×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

JE ALLAH MTUKUFU ANASHUKA MCHANA SIKU YA ARAFA ?

More
8 months 3 weeks ago #2743 by
JE ALLAH MTUKUFU ANASHUKA MCHANA SIKU YA ARAFA ?

Sheikh wangu, Je hii message ni ya kweli ?

Siku ya Arafa itakuwa siku ya alkhamisi Inshallah ... Allah anashuka katika mbigu ya dunia siku zote usiku wa mwisho tu ila siku ya Arafa pekee Allah anahuka mchana wa siku hiyo kwa utukufu wa siku hiyo .. na Allah anasemehe madhambi ya miaka miwili mwaka uliopita na mwaka ujao kwa kufunga siku hiyo isikupite kufunga siku hiyo upate kusamehewa madhambi yako na watumie ndugu zako wengine wajue na upate ajra.

⯑ JAWABU:
Allah mtukufu atukinge na itikadi za kifirauni na kiyahudi. Itikadi ya Mola mwenye sehemu maalumu ni itikadi ya firauni aliyeangamizwa, Mayahudi waliolaaniwa na Allah mtukufu na Wakristo waliopotea kama alivyotuambia Allah mtukufu katika Qur an.

وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَا هَامَانُ ابْنِ لِي صَرْحًا لَعَلِّي أَبْلُغُ الْأَسْبَابَ

أَسْبَابَ السَّمَاوَاتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰ إِلَٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ كَاذِبًا ۚ وَكَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِفِرْعَوْنَ سُوءُ عَمَلِهِ وَصُدَّ عَنِ السَّبِيلِ ۚ وَمَا كَيْدُ فِرْعَوْنَ إِلَّا فِي تَبَابٍ

Na Firauni akasema: Ewe Hamana! Nijengee mnara ili nipate kuzifikia njia,Njia za mbinguni ili nikamwone Mungu wa Musa. Na kwa hakika mimi bila ya shaka namjua kuwa ni mwongo tu. Na hivi ndivyo Firauni alivyo pambiwa ubaya wa vitendo vyake, na akazuiliwa Njia. Na vitimbi vya Firauni havikuwa ila katika kuangamia tu.

((Sura Ghafir, Ayah 36, 37))

Na ni wao Mayahudi katika Zaburi yao waliyoibadilisha wanasema Mola alishuka kwa Yaaqoub akapigana naye usiku kucha, hata ilipokaribia asubuhi Yaqub akamlazimisha Mola ambariki ili amuachie apande tena mbinguni ndio akabarikiwa akapewa jina la Israel.

Na wakristo wanasema bila shaka mola wao amekaa kitako mbinguni, na huu ni katika upotevu wa kiitikadi, Sheitan anawapoteza watu.

Amma waislam, Itikadi yetu ni kama asemavyo Allah mtukufu:

أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ مَا يَكُونُ مِنْ نَجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِنْ ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا ۖ ثُمَّ يُنَبِّئُهُمْ بِمَا عَمِلُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ إِنَّ اللَّهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ


Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi? Hauwi mnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wane wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yu pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku ya Kiyama atawaambia waliyo yatenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

((Sura Al-Mujadila, Ayah 7))

Wala Usighururike ndugu yangu muislam na riwaya za kutunga, na porojo la wapotezaji ambao wanawafanyia kazi mayahudi ili kupoteza itikadi sahihi ya Waislam.

Allah mtukufu ametakasika na kuwa na sehem, kushuka na kupanda, n.k. kwani ni sifa za viumbe :

فَاطِرُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ جَعَلَ لَكُمْ مِنْ أَنْفُسِكُمْ أَزْوَاجًا وَمِنَ الْأَنْعَامِ أَزْوَاجًا ۖ يَذْرَؤُكُمْ فِيهِ ۚ لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

(Ali Muhsin Al-Barwani)
Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi, amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu, na katika nyama hoa dume na jike, anakuzidishieni namna hii. Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.
((Sura Ash-Shura, Ayah 11))

Allah mtukufu atukinge na itikadi mbovu za kiyahudi na kikristo zinazopenyezwa kwa waislam.
Wallahu aalam.

Ameyaandika, mja dhaifu
⯑ Khamis Alghammawi
⯑ FAIDIKA NA MAWAIDHA
⯑ +96879056144

Ukinyoa upara usiokote madoriani

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.384 seconds