×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

Je, Kulia katika Swala au Dua ni Dalili ya Ucha Mungu?

More
3 years 5 months ago #2003 by Sindibad
Ø Nini maana ya Unyenyekevu?

Ø Unaposikia aya kuhusu Mwenyezi Mungu, sema “Subhaanallah.”
Ø Unaposikia aya kuhusu Jahanamu, sema, “a’uudhubillaahi mina-n-naar”.

Na Dkt. Mamdouh Mohammed, Mkusanyaji, Mfasiri S. Hussein

Kwa Watazamaji wa PeaceTV, jina Mamdouh Mohammed si geni kwao. Huyu ni Mwanazuoni wa Kiislamu ambaye mara nyingi huwasilisha mada mbalimbali zinazohusu Uislamu kupitia Televisheni hiyo.

Moja ya mada hizo ni ile inayohusu athari za Qur’an kwa wasikilizaji. Daktari huyu wa shahada ya Uzamivu amefafanua jinsi Qur’an inavyoweza kuwaathiri Wasikilizaji kwa namna mbalimbali.

Hii ni pamoja na nyoyo kulainika na ngozi kusisimka. Watu wengi husoma Qur’an lakini wengi hawapati athari zake. Ukweli ni kwamba kuelewa kinachosomwa pamoja na kukizingatia ndiko kunakoleta athari hizo.

Makala hii inajaribu kujibu swali linaloulizwa mara kwa mara, je, Mtu huupataje Unyenyekevu katika Swala? Kwanza hebu niuainishe unyenyekevu.

Unyenyekevu ni Nini

Unyenyekevu katika Swala (Khushui) huwa unaeleweka visivyo kwa baadhi ya watu ambao hudhani ni kule kulia-lia. Bali, unyenyekevu ni uhudhurishaji wa moyo katika muda wote wa ibada hiyo.

Pale moyo wa mtu unapohudhurishwa katika kile mtu anachokisema au kukisikia, basi huyo kweli yupo katika hali ya unyenyekevu. Dhana ya Khushui katika Swala ni ya msingi sana.

1. Ni kipengele muhimu cha kumfanya mtu afanikiwe katika maisha haya na maisha ya Akhera. “Hakika wamefuzu Waumini ambao katika Sala zao huwa ni wanyenyekevu.” (23:1-2)
2. Ni kipengele kinachochangia kukubaliwa kwa Swala.

3. Ni njia ya kupatia fadhila nyingi za Mwenyezi Mungu, subhaanahu wa ta’ala. Kadri mtu anavyokuwa na unyenyekevu zaidi ndivyo anavyopata fadhila zaidi.

4. Bila unyenyekevu, moyo hauwezi kutakasika kirahisi.


Njia za Kupata Unyenyekevu

A. Sala za Kablia

1. Muislamu anapaswa kumjua Mola wake kikamilifu. Kumjua Mwenyezi Mungu ndiko kunakomfanya mtu awe muumini bora. (Kuswali huku mtu akiwa hamjui Mungu, au akiwa na shaka naye hakumwezeshi mtu kujihudhurisha barabara katika Swala. Yanabaki mazoea tu ya kufanya mazoezi ya viungo-nyongeza ya mfasiri). Kuwa na elimu sahihi juu ya Mwenyezi Mungu ndiko kunakozidisha mapenzi yetu juu Yake. Kwa hali hiyo, imani nayo huongezeka.

2. Kuepuka dhambi kubwa na ndogo ni jambo linalosaidia sana kupata unyenyekevu. (Mtu anayeshiriki-shiriki katika dhambi, moyo wake huwa mkavu, hawezi kupata matunda ya Swala hata kama atakuwa anajiliza kilio cha machozi katika swala, tangu hapo, ameshakwenda kinyume na lengo lake-nyongeza ya mfasiri). Moyo unakuwa mgumu kupokea maneno ya Mwenyezi Mungu wakati wa Swala na baada ya swala.

3. Kusoma Qur’an mara kwa mara na siku zote hulainisha nyoyo na kuziandaa kupata unyenyekevu.

4. Punguza kuyakumbatia mambo ya kidunia. (Yatimize kama sehemu yako ya dunia lakini jifanye kama huna habari nayo-Mfasiri) Kuelekeza mazingatio katika maisha ya Akhera ndiko kunakozima vishawishi vya kidunia.

5. Epuka kucheka kupita kiasi na epuka mabishano yasiyo na maana kwani haya ni mambo yanayoutia ugumu moyo na kupoteza mazingatio.

