×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

Ardhi nazo ziko 7 kama Mbingu?

More
3 years 5 months ago #2036 by Oyo
· Umbali kutoka Ardhi moja hadi nyingine ni safari ya miaka 500


· Umbali kutoka Mbingu ya Juu kabisa hadi Arshi ni miaka 500

· Siku ya Kiama Mwenyezi Mungu ataiweka ardhi Mkononi


Na Sidi Abdullah, Mfasiri S. Hussein


Aya ya Qur’an, Surat al-Talaq, inasema, “Mwenyezi Mungu ni Yule ambaye ameziumba mbingu saba, na ardhi kuwa mfano wa hizo. Amri Zake zinashuka baina yao ili mjue kwamba Mwenyezi Mungu amekizunguuka kila kitu kukijua (vilivyo kwa ilimu Yake). (65:12)
Katika tafsiri yake ya Qur’an, Imam al-Suyut, anasema kuwa Aya hii inabainisha kuwa kuna Ardhi Saba (seven earths or lands) kama vilevile zilivyo Mbingu Saba. (Taz. Tafsir al-Jalalayn, al-Suyut).
Hili ni jambo la kuvutia sana. Zikoje hasa hizi Ardhi saba? Kwa vile Vitabu vingi vya tafsiri vimelizungumzia kwa kina fulani jambo hili, mimi nitachukua maelezo ya karibu zaidi katika tafsiri ya Imam al-Alusi:
1) Imam al-Alusi anasema kuwa tafsiri ya wanazuoni wengi wakubwa ni kwamba kuna Ardhi saba (seven Earths). Kila Ardhi ina viumbe vyake ambavyo Mwenyezi Mungu kaviumba mahususi kwa ajili ya Ardhi husika. Uhalisia wa viumbe hao Anaujua Mwenyezi Mungu pekee.
2) Kwa kuzingatia maelezo yanayopatikana katika makusanyo ya Hadith ya al-Hakim, yawezekana kuwa viumbe wa ardhi hizo (ukiacha hii yetu) walipelekewa Manabii wao kutoka kwa Mwenyezi Mungu, lakini jambo hili halijathibitika wala kuhakikiwa usahihi wake.
3) Aidha Imam Alusi anaelezea maana ya, matabaka saba (seven layers) kuwa ni matabaka ya ardhi yetu sisi pamoja sehemu ya angahewa (atmosphere) yake. Haya ni matabaka ya Metali na Madini (metals and minerals), kisha udongo (Soil), kisha Gamba la Ardhi (The crust of the Erath), kisha tabaka la mawingu au moshi (layer of clouds), kisha tabaka la baridi kali mno (extremely cold air), na mwisho tabaka ambalo hewa yake ni nyepesi mno (extremely thin air).
(4) Kaorodhesha rai kuwa “Ardhi Saba” ni mabara makuu saba yanayotenganishwa na bahari, na kayataja mabara ya Amerika na Asia kama mfano.
5) Kaeleza kuwa baadhi ya wanazuoni pia walihisi kuwa “Ardhi saba” zina maana ya aina saba za miji yenye hali ya hewa ya kipekee (unique climate-regions).
(6) Pia kaorodhesha rai mbalimbali kuhusiana na iwapo ardhi saba ziko chini ya mbingu moja, au kila ardhi ina mbingu yake kati ya mbingu saba, na iwapo zote zinachangia maumbile ya angani au la, na kadhalika. (Taz. Ruh al-Ma’ani, al-Alusi)
