×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

Mazungumzo ndio njia pekee ya kumaliza Vita vya Afghanistan

More
3 months 2 weeks ago #2791 by
Na Nizar Visram - Ottawa
TAREHE 21 Agosti mwaka huu Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza nia ya kuongeza majeshi yake nchini Afghanistan. Ingawa hakutoa idadi kamili lakini imeripotiwa kuwa atatuma wanajeshi 4,000 ili kuungana na 10,000 walioko huko wakitoa “ushauri na mafunzo” kwa askari wa Afghanistan wanaopigana dhidi ya Taliban na Daesh
Trump pia amezitaka nchi za NATO nazo ziongeze nguvu zao za kijeshi huko Afghanistan. Hivi sasa kuna askari wa NATO takriban 6,500 na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka. Marekani imezitaka ziongeze askari 3,000 hadi 5,000
Trump siku zote amekuwa akipinga Marekani kujiingiza katika mgogoro wa Afghanistan. Mnamo Januari 2013 alitoa maoni yake katika mtandao akisema “Tunapaswa kujitoa kutoka Afghanistan kwa haraka. Askari wetu wanauliwa na askari wa Afghanistan tuliowafunza sisi wenyewe. Wakati huohuo tunapoteza mabilioni ya fedha. Ni upuuzi mtupu!”
Wakati wa kampeni mwaka jana alikuwa akimlaumu Rais Obama kuwa anapoteza mabilioni huko Afghanistan badala ya kuzitumia nchini Marekani. Sasa mara tu baada ya kukalia kiti cha urais Trump anaona ni vizuri Marekani “ipigane na magaidi hadi ushindi” ingawa wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda wa miaka 16.

Hata Rais Obama naye aliposhika madaraka mwaka 2009 aliongeza idadi ya askari na kufikia karibu askari 100,000. Walikuwepo askari 30,000 naye akaongeza 70,000. Pia waliajiriwa mamluki, yaani askari wa kukodiwa 100,000.
Obama naye alifanya hivyo kwa nia ya kumaliza vita. Lakini alipoona vita havimaliziki akapunguza askari kuanzia 2011, Sasa Trump anaongeza.
Obama aliamua kujitoa kwa sababu idadi ya askari wa Marekani na wa Afghanistan waliokufa na kujeruhiwa ilizidi kuongezeka. Wakati huo Marekani ilimtaka aliyekuwa rais Hamid Karzai wa Afghanistan asaini mkataba kuwa askari wa Marekani hawatashitakiwa kwa uhalifu wa kivita. Karzai akakataa na ndipo Obama akatangaza kuwa ifikapo 2016 ataondoa askari wake wote.

Mwaka 2014 rais mpya wa Afghanistan, Bw Ashraf Ghani akakubali kusaini mkataba huo na ndipo Obama akaamua kubakiza askari 9,000 wakati anamaliza awamu yake. Sasa Trump ameamua kuongeza askari kwa azma ya “kuwamaliza magaidi”
Wengi wanajiuliza iwapo mkakati huu wa Trump utafanikiwa. Ni kwa sababu baada ya jitihada zote za Bush na Obama leo hii serikali ya Afghanistan inadhibiti asilimia 60 ya nchi na maeneo yaliyobaki yanadhibitiwa na Taliban au yanagombaniwa. Mwaka jana serikali ilikuwa inashikilia asilimia 65
Ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) inasema licha ya Obama kuongeza majeshi, askari wa Marekani takriban 2,400 wameuawa. Askari wa Afghanistan nao pia wanakufa kwa wingi, kwani mnamo miezi minne ya 2017 askari 807 wameuawa.
Na ripoti ya wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan inasema askari wa polisi 1,302 waliuawa kati ya Machi na Agosti mwaka huu, yaani wastani wa askari tisa kufa kila siku
Kile ambacho hakisemwi sana ni kuwa raia wa Afghanistan ndio wanaoumia zaidi, kwani tayari 26,512 wamepoteza maisha yao na 48,931 wamejeruhiwa. Katika miezi sita ya 2017 peke yake raia 1,662 wameuawa.
Tangu rais Bush kushambulia Afghanistan mnamo Oktoba 2001 raia wasiopungua 175,000 wameuawa nchini humo, wakati mamilioni wamelazimika kuyahama makazi yao.

Taliban 800 waliofungwa gerezani Mazar-i-Sharif waliuliwa. Jijini Kakarak raia 48 waliuawa wakiwa wanasheherekea harusi. Mwaka 2015 madaktari na wagonjwa 42 waliuliwa wakati hospitali ya Kunduz ilipopigwa mabomu kutoka angani
Wakati haya yanafanyika chini ya utawala wa Bush na Obama ndivyo Taliban wamekuwa wakichukua maeneo zaidi. Sasa Trump akiwa madarakani atabidi apambane siyo tu na Taliban bali pia na waasi wanaojulikana kama dola ya Kiislamu au Daesh ambao tayari wanadhibiti mashariki ya Afghanistan
Hata waziri wa majeshi wa Marekani Bw James Mattis alitamka mnamo Juni kuwa “Kwa hali ya sasa ilivyo vita vya Afghanistan vimetushinda”. Na wakati Trump anaongeza majeshi huko Afghanistan na gharama pia zitaongezeka. Tayari amepitisha bajeti ya kijeshi ya mwaka huu inayofikia jumla ya dola bilioni 700. Katika Afghanistan peke yake Marekani imetumia dola bilioni 700 katika muda wa miaka 17.

