×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

Makaazi ya Majini, Mahali na Muda wanaoweza kupatikana

More
3 years 5 months ago #2012 by NUUR
Na Prof. Dkt. Umar Suleiman all-Ashqar

Majini wanaishi papa hapa duniani wanapoishi binadamu. Wengi miongoni mwao huweza kukutikana kwenye magofu na maeneo makongwe (miji mikongwe), na pia hukutikana mahali palipo na najisi nyingi kama vile chooni. Pia wanakutikana kwenye vichaka vya bangi, mazizi ya ngamia na Makaburini.

Ndiyo sababu Mwanazuoni IbnTaimiya amesema kuwa wale waliokaribu na Ibilisi mara nyingi hukaa kwenye maeneo hayo. Kuna Hadith zisemazo kuwa mtu asiswalie chooni kwa sababu ya najisi iliyomo humo na kwa sababu hayo ni makazi ya shetani na asiswalie makaburini kwani jambo hili hupelekea kwenye ushirikina na pia makaburini ndiyo makazi ya Mashetani.

Aidha Mashetani wengi wa kijini wapo kwenye maeneo yanayoweza kuwa vyanzo vya maasi kama vile sokoni. Mtume (saw) alimpa Swahaba mmoja nasaha hizi:

“Ukiweza, basi usiwe mtu wa kwanza kuingia sokoni. Na usiwe mtu wa mwisho kuondoka sokoni. Kwani hayo ni makazi ya Ibilisi na humo ndimo anamosimamisha bendera yake.” Hadith hii imenakiliwa katika Sahih Muslim.

Mashetani pia huishi ndani ya majumba wanayoishi watu. Mtu anaweza kuwazuia wasiingie ndani ya nyumba au anaweza kuwafukuza ndani kwa kulitaja Jina la MwenyeziMungu (Bismillah), kumdhukuru au kumtaja Allah, kusoma Qur’an hasa hasa “Ayatu Qursiyu ya Surati Baqara (ambayo ni aya ya 255 ya sura hiyo).

Mtume (saw) amesema kuwa mashetani huzagaa na kurandaranda kwa wingi pale giza linapoanza kuingia. Kwa sababu hii, amewanasihi Waislamu kuwarudisha ndani watoto wao katika muda huo. Haya yamesemwa katika Hadith iliyonakiliwa na Bukhari na Muslim.

Mashetani huikimbia Adhana na hushindwa kustahamili kuisikiliza. Katika Mwezi wa Ramadhani Mashetani hufungwa minyororo (pingu).

Mahali wanapopenda kukaa au kukusanyika Mashetani

Mashetani hupendelea kukaa baina ya kivulini na juani (baina ya kivuli na mwanga wa jua). Kwa sababu hiyo, Mtume (saw) amewakataza Waislamu kukaa sehemu hizo. Hadith hii sahihi imenakiliwa katika vitabu vya Sunan na vitabu vingine.


Wanyama wa Majini

Katika Hadith ya Ibn Masud iliyonakiliwa katika Sahih Muslim, Majini walimuuliza Mtume (saw) kuhusu chakula chao. Akawaambia, “kila mfupa uliosomewa Jina la Allah ni chakula chenu.

Muda uleule mfupa utakapofika mikononi mwenu utavikwa nyama. Na kinyesi ( cha ngamia) ni chakula cha wanyama wenu.” Hivyo, Mtume (saw) katujuza kuwa majini wanao wanyama wao ambao chakula chao ni kinyesi cha wanyama wa binadamu.

Wanyama maalum ambao mashetani huandamana nao

Mashetani huandamana na wanyama kadha wa kadha kama vile ngamia. Mtume (saw) kasema:

“Kwa hakika ngamia kaumbwa kutokana na mashetani. Na nyuma ya kila ngamia yupo shetani.”1 Kwa sababu hiyo, Mtume (saw) katukataza kusalia kwenye mazizi ya ngamia. Imenakiliwa Hadith katika Vitabu vya Musnad Ahmad na Sunan Abu Dawud kuwa Mtume (saw) amesema:

“Msiswalie katika mazizi ya ngamia, kwani wanatokana na mashetani. Ila swalieni kwenye machungio ya kondoo kwani wana bar-ka.”2 Ibn Majah,
katika Kitabu chake, Sunan, kanakili Hadith yenye isinadi sahihi kuwa Mtume amesema:

“Msiswalie mahali wanapopumzikia ngamia (yaani pale waendapo baada ya kunyweshwa maji), kwani wao wameumbwa kutokana na mashetani.” Hadith hii inakanusha madai ya wale wanaosema kuwa sababu ya kukatazwa kusalia kwenye mazizi ya ngamia ni kuwa mkojo na kinyesi chao ni najisi. Ukweli ni kuwa mkojo na kinyesi cha mnyama yeyote yule anambaye ni halali kuliwa hakihesabiwi kuwa ni najisi.

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.434 seconds