Kama tulivyoona, kuna tofauti nyingi za rai juu ya tafsiri ya aya tuliyoinukuu hapo juu. Kama Waislamu, tunasema, tunaamini kila kitu ambacho kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, Subhaahahu wata’ala, kwa maana ileile Aliyoikusudia Yeye , na tunaiacha elimu ya mambo yote haya kwa Mwenyezi Mungu, Mjuzi wa Yote.
Mawaidha Mazuri
Imam wa Andalusia ya zama za kati, Imam al-Qurtubi, akisherehesha Aya hiyo katika tafsiri yake, yeye anakuja na maelezo yanayohusiana na mjadala wetu.
Huku akizingatia idadi na sura ya ardhi mbalimbali, Imam Qurtubi kadadisi iwapo inawawajibikia Waislamu kuwapelekea ujumbe wa Uislamu watu wa ardhi nyingine. Yeye anasema:
“…Kwa kuwa haiwezekani kwa watu wa ardhi hii (yetu) kuifikia ardhi nyingine, basi ujumbe wa Uislamu utabaki kuwafikia watu wa Ardhi hii tu…”
Hata hivyo, iwapo kundi, japo moja, la watu miongoni mwa watu wa ardhi hii wangeweza kuifikia ardhi nyingine, basi yumkini kabisa kuwa ufikishaji wa ujumbe wa Uislamu ungelikuwa ni wajibu kwetu kwa kuwa ingeliwezekana kuwafikia viumbe wa ardhi hizo nyingine.
Hiyo ni kwa sababu mtenganiko wa mabahari, maadam yawezekana kuzivuka, basi haukwazi wajibu ulioamrishwa kwetu sote (nao ni kulingania katika Uislamu). (Taz. Jami’ Ahkam al-Quran, al-Qurtubi)
Maelezo hayo yenye maono yalisemwa na al-Qurtubi ambaye aliishi katika nchi ya Hispania mnamo karne ya 13 (AD), kilikuwa ni kitambo kirefu mno kabla ya watu wengi wa Ulaya na Asia hawajajua kuwa kulikuwa na Ardhi nje ya Bahari ya Atlantiki, ikiwa na tamaduni zake: nayo ni Amerika.
Haya ni mawaidha kwetu Waislamu kwamba tushughulike kila siku kuzifikia pembe za mbali za ulimwengu tukiwa na ujumbe wa busara wa Dini ya Mwenyezi Mungu, na tutafakari kwa uoni na maono kulifikia lengo hilo.
Turudi katika Nukta
Badala ya kuzama katika maelezo ya tafsiri, tunayopaswa kuizingatia ni aya yenyewe ya Qur’an: kwamba Mwenyezi Mungu, subhaanahu wata’ala ameuumba ulimwengu maridadi ambao unatuacha katika mshangao kila tunapochunguza ukamilifu wake.
Kisha akatushushia Qur’an ili walimwengu tutambue kuwa Mwenyezi Mungu ni Muweza wa yote, kwamba Ujuzi wake umekizunguuka kila kitu. Ni ujumbe wa kuzitumia ishara za ajabu za maumbile ili kuuona ulimwengu nje ya huu wa kimwili, na kumrejea Muumba wetu.
Mtazamo wa Sayansi na Qur’an juu ya Mbingu Saba
Kuwepo kwa Ardhi Saba na mahali zilipo

