×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

Je, Mume mwenye wake wanne anaweza kuwaingilia kwa pamoja?

More
3 years 6 months ago #1991 by Asmaa
Na Mwanazuoni wetu)
Si wajibu na wala haipendelewi kwa mume kuwa na maingiliano ya kimwili na wakeze wawili, watatu au wanne kwa wakati mmoja. Hata hivyo, bado ni haki yake ikiwa atafanya uadilifu wa kuhakikisha kuwa kila atakachofanya nao, anakifanya sawasawa kwa kila mmoja wao ili asiende kinyume na Aya hii ya Qur’an:

“Na mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu, basi bakini na mmoja tu.” (4:3)
Muktadha wa aya hiyo ni ndoa yenyewe kwamba suala la uadilifu na insafu lizingatiwe katika ndoa ya mitala. Ikiwa mtu hawezi kufanya uadilifu kwa wakeze wawili, watatu au wanne basi abakie na mmoja.

Kwa kuzingatia uadilifu na uwezo wa kimaumbile, ratiba ya kuwaendea wake kwa siku tofauti inaweza kuwa bora zaidi katika kufanya insafu. Lakini kama mtu ana hakika kuwa hata akiwaendea wakeze kwa wakati mmoja, anaweza kutimiza uadilifu na insafu, basi ni haki yake kwani yuko ndani ya mipaka halali.

Lakini mara nyingi, Sunna ya Mtume ni bora zaidi kuifuata kwani ina wepesi wa kimaumbile na ina hakikisho la insafu na haki sawa kwa kila mke. Sunna hiyo ni ya kuwa na mzunguuko wa siku tofati lakini zinazowiana.

Kimaumbile, mtu asijitie mtihanini kwa kuwakusanya wakeze pamoja halafu akafika mahala akashindwa kuwatimizia wengine. Huo utakuwa ni ukiukaji mkubwa wa aya iliyonukuliwa hapo huu, na mtu ataingia lawani bila sababu.

Kwa mujibu wa Hadiyth ya Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, Siku ya Kiama mtu huyu atakuja na ubavu mmoja ukilebela kwa sababu ya kushindwa kuwatimizia wakeze sawa kwa sawa.

Yapo mambo ambayo kwa hakika mtu anaweza kuwatimizia wakeze sawasawa kwa wakati mmoja kama kuwabusu, kuwakumbatia kwa namna ya kusalimiana na hata kuongea nao. Lakini inapokuja faragha ya jimai, si jambo rahisi kwa mtu kufanya insafu kwa kuwaingilia wakeze wote kwa wakati mmoja.

Baada ya kuwaoa, ni kweli wake wote wanakuhalalikia, na kweli mtu anayo haki ya kuwaendea kwa pamoja lakini Sunna ya Mtume ni bora zaidi katika kuitafsiri Qur’an kwa vitendo kuliko mawazo na matamanio yetu ambayo wakati mwingine huwa ni uchochoro wa Shetani wa kutuvurugia Uislamu wetu.

Ili kujiweka salama, tubakie na Sunna ya kupanga ratiba ya siku za kuwazunguukia wake zetu- Allah ndiye Mjuzi wa yote.

Please Log in or Create an account to join the conversation.

More
2 years 1 month ago #2397 by Mfaume
Swali: Je, naruhusiwa kuwaingilia wake zangu wawili kwa wakati mmoja kwa sharti kwamba kila mmoja akishiriki kivyake, na si kukaa kumwangalia mwenziwe?
Jawabu: Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu, na rehema na amani zimshukie Mtume Muhammad, Ahli zake, na Maswahaba wake.
Kuwaingilia wake wawili kwa wakati mmoja huku wote wawili wakionana imekatazwa na ni karaha. Ibn Qudama anasema: “hata kama mke anakubali kufanya tendo la unyumba huku mwenziwe akimuona bado jambo hilo linakatazwa. Jambo hili ni la udhalili na linakinzana na maadili mema, hivyo, haliwezi kuruhusiwa hata kama wake wenyewe wataliridhia.

