×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

Viumbe ambao Mwenyezi Mungu kawaumba na milango mikali ya fahamu

More
4 years 3 months ago #1722 by Al-Jabri
         ·        Vyura walitoweka Italia Siku tatu kabla ya Tetemeko la ardhi! ·        Nyoka ‘walitoweka’ China mwezi mmoja kabla ya Tetemeko!     Na Harun Yahya, Mfasiri Abu Kawthar   KWA NINI BAADHI YA WANYAMA  huonekana kuwa na ung’amuzi usiokuwa wa kawaida pale linapotokea tetemeko la ardhi? Je, baadhi ya viumbe huwa na tabia gani vinapokabiliana na hatari? Kwa nini baadhi ya milango ya utambuzi ya baadhi ya wanyama ni mikali kuliko ile ya binadamu?                          Viumbe na Ishara ya Hatari   Moja ya faida kubwa za kuishi kijamii ni kwamba maisha ya kijamii yanaweka ulinzi zaidi dhidi ya hatari kwani pale mmoja wa wanyama wanaoishi kijamii anapohisi hatari, basi huwapa tahadhari wenziwe badala ya kujinusuru peke yake kimyakimya. Kila jamii ya viumbe hai ina aina mahususi ya tahadhari.   Sungura na baadhi dondolo (paa) hunyanyua mikia yao kama ishara ya kuwatahadharisha wanyama waliopamoja nao au walio karibu yao pale wanapohisi hatari.   Ndege wengi wadogo hupeana ishara ya tahadhari kwa mlio mahususi pale wanapomng’amua adui yao. Jamii za viumbe kama ndege wa aina ya Golden oriole wa Amerika au Ulaya wao hutoa sauti kali yenye muda mfupi-mfupi wa kunyamaza pale wanapotoa tahadhari.   Sikio la binadamu husikia sauti hiyo kama kifilimbi tu. Sifa muhimu zaidi ya sauti hii ni kwamba kule inakotokea hakuwezi kung’amulika. Hii ni salama kwa ndege anayewatahadharisha wenzake, kwani, kwa hakika ndege huyo hujitia hatarini kwa sababu kitendo cha kulia kinakaribisha hatari kwake mwenyewe. Lakini kwa vile kule inakotokea sauti hakufahamiki, hatari, kwa kiasi fulani, hupungua.   Kwa wadudu ambao wanaishi katika makundi ya kijamii, mdudu anayeanza kung’amua hatari huwatahadharisha wenziwe wa jamii yake. Hata hivyo, harufu ya hatari inayotoka kwa mdudu anayewatonya wenziwe nayo huchokoza hisia za adui. Hivyo, mdudu anayewatahadharisha wadudu wenziwe wa jamii yake dhidi ya hatari iliyopo naye hujiweka hatarini kuuawa.   Kuchakulo au Vidiri (Prairie dogs) wa Amerika huishi katika makundi makubwa ya jamii zao. Viota vyao, ambavyo hufanana na mji, hugawanyika katika takribani sehemu nne ambazo wanyama huishi.   Wanyama wote katika maeneo haya hujuana. Wapo vidiri ambao hudumisha ulinzi muda wote wakisimamia miguu yao ya nyuma kwa namna ya kuona pande zote za kuingilia na kutokea.   Iwapo mnyama mmojawapo anamuona adui, hutoa mlio wa kubweka unaofanana na sauti ya filimbi. Tahadhari hii hurudiwa-rudiwa na walinzi, na huipelekea jamii husika ya wadudu kuwa katika hali ya tahadhari.   Wanasayansi wanaoushuhudia ushirikiano huu wa kimaumbile hushangazwa na tabia za kustaajabisha za viumbe hawa wasio na akili ya kujitambua. Bila shaka, Mwenyezi Mungu ndiye anayewaongoza viumbe hawa kwa kuwapa ilihamu wakati wote. Yeye ndiye anayemmiliki kila mmoja wao na kumuamrisha awe na mwenendo gani. Ukweli huu unabainishwa katika Qur’an:   “Na vinamsujudia Mwenyezi Mungu vyote vinavyokwenda mbinguni na katika ardhi; katika wanyama na Malaika pia, nao hawatakabari. Wanamuogopa Mola wao aliye juu yao, na wanatenda wanayoamrishwa.” (16:49:50)   Wanyama Wenye Milango ya Fahamu tofauti na Binadamu   Mwenyezi Mungu kajaalia milango ya fahamu ya wanyama kuwa mikali zaidi kuliko ile ya binadamu. Baadhi ya wanyama wanayo hata milango mingine ya fahamu ambayo binadamu hawana.    Mathalani, kwa kuwa tembo ni wanyama wanaoishi katika maeneo mapana ya wazi, ni jambo muhimu kuwa wao wana “mawasiliano” makali.   Mawasiliano haya sio tu ni matokeo ya hisia kali za harufu walizonazo tembo bali, mbali ya hivyo, Mwenyezi Mungu amewaumba na kiungo katika sehemu ya mbele ya kichwa (paji)  ambacho kinapiga kelele za ndani kwa ndani ambazo binadamu hawawezi kuzisikia.   