Yaweza kuwashangaza baadhi ya wasomaji kuona Qur’an ikisema kuwa Mwenyezi Mungu kaumba Ardhi saba.

“Mwenyezi Mungu ni Yule ambaye ameziumba mbingu saba, na ardhi kuwa mfano wa hizo.” (65: 12).

Ni nini tunachopaswa kujua kuhusiana na ardhi hizi saba? Je, ni Ardhi kwa maana ya mkusanyiko wa nchi, yaani mabara saba yaliyopo katika sayari yetu ya dunia? Je, ni sayari nyingine sawa na Dunia yetu?

Mchoro huu unaonesha mgawanyiko wa sehemu ya ndani ya Ardhi katika matabaka 7 (Batty 1990)

Kabla hatujatathmini usahihi wa Aya ya Qur’an, yaani kuona usahihi wake wa kisayansi, hatuna budi kufafanua ufahamu halisi wa ardhi hizi saba hasahasa jinsi Mtume Muhammad, swallallahu alayhi wa sallam, alivyozielewa. Maelezo kuhusu ardhi saba tunayakuta katika data za awali za Uislamu; Hadith na tafsiri za Qur’an.

Ushahidi wa Hadith
Sahih Al-Bukhari
Imesimuliwa na Muhammad bin Ibrahim bin Al-Harith:
Kutoka kwa Abu Salama bin Abdur-Rahman ambaye alikuwa na mgogoro wa kipande cha ardhi na watu fulani, na hivyo, akaenda kwa Aisha (Mke wa Mtume) na kumwambia jambo hilo. Aisha akasema, ‘Ewe Abu Salama, epuka ardhi, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema, “mtu yoyote anayetwaa hata kipande cha ardhi kwa dhuluma, shingo yake itabiringita (itabimbilika) na ardhi hiyo hadi chini ya ardhi saba.’” (Taz. Juz. 4 Kitabu cha 54, Namba 417; Tazama pia Namba 418, 420; Juz. 3, Kitabu cha 43, Namba 632-633).

Imesumuliwa na Abdullah:
Mwalimu wa Kiyahudi (Rabbi) alikuja kwa Mtume na kusema, “Ewe Muhammad! Tunasikia kuwa Mwenyezi Mungu ataziweka mbingu zote kwenye kidole kimoja, na ardhi zote kwenye kidole kimoja, na miti yote kwenye kidole kimoja,, na maji yote na udongo wote kwenye kidole kimoja, na viumbe vingine vyote kwenye kidole kimoja. Kisha atasema, ‘Mimi ndiye Mfalme.’” Hapo Mtume akatabasamu kiasi cha magego yake kuonekana, na huo ndio ukawa uthibitisho (wa alichokisema) Rabbi. Halafu Mtume wa Mwenyezi Mungu akasoma Aya hii: ‘Na hawakumuheshimu Mwenyezi Mungu hishima ipasayo. Na Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi Mwake, na mbingu zitakunjwa katika Mkono Wake wa kuume (kulia). Na Ameepukana na upungufu na Yu juu kabisa kuliko yale wanayomshirikishiya.” (39:67). (Taz. 6, Kitabu cha 60, Namba 335).