6. Acha kazi, au chochote unachofanya (isipokuwa kwa dharura kubwa) punde tu unaposikia adhana. Unaposikiliza adhana, mfuatilie muadhini kila anapomaliza kusema. (yapo maneno mahususi ya kutamka pale anaposema haiyyalal-swala, haiyalal-falah). Hii ndiyo inayokuandaa (kiimani na kisaikolojia) kutoka kwenye shughuli zako za kidunia kwenda kwenye Swala.

7. Kutia udhu punde tu baada ya kusikia adhana ndiko kunakokutayarisha kwa Swala iliyombioni. Udhu pia hufanya kazi kama bafu la (utakaso maalum wa mwili wenye uhusiano wa ndani na wa moja kwa moja na utakaso wa nafsi) kabla ya kuingia katika Swala.

8. Kwenda Msikitini mapema kwa ajili ya Sala na kudumisha dhikri (kumkumbuka Mwenyezi Mungu) ndiko kunakomfukuzilia mbali Shetani na kusaidia kupata mazingatio.

9. Muda wa kusubiria Swala ya Jamaa husaidia kujenga utulivu wa nafsi kabla ya Swala na utulivu wa nafsi wakati wa Swalah.

B. Wakati wa Swala

1. Ile Iqama tu yenyewe ni kiashiria cha nafsi kujiandaa na utekelezaji wa Swala. Kumbuka kile alichosema Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, kumwambia Bilal: “Hebu tupate raha ya Swalah.”

2. Pale unaposimama kuelekea kibla, kumbuka haya yafuatayo:

a. Huenda ikawa hiyo ndiyo Sala yako ya mwisho katika uhai wako. Hakuna uhakika kwamba utaendelea kuwa hai ili kuipata Swala nyingine.
b. Unasimama katikati ya Mikono ya Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu. Je, unawezaje basi kushughulishwa na jambo jingine?
c. Malaika wa mauti anakunyemelea.

3. Usisahau kuleta isti’azah. Inakinga minong’ono ya Shetani.

4. Yaelekeze na yakazie macho yako mahali unaposujudu. Hii husaidia kukuongezea mazingatio.

5. Wakati unaposoma Surat al-Fatiha, jaribu kukumbuka mwitiko wa Mwenyezi Mungu kila mara unaposoma aya. Unaposema “al-hamdulillahi rab-bil ‘alamin’, Mwenyezi Mungu hujibu, “Mja wangu kanitukuza.” Na kadhalika. Hisia hizi za kuzungumza na Mwenyezi Mungu hukuweka katika hali nzuri ya unyenyekevu.

6. Kuisoma vizuri Qur’an kuna athari chanya moyoni.

7. Isome Qur’an polepole na tafakari maana yake kwa undani.

8. Inapendekezwa kubadilisha-badilisha Sura unazosoma ili kuepuka kuzirudia-rudia kinyume na mvuto wake.

9. Badilisha-badilisha Sunna sahihi kama vile kutamka nyiradi tofauti-tofauti za kuanzia kila Swala.

10. Bila shaka, kufahamu Kiarabu kwasaidia kuleta mazingatio juu ya maana iliyokusudiwa.

11. Fuatana na aya zinazosomwa.

a. Unaposikia aya kuhusu Mwenyezi Mungu, mtukuze kwa kusema “Subhaanallah.”
b. Unaposikia aya kuhusu Moto wa jahanamu, sema, “a’uudhubillaahi mina-n-naar”.
c. Ukisikia amri ya kuleta istighfar, lete istighfar.
d. Ukisikia aya inayotaka tasbihi, lete tasbih.


12.Aina hizi za kuingiza-ingiza matamshi kusaidia kudumisha mazingatio.
13. Pale unaposujudu, kumbuka kuwa jambo hili linakukurubisha kwa Mola wako. Tumia fursa hii kuleta dua kwa ikhilasi. Wekeza dakika hizi kwa kuleta dua za kweli

C. Baada ya Sala

e. Unapotoa salamu (unapoleta tasliim ya kumaliza Swala), lete istighfar kama ile ambayo ungeweza kuleta wakati wa Sala.
f. Unapomhimidi Mwenyezi Mungu, mshukuru Mwenyezi Mungu kutoka ndani ya moyo wako kwamba umefaidi uzuri wa Sala. Hii itakufanya upende Swala inayokuja kwani mara kwa mara akili itajielekeza katika Ibada ya sala.
g. Mtu anayeitimiza Swala yake, hupata hamasa ya kudumu na Swala.

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.419 seconds