Wakati anazungumzia kuongeza vita nchini Afghanistan, Rais Trump pia aliionya Pakistan, akidai kuwa nchi hiyo ya jirani inawalea magaidi wanaopenya Afghanistan. Akaiambia Pakistan iache kutoa hifadhi na mafunzo kwa Taliban na wengineo la sivyo Marekani italazimika “kuchukua hatua za kijeshi”.

Inafaa ikumbukwe kuwa tangu miaka ya 1979 Marekani imekuwa ikitumia Pakistan kama kituo cha kuwafunza mujahidin waliotumika kwenda kuipindua serikali ya Afghanistan iliyokuwa ikisaidiwa na Umoja wa Sovieti (USSR).

Marekani ikamwaga mabilioni kwa utawala wa dikteta Zia-Ul-Hak nchini Pakistan. Osama Bin Laden (kutoka Saudi Arabia) ndiye aliyekuwa mkuu wa mujahidin hao. Baadae akawa adui wa Marekani na ndipo wakamuua akiwa nchini Pakistan.

Wakati huo Zbigniew Brezinski ndiye alikuwa mshauri wa rais Carter katika mambo ya usalama, naye alikuwa akizuru Pakistan ili kusimamia mafunzo, silaha na fedha zilizotolewa kwa mujahidina. Matokeo yake Taliban kutoka Afghanistan na nchi kwengineko wakaweka makazi yao nchini Pakistan.

Kuhusu onyo la Trump kwa Pakistan, mwanasiasa mashuhuri na kiongozi wa chama cha Tehreek-e-Insaf (PTI) nchini humo, Bw Imran Khan alimjibu kwa kusema “Iwapo Trump ataongeza majeshi yake nchini Afghanistan ni nini cha ziada watakachofanya ambacho kiliwashinda askari 150,000 wa Marekani?” Akaongeza kuwa Rais Bush na nchi wenzake wa NATO walivamia Afghanistan tarehe 7 Oktoba 2001 na wakaupindua utawala wa Taliban. Sasa ilikuwaje mpaka sasa vita vingali vinaendelea?

Khan akaongeza kuwa kama nia ya Trump ni “kuwamaliza maadui” kama alivyotangaza basi si tofauti na kile walichokuwa wakifanya siku zote kina Bush na Obama.

Alipoulizwa nini kifanyike, Khan akashauri kuwa njia pekee na sahihi ya kumaliza vita ni kuondoa majeshi yote ya kigeni na nchi kisha kuanzisha mazungumzo baina ya wananchi wa Afghanistan wenyewe. Nchi za jirani kama Pakistan, China, Iran na Russia ni vizuri zikashirikishwa.

Lengo la mazungumzo ni kuunda serikali ya maridhiano, ikishirikisha pande zote zinazopigana, ameshauri Khan. Pia anaongeza kuwa wakati Trump anataka kuishambulia Pakistan ni vizuri ikumbukwe kuwa nchi hiyo imepoteza raia wake 70,000 katika kusaidiana na Marekani dhidi ya Taliban. Pia uchumi wake umepata hasara ya dola bilioni 100.

Sasa Trump anasema ataacha kutoa misaada kwa Pakistan. Khan amesema nchi yake inaweza kujitegemea bila ya hiyo misaada iliyoleta hasara ya mali na maisha.

Hakuna vita vya Marekani vilivyodumu muda mrefu kama hivi vya Afghanistan. Mara ya kwanza waliingia nchini humo miaka 38 iliyopita, wakati Rais Jimmy Carter alipotangaza nia yake ya kuipindua serikali iliyokuwa ikisaidiwa na Urusi (USSR). Tangu wakati huo vita vingali vinaendelea.

Ili kuelewa nia halisi ya vita hivi ni vizuri tukajua kuwa Afghanistan inakisiwa kuwa na akiba ya madini yenye thamani ya zaidi ya dola Trilioni moja. Haya ni madini ya kila aina kuanzia dhahabu, shaba, chuma, cobalt hadi lithium. Ripoti ya siri iliyotayarishwa na makao makuu ya majeshi nchini Marekani (Pentagon) inasema Afghanistan inaweza ikawa “Saudi Arabia ya madini”.

Hata wachunguzi wa USSR wakati huo pia waligundua kuwa Afghanistan ina akiba ya tani milioni 60 ya shaba, bilioni 2.2 ya chuma, milioni 1.4 ya madini adimu kama lanthanum, cerium na neodymium pamoja na aluminium, dhahabu, silver, zinc, sebaki na lithium.

Katika hali kama hii tunaona serikali ya Afghanistan ikisaini mkataba wa miaka 30 na kampuni ya China iitwayo China Metallurgical Group. Kwa mujibu wa mkataba huu kampuni hiyo itachimba shaba ya dola bilioni tatu. Pia kampuni za India zimepewa leseni ya kuchimba chuma.

Ukiacha hayo madini kuna mradi mkubwa wa China wa kujenga njia za usafirishaji (silk road) kuunganisha makontinenti ya Asia na Ulaya. Afghanistan imo katika mradi huu. Hiki ndicho chanzo cha vita virefu vya Marekani nchini Afghanistan.

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
+1 613 699 2933.

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.530 seconds