×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

Ukitaka Dua ijibiwe, anza kutia Udhu, Swali rakaa mbili

More
1 year 4 months ago #2621 by
· Unaweza kuahirishiwa msiba badala ya kitu unachoomba

Na Khansa Padri
Wakati fulani nilihitaji kitu fulani, kwa kweli, nilikihitaji kwelikweli. Nikawa naomba dua ya kukipata kila nilipopata fursa ya kuomba. Nilikuwa nikinyoosha mikono juu Mbinguni, huku machozi mengi yakinibubujika na kuchuruzika mashavuni. Nilimlilia Mola wangu kwa unyenyekevu kumuomba Aipokee dua yangu.
Masiku yakakatika. Hakuna kilichotokea. Miezi ikapita, hakuna kilichotokea. Miaka ikayoyoma, hakuna kilichotokea. Nikafika mahala pa kudhani labda nina upungufu fulani katika dua zangu. Lakini pia nikautafakari ule wakati nilioutumia, na unyenyekevu niliokuwa nao katika kuomba na kuomba, na nikaona sikuwa na upungufu.
Hatimaye, miaka mingi baadae, dua yangu ikajibiwa. Na hapo ndipo nilipoweza kutanabahi sawasawa kwa nini Mola wangu alikawiza kuijibu dua yangu. Kwa rehema za Mola wangu, Muweza wa Yote, niliruzukiwa ufahamu na ilimu ambayo niliihitaji katika kufanya maamuzi sahihi.
Laiti ningelikitimiziwa dua yangu mapema zaidi, katika wakati ambao sikuwa na uwezo wa kufikiri sawasawa, basi ningeliweza kuangukia katika makosa mabaya sana. Hivyo, nilikuwa kama mtoto anayelilia kuchezea kisu, wakati Mwenyezi Mungu aliyetakasika na upungufu, alikuwa kama ‘mzazi madhubuti lakini mwenye mapenzi, ambaye alininyima kisu hicho kutokana na mapenzi na huruma yake kubwa.
Si kwamba Mola wangu alikuwa hasikilizi kilio changu. Si kwamba nilikuwa na upungufu katika dua zangu. Bali yalikuwa ni mapenzi ya Mola wangu kwa mja wake mnyenyekevu ambayo yalinikinga. Ukweli ni kwamba dua yangu ilikuwa inajibiwa kwa namna ambayo mimi mwenyewe sikuelewa hadi baadae sana.

Mwisho kabisa dua yangu ilipotokezea kwa sura niliyokuwa nikiiomba, Mwenyezi Mungu, akanijaalia taufiqi niliyoihitaji ili kufanya maamuzi sahihi. Kwa hiyo, katika kipindi chote hicho, Mola wangu alikuwa akiniandaa kwa ajili hiyo-Allahu Akbar!
Kama ilivyosimuliwa na Imam Ali Ibn Abi Talib ambaye alisema: “Dua ndiyo silaha ya Muumini.” (Baadhi ya watu huutumia usemi huu kama hadith ya Mtume Muhammad, swallallahu alayhi wa sallam, lakini huu ni usemi wa Sayyidna Ali).
Dua ina uwezo wa kubadili qadari yako ingawaje tayari Mwenyezi Mungu alikwishajua kuwa wewe utakuja kuomba dua hiyo, Naye ataikubali. Ilishapangwa katika kadari kuwa endapo mja ataomba dua basi yatatokea haya na yale katika maisha yake, na asipoomba dua, yatatokea mengine. Vyote vimo ndani ya Qadari.
Kipenzi chetu Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema kuwa Dua hukubaliwa kwa njia tatu; Mosi, unaweza kupewa mapema papa hapa duniani kile unachokiomba na kwa kadri ya vile ulivyoomba au vizuri zaidi ya hivyo.
Pili, yawezekana shida au msiba ulikuwa uje kwako, lakini Mwenyezi Mungu, subhaahahu wata’ala, kwa rehema Zake, akazuia usikufike au kukusibu. Tatu, Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Hikima, anakuwekea akiba ya malipo ya Akhera na wakati huo huo kakupangia kitu kizuri zaidi. Hivyo, kila dua yetu hujibiwa ama sisi wenyewe tukijua au bila kujua.

