nyuma inaruhusiwa kwa sharti kuwa “ruhusa hiyo itokane na ridhaa ya mwanamke.” Lakini tendo lenyewe ni makuruhu kabisa.
Mwisho hatuna budi kutahadharisha kuwa japo Hadth inasema kuwa mabasha na mashoga wauawe lakini kwa kuwa hatuishi chini ya sheria za Kiislamu, na maadam bado hatujakinaisha Da’awah kwa Umma, hatua hii iepukwe katika mazingira yetu kwani inaweza kuzaa kesi ya mauaji kwa mujibu wa sheria za nchi.
Bado tujitahidi katika kazi ya kulingania na kuwakataza watu mabaya na kuwaamrisha mema, na hukumu tumwachie Mwenyezi Mungu. Hata Lut katika mazingira yake hakuwa na sheria ya kuwaadhibu mashoga bali aliwalingania na kumwachia Mwenyezi Mungu. (Mhariri)

Ukinyoa upara usiokote madoriani

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.406 seconds