×
INSHA YA UCHUMAJI KARAFUU (21 Apr 2016)

Assalaam alaykum.
Tunakaribisha insha zinazoelezea shughuli za uchumaji karafuu.

Kanuni za urafiki katika Uislamu

More
11 months 22 hours ago #2710 by
Na Ahmet Tasgetiren
Tumeelezwa juu ya sifa za “Watu anaowapenda, na wanaompenda” Allah (S.W) katika Quran Tukufu.

Mwenyezi Mumgu Mtukufu anasema; “Enyi mlioamini! Atakayeiacha miongoni mwenu Dini yake, basi Mwenyezi Mungu atakuja kuleta watu anaowapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa Waumini na wenye nguvu juu ya makafiri, wanapigania Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama ya anayelaumu. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpaamtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu na Mwenye kujua.” (Quran 5:54) na haya ni machache tu.

Katika Aya nyingine ya Qur’aanambayo inasema: “Marafikiwa Mola hawana woga ndani yao, wala hawahuzuniki”.

“Walioamini na Kumcha Mungu”wametajwa pia, hivyo kuzikusudia haswa sifa hizo kuu…”. (Quran 10:62).

Imani na UchaMungu ni sifa kuu za uaminifu wa Nabii Ibrahim (A.S), pia uaminifu ni sifa iliyooneshwa kwa umma na Mtume Muhammad (S.A.W).

Tunaposoma aya za Quran, tunapata watu waliopita mipaka ya upendo wa Mola wetu Mtukufu kwa maana kuwa, Kanuni inaletwa na Mwenyezi Mungu (S.W), ambaye kwa hakika anafungua daftari ya kumbukumbu ya upendo na urafiki.
Mola anawapenda wanaoishi maisha ya wema na ubora (Muhsin);anawapenda pia wanaofanya makosa na kujutia, ambao roho zao na miili yao imetakaswa kutokana na taka zote, ambao wanavumilia dhiki na maudhi kwa ustahimilivu, ambao wameweka imani zao zote Kwake, na ambao wana kadiri; aidha anawapenda wenye kutenda haki na uwadilifu.

Inawezekana pia kufikia kanuni ya urafiki na upendo kwa kubainisha aya ambazo Mola amezielezea juu ya wale “asiowapenda”.

Mola wetu Mtukufu hawapendi wanyonyaji, wenye majivuno, waharibifu, wasaliti, wanaovunja uaminifu, wenye kukataa ukweli, wasiona kiasi, wahaini na wengineo mfano wa hao.

“Huwapati (huwaoni) watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, kuwa wanawapenda wale wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake…”(Qur’an 58:22).

Kama binadamu watachukua sifa hizi za Mitume hawa kama mwongozo na kama wataweza kufumbua kanuni kwa kuweka sifa hizi katika nafsi zao wenyewe, je? Hawataweza kufikia katika njia inayoelekea kwenye “Rejesta ya urafiki”?

Hii ni miongozo mingine ya kanuni:
Katika Kuitafuta Qur’aan, inawezekana tunaweza kupata kanuni ya “urafiki” katika aya inayosema; “Jina la Mola likitajwa, mioyo yao hutetemeka”.

Labda katika sura ya Ikhlas au katika dua ya “Swala zangu, kujitoa kwangu, na kifo changu ni kwa ajili ya Mola wangu, Bwana wa ulimwengu”.

Au kujikabidhi kwa kusema; “Sisi ni wa Mola na kwake tutarejea”, au labda mwujiza wa upendo wa Mwenyezi Mungu ni katika kupenda kwa ajili ya Mola.

Na labda Nguvu ya Mwenyezi Mungu huendezwa kusawazishwa kwa utulivu wa kiroho uliotawazwa katika uumbaji wote……nani anajua…?

Akiwaelezea marafiki wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mwanachuoni Zunnun Al-Misri anasema; “Qur’aan imebebwa katika nyama zao na damu zao. Masikitiko yaohupotea katika Qur’aan na huwashawishi. Wameifanya Qur’aan kuwa mwongozo wao katika mwujiza wa kiroho, kitanda chao cha kulalia, mwongozo wao kuwaongoza katika njia, na chanzo cha ushahidi wao. Kutokana na sheria ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, iliyoelezwa katika Qur’aan,wanaongeza hatua zao za wokovu. Wanaangaza ubinafsi wao kwa mwangaza wa Mola Muumba. Wanafikia matakwa yao kupitia Qur’aan. Wao ni mabubu kwenye maneno yenye uovu, na vipofu katika matendo yaliyokatazwa.” Rejea kitabu “Marafiki wa Mwenyezi Mungu, VI: p.63”.

Kwa hakika maisha ya Muumini hayana kujikwaa katika uelekeo wa kumtii Mola wake, mapema kama ilivyopatikana, ndivyo Rejesta ya “Marafiki wa Allah (S.W)” inavyofunguka.

Nihitimishe kwa kusisitiza kuwa, Muumini anatakiwa asiche kukimbia, kusonga mbele katika njia hii ya kuusaka urafiki na Mola wake Muumba kwa matumaini makubwa, hamu, njaa, kiu, shauku kubwana kushusha pumzi akiwa katika njia hii.

Ukinyoa upara usiokote madoriani

Please Log in or Create an account to join the conversation.

Time to create page: 0.425 seconds