Mtume, Kigezo chetu, pia katufundisha njia ambazo zinaweza kuongeza uwezekano wa dua zetu kujibiwa haraka zaidi tena kwa namna tutakavyo, na tukaweza kuelewa kuwa tumejibiwa.

1. Kwanza, anza kwa kutia udhu na kuswali rakaa mbili

2. Kisha anguka kusujudu huku viganja vikinyanyuliwa juu (hasa kwa kuvibana pamoja). Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema, “Aliyekaribu zaidi na Mwenyezi Mungu kati yenu ni yule ambaye wakati anaposujudu, huomba dua nyingi ndani yake.” Na pia Mtume amesema, “Wakati wa sijida, jitahidini kuomba dua. Yaelekea kabisa, mtajibiwa.” (Muslim)

3. Anza kwa kumswalia Mtume, swallallahu alayhi wa sallam

4. Msifu Mwenyezi Mungu kama anavyostahiki kusifiwa, japo hatuwezi kukamilisha sifa Zake.

5. Omba msamaha kwa dhambi na upungufu wako

6. Kisha Muombe Mola Mwingi wa Ukarimu na Mpaji akukidhie chochote cha kheri unachokiomba katika dunia hii na Akhera.

7. Maliza dua yako kwa kumswalia Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, na ahli zake.

Aidha kuna nyakati maalum za mchana na usiku ambazo dua zako zinaweza kukubalika zaidi. Kwa uchache, nyakati hizo ni pamoja na:

1. Saa mojawapo ya Siku ya Ijumaa japokuwa hatukuambiwa ni saa ngapi hasa hiyo ambapo tunahimizwa kuitumia siku hiyo ya Ijumaa kwa dua.
2. Muda baada ya adhana ya Swala kuadhiniwa
3. Baada ya kutia udhu, na kushuhudia kuwa Mungu ni Mmoja, na Muhammad ni Mtume Wake.
4. Na katika theluthi ya mwisho ya kila usiku. Kuhusiana na muda huu wa usiku, Mwenyezi Mungu, subhaanahu wata’ala, anasema, “Nani anayeniita ili nimwitikie? Nani anayeniomba ili nimpe? Nani anayeomba msamaha Wangu ili nimsamehe?” (Sahih Bukhari, Hadith Qudsi).

Katika kipindi nilichokuwa nikiomba dua, kwa kweli, nafsi yangu haikutulia, na nilikaribia kushawishika kuacha dua na kukata tamaa. Lakini sikutetereka. Kwani nilijua kuwa hivyo ndivyo alivyokuwa akitaka Shetani: Alitaka nipoteze imani kwa Mola wangu. Nilipoona moyo unaanza kusononeka na kuonesha dalili za kupoteza matumaini, nikakazana mara dufu kuomba dua.
Ndugu zangu Waislamu, jueni kuwa tunapokata tamaa na kuacha kuomba dua basi Shetani hupata nafasi ya kuua imani zetu. Licha ya uzito wa machungu, huzuni, majonzi wakati wa kusubiri dua kujibiwa, katu tusikate tamaa. Badala yake ndio tuongeze imani kwamba Mola wetu Yu karibu nasi na huwaitikia waja Wake.
Kwa kuzingatia hilo, mara zote, tunapofikwa na mitihani, na tunapozongwa na matatizo, au kupata masaibu, tuseme Alhamdulillahi wa ‘ala kulli hal, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila hali.’ Tudumu na imani thabiti kwa Mwenyezi Mungu, na dua zetu zitajibiwa InshaAllah

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.545 seconds