Sahih Muslim
Muhammad bin Ibrahim amesema kuwa Abu Salama alimtaarifu kuwa kulikuwa na mgogoro wa kipande cha ardhi kati yake na watu wake, na akaenda kwa Aisha na kumueleza jambo hilo, Aisha akasema: Abu Salama epuka kuchukua ardhi hiyo, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema, yeyote anayetwaa hata kipande cha ardhi atavishwa shingoni mwake ardhi saba.” (Kitabu 10, Namba 3925); tazama pia Namba 3920-3924)
Al-Tirmidh
Kasimulia Abu Hurayrah:
Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema na amani zimshukie) na Maswahaba zake walipokuwa wamekaa, mawingu yakawagubika, ambapo Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, akauliza: ‘Je, mnajua haya ni nini?’ Walipojibu kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio wanaojua zaidi, akasema: “haya ni mawingu (anan), haya ndiyo yanayobeba maji ya Ardhi (water-carriers of the Earth) ambayo Mwenyezi Mungu huyasafirisha hadi kwa watu wasiomshukuru au kumuomba.” Kisha akauliza: Je, mnajua kilicho juu yenu?’ Walipojibu kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio wanaojua zaidi, akasema, “kuna mbingu, ni dari ambalo linalindwa na mawimbi yanarejeshwa nyuma.” Kisha akauliza,: “ni nini kilichopo baina yenu na mbingu?” Walipojibu kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio wanaojua zaidi, akasema: “Baina yenu na mbingu ni miaka mia tano. Kisha akauliza, “Je, mnajua kilicho juu yake?”Walipojibu kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio wanaojua zaidi, akasema, “mbingu mbili zina umbali wa miaka mia tano baina yao.” Aliendelea kusema hivyo hadi kahesabu mbingu saba. Umbali baina ya kila mbingu mbili ni sawa na umbali baina ya mbingu na ardhi. Kisha akauliza: “Mnajua kilicho juu yake?”Walipojibu kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio wanaojua zaidi, akasema: “juu yake ni Arshi ambapo umbali baina ya Arshi na Mbingu ya saba ni sawa na umbali baina ya mbingu moja na nyingine. Kisha akauliza, “mnajua kilicho chini yenu?” Walipojibu Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanaojua zaidi, akasema: “kuna ardhi.” Kisha akauliza: “mnajua kilicho chini yake (ardhi)? Walipojibu Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanaojua zaidi, akasema: “Chini yake kuna ardhi nyingine ambapo safari kutoka ardhi hii hadi hiyo nyingine ni ya miaka mia tano,” na akaendelea hadi akahesabu ardhi saba, ambapo safari ya kutoka ardhi moja hadi nyingine ni ya miaka mia tano.” Kisha akasema, “Naapa kwa Yule ambaye Mkononi Mwake ipo roho ya Muhammad, laiti mngeliteremsha kamba hadi ardhi ya chini (mwisho) kabisa, basi isingelipita bila Mwenyezi Mungu kujua.” Kisha akasoma, Yeye ndiye wa Mwanzo na wa Mwisho, Ndiye Ndani, Ndiye Nje, Ni Muweza wa Mambo yote.” (Tirmidh kaeleza kuwa kisomo cha Aya hii cha Mtume wa Mwenyezi Mungu kinaashiria kuwa kamba hiyo ingefika chini kwa Ujuzi wa Mwenyezi Mungu, Uweza na Mamlaka Yake kwani Ujuzi , Uweza na Mamlaka ya Mwenyezi Mungu yako kila mahali wakati Mwenyewe akiwa kwenye Arshi, kama alivyoeleza katika Kitabu Chake.) (Ahmad na Tirmidh (Namba 1513).
Hadith hiyo ndiyo hasa inayohusiana na mada yetu kwani inazungumzia moja kwa moja Ardhi saba. Ni Mtume Muhammad mwenyewe aliyechukua dhima ya kuwafundisha wafuasi wake umbile la Ulimwengu.
Ukweli kwamba kuna mbingu saba na ardhi saba tayari umeshaelezwa katika Qur’an. Hata hivyo, Mtume alitaka Maswahaba wake wajue pia kuna uhusiano gani baina ya mbingu saba na ardhi saba, ni mahali gani hasa kila moja ipo, na kuna umbali gani baina yao au kutoka moja hadi nyingine.
Imesimuliwa na Ubayy ibn Ka’b
Kuhusiana na maneno ya Mwenyezi Mungu, Subhaanahu wata’ala, “Kumbuka Mola wako Alipowaleta katika wanadamu kutoka migongini mwao kizazi chao, na Akawashuhudisha juu ya nafsi zao, “Je, Mimi siye Mola wenu?” (7:172), Ubayy akasema: Mwenyezi Mungu aliwakusanya, akawafanya jozi, kisha akawatengeneza na kuwapa uwezo wa kusema, nao wakaanza kusema. Kisha akawekeana nao ahadi. Aliwashuhudisha, je, Mimi siye Mola wenu? Wakasema: Ndiye. Akasema, Naziita kushuhudia mbingu saba na ardhi saba kuhusiana nanyi. (Ahmad, Namba 41)

Imesimuliwa na Abu Said al-Khudhri

Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema na amani zimshukie), amesema kuwa Nabii Musa alimuomba Mola wake amfundishe jambo la kumtaja au kumuomba Yeye, na akaambiwa aseme, ‘Hakuna mungu ila Allah.’ Musa akamjibu Mola wake kuwa waja wote (wa Mwenyezi Mungu) hutamka maneno hayo, lakini yeye alitaka maneno mahususi kwa ajili yake. Mwenyezi Mungu akasema, “Musa, kama mbingu saba na wakaazi wake, ukiniondoa Mimi, pamoja na Ardhi saba zingeliwekwa upande mmoja wa mizani halafu kauli hii ‘hakuna mungu ila Allah’ ingeliwekwa upande mwingine wa mizani, basi kauli hii, ‘hakuna mungu ila Allah, ingezidi uzito.”(Sharh as-Sunna (Namba 731)
Imesimuliwa na Ya’ala ibn Murrah
Ya’ala kasimulia alivyomsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema na amani ziwe juu yake) akisema: Ikiwa mtu yoyote atachukua kipande cha ardhi kwa dhuluma, Mwenyezi Mungu, Subhaanahu wata’ala, atamuamuru aichimbe ardhi hiyo hadi afike mwisho wa Ardhi saba, kisha atafungwa nayo shingoni hadi Siku ya Kufufuliwa pale watu watakapohukumiwa. (Ahmad, Number 885)

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.493 seconds