Kutokana na kiungo hiki, tembo huweza kuwasiliana kwa siri na kwa lugha ya kiusalama (encrypted language) ambayo viumbe wengine hawawezi kuielewa.   Kelele hizi za ndani kwa ndani zinazopigwa na tembo huweza kufika masafa na masafa. Hivyo, sauti hii maalum inayolizwa na tembo ni muhimu kwa mawasiliano ya masafa marefu.   Macho ya baadhi ya viumbe yana ubora mkubwa zaidi kuliko macho ya binadamu. Kwa mfano, wadudu kama nyuki huweza kuona mionzi isiyoonekana kwa macho ya binadamu.    Tabaka moja katika macho ya wanyama wanaowinda usiku na katika macho ya ndege wanaoruka usiku huwawezesha viumbe hawa kuona gizani. Vipanga wa Barani Afrika huweza kung’amua kama mnyama aliyelala ardhini kafa au mzima wakiwa umbali wa zaidi ya mita 4,000 angani, huu ni umbali ambao binadamu hawezi kuona hata kwa darubini.   Utambuzi wa harufu wa baadhi ya wanyama ni mkali mara laki moja na hata milioni moja zaidi kuliko ule wa binadamu. Mathalani, mbwa huweza kutambua harufu ya mbali mno.   Kutokana na sifa hizi, mbwa hutumika katika uchunguzi wa awali wa magonjwa ya kuharibika kwa mfumo wa umengenyaji ndani ya mwili wa binadamu hali ambayo hudhihirishwa na harufu mbalimbali zitokazo mwilini.   Vilevile, mbwa hutumika katika shughuli za kipolisi kama vile kunusa dawa za kulevya na kuwakagua wahalifu na hutumika katika kunusa miili ya wahanga waliofudikizwa na majanga kama matetemeko ya ardhi.   Baadhi ya jamii ya nyoka wana kiungo maalum cha utambuzi ambacho hutambua mabadiliko ya halijoto (temperature changes). Kiungo hiki kilichomo ndani ya kishimo kidogo baina ya tundu za pua hutumika kubaini iwapo vitu ni vya moto au baridi.   Kutokana na kiungo hiki, nyoka huweza kung’amua hata halijoto ya wastani wa chini ya nyuzi 10C inayotoka kwa mnyama wa damumoto kama vile panya. Pia nyoka huwa na hisia kali sana dhidi ya hewa inayotoka kwa mtu  na chombo kama ndege   Viumbe wote hutoa umeme na joto. Ni vigumu kwa kiumbe anayeishi ardhini kung’amua hali hizi, kwa sababu hewa hutumika kama kihami (insulator) cha kukinga na kuhifadhi umeme huo.   Lakini hali huwa tofauti chini ya maji. Umeme hutiririka kwa njia ya maji  ambayo ndiyo kihami umeme asilia (natural insulator). Kwa hiyo, kiumbe ambaye huweza kuutambua umeme huu ana tunu kubwa.   . Hivyo, papa wana tunu hii, wanaweza kutambua mikumbo yote ya  hali ya hewa kwenye maji, wanaweza kutambua mabadiliko ya halijoto, kiwango cha chumvi ya maji, na hasahasa mabadiliko madogo katika maeneo yenye umeme kutokana na viumbe wanaopita hapo.   Kuna matundu mengi katika miili ya papa yaliyojaa dutu za mafuta-mafuta. Hata kama matundu haya, kwa kiasi kikubwa, yamo ndani ya kichwa cha papa, yemesambaa katika mwili wote wa samaki huyu. Viungo hivi maalum vinayoitwa “Lorenzini Bulbs” ni ving’amuzi madhubuti vya umeme (perfect electricity Sensors).   Viungo hivi vinafungwa kwenye vitundu kwenye kichwa na uso wa mnyama huyu, na huwa kali kama vipokezi vya umeme. Kiasi kwamba papa huweza kutambua mtawanyiko wa umeme kwa kiwango cha volti bilioni mia moja na ishirini.   Hii ni nguvu ya ajabu, kwani ina maana kuwa pale mabetrii mawili ya volti 1.5 yanapowekwa umbali kwa kilometa 1, 600 kutoka betri moja hadi jingine, papa huweza kung’amua mkondo wa mawimbi unaotokana na mabetrii haya.   Mwenyezi Mungu, Mjuzi na Muweza wa Yote ndiye mwenye kuumba milango hii ya hali ya juu ya utambuzi au viungo maalum walivyonavyo viumbe hai. Katika aya moja ya Qur’an, sanaa ya maumbile ya Mola wetu inabainishwa hivi:   “Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kasha Akakufanyeni wanaume na wanawake. Na mwanamke yeyote hachukui mamba wala hazai ila kwa ilimu Yake. Na mwenye kupewa umri hapewi umri wala hapunguziwi umri wake ila yamo katika Kitabu (cha Mwenyezi Mungu). Bila shaka haya ni sahali kwa Mwenyezi Mungu.” (35:11)              Viumbe wanaong’amua Tetemeko la Ardhi   Utafiti wa Kisayansi  umeonesha kuwa matabaka ya juu ya ardhi huwa katika msongo mkubwa kabla ya tetemeko la ardhi na kwamba majabali hutoa chembechembe zenye chaji ya umeme wakati wa msongo huo.    