Iwapo mmoja wao hatamuona mwenziwe anavyokuwa katika kitendo bali atasikia sauti tu basi jambo hili ni makuruhu japo halikatazwi. Baadhi ya Maulamaa wanaamini kuwa jambo hilo linakatazwa kwani linaleta aibu kama ilivyosimuliwa kutoka kwa al-Qadi Abu al-Tayyib na kundi la Maulamaa wa Shafii.
Rai yenye nguvu ni kwamba jambo hilo linakatazwa kwa vile tu inakatazwa kwa mwanaume au mwanamke kuangalia maungo ya siri ya mwingine (pasipo nguo). Imeandikwa katika Kasshaf al-Qana:
“kuingiliana na wake au vijakazi (kwa wakati mmoja) huku maungo ya siri yakifunikwa lakini sauti ikisikika na mtu mwingine isipokuwa mtoto mdogo asiyejua chochote ni makuruhu hata kama wote wataliridhia jambo hilo. Na tupu zinapoachwa wazi ndio haramu kabisa.
Kufanya tendo la unyumba na mke mmoja huku wengine wakiwepo hakuna mabishano kwamba ni haramu. Imam Al-Hasan al-Basri anasema: Maswahaba na Matabiin walikuwa wakiona wajs ni makuruhu yaani kumuingilia mke mmoja huku wengine wakisikia sauti. Neno “Makuruhu”, kwa mujibu wa Maulamaa wa zamani, lina maana ya haramu.
Imesimuliwa na Ibn Abi Ahaybah al-Musannaf(4/388)

Ibn Qudama (Mwenyezi Mungu amrehemu) amesema: Iwapo wake wawili wanaridhia kuishi pamoja ndani ya nyumba moja, hiyo inaruhusiwa kwa sababu wote wawili wana haki na nyumba yao, lakini wanayo haki ya kuachiana haki hiyo. Pia wake hao wanaweza kuridhiana mume wao alale katikati yao katika kitanda kimoja. Lakini wakiridhiana kuwa amuingilie mmoja huku mwingine akiangalia, hiyo hairuhusiwi, kwa sababu ni kitendo cha aibu na cha kudhalilisha, hakifai. Hakiruhusiwi hata kama wenyewe wanakiridhia.
(Taz. al-Mughni, 8/137)
alHajaawi, mwandishi wa Zaad al-Mustanqi’ anasema: Ni makuruhu kumuingilia mke huku mtu yeyote akiona (wakiwemo wakewenza).
Sheikh Ibn ‘Uthaymiin alisherehesha maneno hayo kwa kusema: Kwamba hapo yanadhihirika mambo mawili; la kwanza, kuingiliana huku maungo ya wote wawili (mume na mke) yakionekana. Bila shaka, kusema kwamba jambo hili ni makuruhu ni makosa, kwa sababu kufunika maungo ya siri ni faradhi. Kwa hiyo, mwingine kuona maungo ya siri ya mwenziwe ni haramu kabisa.
Pili, kufanya tendo la unyumba huku maungo ya siri yakiwa yamefunikwa, kwa maana hayaonekani, kusema jambo ni makuruhu ni jambo linalohitaji mjadala zaidi.
Mathalani, kama wanyumba wanajifunika blanketi na kuanza tendo la unyumba, bado mitikisiko itaonekana. Hii bila shaka, yaelekea kuwa haramu kwa sababu haifai kwa Muislamu kujidhalilisha kiasi hicho. Jambo hili linaweza kuchokoza matamanio kwa mtu anayeangalia, na hilo linaweza kuleta matokeo mabaya.
Rai sahihi kuhusiana na jambo hili ni kwamba ni haramu kufanya tendo la unyumba na mke huku mtu mwingine yeyote yule akiona (hata mke mwenza) isipokuwa labda mtazamaji awe mtoto asiyejua kile kinachofanyika.
Kwa mtoto kama huyo hakuna neno. Lakini kama mtoto anaelewa kile kinachofanyika, basi kitendo hicho kisifanyike machoni mwake kwa sababu mtoto anaweza kuhadithia kile anachokiona. (Taz.Sharh Kitaab al-Nikaah min Zaad al-Mustanqi’, tape 17).

Allah ndiye Mjuzi wa yote

Kila mmoja wenu ni mchunga na ataulizwa kwa alichokichunga.

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.397 seconds