×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

Jee inafaa muislamu kufunga safari ya kwenda Mirikh (Mars)?.

More
4 years 4 months ago - 4 years 3 months ago #1666 by Al-Jabri
Jee inafaa muislamu kufunga safari ya kwenda Mirikh (Mars)?.
Mamlaka kuu ya mambo ya kiislamu yanayohusiana na wakfu na vipaji  ya Umoja wa falme za kiarabu imetoa fatwa ya onyo kwa muislamu kufanya safari ya kwenda sayari ya Mars pasipo matarajio ya kurudi tena duniani.
[img]components/com_ccboard/assets/uploads/421_225b486fb17c79d65841cb74b9b526f2.jpg
Tayari nchi hiyo ina kitengo cha uwekezaji kinachotoa fursa kwa watu wan chi hiyo  kushiriki safari za  kitalii za kwenda anga za juu (Aabar Investments ) .Kituo hicho kinaongozwa na mwanaanga Richard Branson's  na mamlaka hayo yameridhia safari hizo
Katika tamko lake hilo chini ya mufti wan chi hiyo,mamlaka hiyo  "GAIAE" imetoa tamko lisemalo  "Hairuhusiwi kwa mtu kwenda Miirikh akijua hatorudi tena na kwa kuwa kwenye sayari hiyo hakujapatikana uthibitisho wa kuwepo kwa nyenzo za uhai.Uwezekano wa mtu huyo kufa ni mkubwa kuliko kuishi.Safari ya namna hiyo ni sawa na kujiuwa,na kwa kuwa haimfalii muislamu kujiuwa hivyo hivyo hairuhusiwa kisharia kushiriki safari ya namna hiyo.
Mtalii wa mwanzo wa anga za juu muislamu ni mwanamfalme Sultan bin Suleiman Alsaud ambaye mwaka 1985 aliungana na wanaanga wa kimarekani katika chombo cha Discovery.Mnamo mwaka 2006 mwanaanga wa kike wa Iran .bi , Anousheh Ansari alikuwa ni mwanaanga wa mwanzo wa  nchi hiyo kuruka ambapo alifanya majaribio ya jinsi ibada za kiislamu zinavyotekelezeka nje ya dunia.
Matokeo ya majaribio hayo yalipelekea kutolewa mwongozo maalum wa matendo ya kiibada kwa mfano kwenye gati la ISS ambako siku moja ya kawaida huko hudumu kwa muda wa dakika 90 tu.
Taasisi ya kidachi inayoshughulika na matayarisho ya safari hiyo ya Mars ijulikanayo kama Mars One imesema mpaka tarehe ya mwisho kupokea maombi ilipofika,jumla ya watu 200,000 walikuwa wameomba kushiriki safari hiyo.Watu 1,058 ndio waliochujwa na kubaki kwenye orodha ya wanaofaa kwenda ambapo baadae watu wane ndio watakaohitajika.Maombi yalitoka nchi 107 na haijulikani kati ya hao wangapi ni waislamu.

Ukinyoa upara usiokote madoriani
Attachments:
Last edit: 4 years 3 months ago by Al-Jabri.

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.555 seconds