Chembechembe hizi huripuka pale zinapokutana na hewa au maji na husababisha molikuli mpya ziundwe. Mathalani, hewa ya haidrojeni peroxide huundwa pale chembechembe hizo zinapochanganyika na maji.   Tukio hili ambalo hubadili kemia ya maji katika vidimbwi-vidimbwi, hung’amuliwa na viumbe hai, na kusababisha waanze kuonesha tabia zisizokuwa za kawaida na kuling’amua tetemeko la ardhi kabla halijatokea.   Mnamo mwaka 2000, jamii yote ya vyura walioishi katika ziwa lililokuwa jirani na eneo lililotokea tetemeko la ardhi ambalo liliathiri jiji la L’Aquila la Italia, waliondoka katika eneo hilo siku tatu kabla ya tetemeko kutokea.   Mnamo mwaka 1975, takribani mwezi mmoja kabla ya tetemeko la ardhi kutokea katika mji wa Haicheng, nchini China, nyoka waliondoka kwa pamoja na kutelekeza viota vyao.   Nukta isiyokuwa ya kawaida ni kwamba nyoka hawa waliondoka licha ya baridi kali ambalo lingesababisha vifo vyao kwa kuyaacha makazi yao ya msimu wa kipupwe.   Katika maeneo fulani iligundulika kuwa samaki wanaokaa chini kabisa ya maji walikuja juu kabla ya tetemeko la ardhi.   Kama ilivyodhihiri katika mifano hiyo, kila kimoja kati ya viumbe hivyo kiko chini ya ulinzi wa Mwenyezi Mungu.Yeye ndiye anayekiongoza kila kimoja jinsi ya kutenda navyo hufuata mwongozo kikamilifu. Kila kimoja kimejisalimisha kwa Mwenyezi Mungu aliyeviumba. Katika Qur’an, ukweli huu unabainishwa:   “Vyote vilivyo mbinguni na ardhini ni Vyake, na vyote humtii Yeye.” (30:26)   Rehema Isiyo na Ukomo ya Mwenyezi Mungu ndiyo inayowafunika Viumbe wote   Ukweli kwamba viumbe hai hudumisha maisha yao kutokana na milango maalum ya fahamu, silika yao na mbinu za kuchukua tahadhari ambazo Mwenyezi Mungu kawajaalia, na kwamba zinalinda vizazi vyao dhidi ya hatari kwa uangalifu mkubwa na kwa kushirikiana, ni ushahidi wa kazi ya kuumba ambayo inahitaji kutafakariwa.   Hakuna shaka kuwa viumbe hai hawajitengenezei sifa hizi wao wenyewe. Kila kitu katika maumbile ni kazi ya Mwenyezi Mungu ambaye ana ilimu isiyo na ukomo na Uweza usio na kikomo, na kila kimoja kinakwenda kwa mwongozo Wake. Yeye ndiye Mwenye Uweza, huruma, rehema, maarifa, ilimu na Hikima. Ukweli huu unabainishwa katika aya moja ya Qur’an:   “Mimi nimtegemea Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola wenu. Hakuna kiumbe yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu anamsarifu atakavyo. Bila shaka Mola wangu yuko juu ya njia iliyonyooka.” (11:56)   Kila kitu katika maumbile ni kazi ya Mwenyezi Mungu ambaye ana ilimu na uweza usiokadirika. Mwenyezi Mungu ni Yule ambaye kaumba viumbe vyote, binadamu, wanyama, wadudu, mimea, viumbe vyote vyenye na visivyo na uhai, Naye ndiye Mwenye uweza mkubwa, Mwenye Ilimu na Hikima.   “Basi sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Muumba wa ardhi, Muumba wa walimengu wote. Na ukubwa ni wake mbinguni na ardhini, naye ni Mwenye nguvu, Mwenye Hikima.” (45:36-37).   Kuna mpangilio usio na kasoro katika ulimwengu mzima. Hakuna shaka kuwa hii ni kazi ya kuumba ya Mwenyezi Mungu ambaye ndiye anayemiliki vilivyo na visivyo na uhai kuanzia viumbe viduchu hadi Masayari makubwa ya Mfumo wa Jua. Kila kimoja kati ya viumbe hivi humtii Mwenyezi Mungu na kutekeleza maamrisho Yake. Aya hii inabainisha:   “ Sema (uwaulize): “Ni vya nani vilivyomo mbinguni na ardhini?” Useme (tena kujibu): “Ni vya Mwenyezi Mungu.” Yeye amejilazimisha kuwafanyia (rehema waja Wake). Hakika atakukusanyeni Siku ya Kiama, siku isiyo na shaka. Wale waliojitia khasarani  hawaiamini (Siku hiyo). (6:12).

Ukinyoa upara usiokote madoriani

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.387 seconds