×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

Kukufurisha na athari zake katika Uislamu

More
11 months 22 hours ago #2711 by
Na Sheikh Kamali Ahmed Hassan – Al Azhar Sharif
Shukurani zote anastahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi waviubwa vyote.

Rehma naAmani zimfikie Mtume (S.A.W), jamaa zake, sahaba zake na wote wale wanaomfuata kwa wema hadi siku ya mwisho.

Ndugu zangu, kwa hakika umma wa Uislamu hivi sasa unashuhudia mawimbi makubwa yanayoifanya Dini hii kuwa kama kaa la moto kwa waumini walioishika.

Mawimbi hayo yanatoka pande mbili tofauti, kwanza ikiwa nje ya Uislamu, na pili ni ndani ya Uislamu.

Ama mawimbi ya nje ya Uislamu hayana shida kukabiliana nayo kwa njia zilizoelekezwa na Dini hii, lakini tatizo kubwa linalosumbua mno waislamu ni wimbi la ndani, ambalo miongoni mwake ni kundi la ukufurishaji na uharaka wa utoaji wa fatua, ambalo huwatoa watu katika Dini ya Kiislamu kwa mapenzi yao bila ya vidhibiti au vifungo vyovyote.

Hivyo basi umeonywa umma huu juu ya kundi hili linalojisifu kuwa nila “watu wa sharia”, ambao wanafanya haraka ya kutoa fatua na kuwakufurisha wale wanaotofautiana nao katika maoni juu ya baadhi ya masuala ya matawi ya Dini.

Kwa sababu za ubaguzi wao, maadui wa nje ya Uislamu wanatumia fursa hiyo kuwaangamiza waislamu na kuhujumu mali na matukufu yao kila uchao na uchwao.

Na kwa upande wa pili, kundi hili limekwendaumbali wa kuwaangamiza Waislamu wenzao kwa kuhalalisha utwaaji kimabavu wa mali zao, kuwavunjia heshima kwa jamii yao, na hata kumwaga damu zao, kwa sababu ya kutofautiana nao rai au mitazamo ya kisheria juu ya matawi ya Dini na sio mizizi au shina la Dini.

Hili ni jambo linalotakiwa kufanyiwa kazi haraka na waumini wa Dini ya Uislamu yenye msamaha,kwa kutumia kitabu cha Mwenyezi Mungu (S.W) na Sunna za Mtume (S.A.W) kwa usahihi wake, ili kurejesha umoja madhubuti wa umma, mshikamano wa kweli, mapenzi na huruma baina yao.

Uislamu umetoa tahadhari kali juu ya fikra hii ya kukufurishana kwani imepinda na kufumbia macho katazo juu ya kuharakisha kutoa fatua ya kumkufurisha Muislam na kumtoa katika Dini yake.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu; “Na wala msiseme kwa yule aliyetoa salamu kuwa si Muislamu kwa kutaka ngawira kwa maisha ya …”.

Na kutoka kwa Abi Dhari amesema, Mtume (S.A.W); “Hamtukani mtu mwenziwe kwa ukafiri isipokuwa huzunguka huo ukafiri kwa mtukanaji”.

Basi dalili hizi na nyinginezo nyingi miongoni mwa Aya na Hadithi zimefikia ukomo wa tahadhari juu ya kukufurisha Muislamu bila ya dalili, na Uislamu unakataza aina hii ya vitendo bila ya dalili kutoka katika Qur’aan wala Sunna, bali inatakiwa uwe na dhana nzuri kwa Muislamu mwenzako hadi ipatikane dalili ya hukumu juu ya kitendo chake chochote akifanyacho.

Anasema mwanachuoni Shaukani kwamba, hukumu kwa mtu aliye Muislamu kwa kutoka kwake katika Dini ya Kiislamu na kuingia kwake katika ukafiri,haiji isipokuwa kwa dalili iliyowazi kama jua la mchana.

Na amesema Bin Hajari Al-Haithami, inatakikana kwa Mufti wa eneo husika, apige vita ukufurishaji kiasi awezacho, kutokana na ukubwa wa athari zake mbayav katika Uislamu.

Hivi sasa Ulimwengu wa Kiislamu unahitaji kuziendea harakati za kusukuma mbele maendeleo ya Uislamu na Waislamu kwa umoja na mshikamano wa kweli, hivyo kukufurishana kunavunja jambo hilo na kugawanya nguvu za kwa namna moja au nyingine.

Ndugu zangu, kitendo cha kumkufurisha mtu bila ya dalili na kumtoa katika Dini yake kwa kuharakisha fatua, humnyang’anya mtu huyo haki ya ubinadamu na kumuweka katika hatari ya kuuawa, kunyongwa na kusambaratishwa kiuchumi na kijamii.

Hivyo hatuna budi kuiweka mbali jamii yetu na hasa kizazi chetu kichanga na jambo hili la kukufurishana na kuharakisha fatua bila ya dalii. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Atuwezeshe kujiweka mbali na jambo hilo linalokwenda kinyume na mafundisho Yake, Aaamin.

Wabillah Tawfiiq,

Kama una maoni, Maswali au ushauri, usisite kuwasiliana na Mudir, Egyptian Islamic Center kwa Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Ukinyoa upara usiokote madoriani

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.407 seconds