Ndoto

FAQs - NDOTO

  Imepokewa kuwa Mtume swallaLlaahu alayhi wa sallam amesema ndoto ni sehemu katika sehemu  arobaini za unabii Mtu anayefaa kutoa tafsiri ya ndoto ni mtu mmoja tu mwenye sifa zifuatazo.

   1.Ni lazima awe na elimu ya kutosha ya tafsiri ya Qur'an.

  2.Awe ni hafidh wa hadithi za Mtume swala Llaahu alayhi wa salaam.

  3.Ajue chimbuko la maneno kiasi cha kuyafahamu asili yake

  4..Awe anafahamu vyema  lugha  ya kiarabu.

  5.Ajue asili ya daraja za watu.

  6.Ajue kanuni za msingi za kutabiri au tafsiri.

  7.Awe mcha Mungu.

  8.Awe ni mtu anayekubalika katika jamii.

  9.Awe mkweli katika maneno na vitendo.

 

Inapotolewa tafsiri ya ndoto wakati mwengine huzingatiwa muda mtu alipoota hiyo ndoto.Wakati mwengine tafsiri hutolewa moja kwa moja kutoka katika  Qur'an na wakati mwengine kutoka katika hadithi..Baadhi ya wakati mfasiri wa ndoto (muabir ) badala ya yule aliyeota hutoa tafsiri kwa kumzingatia mtu anayefanana naye kwa cheo au jina.Wakati mwengine ndoto huaguliwa kwa kutumia jina tu au maana ya maneno au kinyume cha maneno.

Mtua akiota amebeba  mbao au kuni tafsiri yake ni umbeya na udaku.

 

Dalili ni matumizi ya maneno katika lugha ya kiarabu.Msemo hubeba au anabeba mbao hutumika pindi mtu anapochukua umbeya kutoka kwa mtu mmoja kupeleka kwa mwengine.  

 Ukiota unakula nyama punguza kusengenya watu.Wengine ukiona wanakula nyama huenda wanakusengenya angalia kasoro zako.

Dalili  ni kutoka katika Qur'an 49:12

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ وَلا تَجَسَّسُوا وَلا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا

أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ

Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu.

Ukiota umeokota au unacheza na funguo matarajio ni  utapata neema.

Dalili ni kutoka katika Qur'an surat Alqassas 28:76

إِنَّ قَارُونَ كَانَ مِن قَوْمِ مُوسَى فَبَغَى عَلَيْهِمْ وَآتَيْنَاهُ مِنَ الْكُنُوزِ مَا إِنَّ مَفَاتِحَهُ لَتَنُوأُ بِالْعُصْبَةِ أُولِي

 الْقُوَّةِ إِذْ قَالَ لَهُ قَوْمُهُ لا تَفْرَحْ إِنَّ اللَّهَ لا يُحِبُّ الْفَرِحِينَ

Hakika Qaruni alikuwa katika watu wa Musa, lakini aliwafanyia dhulma. Na tulimpa khazina ambazo funguo zake zinawatopeza watu wenye nguvu kuzichukua. Walipo mwambia watu wake: Usijigambe! Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanao jigamba.

Ukiota umepanda chombo cha majini katika kipindi cha shida inayokukabili basi uko karibu kuokoka na janga hilo.

Dalili ni kutoka katika Qur'an Surat Hud 11:40-42

حَتَّى إِذَا جَاءَ أَمْرُنَا وَفَارَ التَّنُّورُ قُلْنَا احْمِلْ فِيهَا مِن كُلٍّ زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلاَّ مَن سَبَقَ عَلَيْهِ الْقَوْلُ

   وَمَنْ آمَنَ وَمَا آمَنَ مَعَهُ إِلاَّ قَلِيلٌ

 40.Hata ilipo kuja amri yetu, na tanuri ikafoka maji, tulisema: Pakia humo wawili wawili, dume na jike, kutoka kila aina, na ahali zako, isipo kuwa wale ambao imekwisha wapitia hukumu; na watu walio amini. Na hawakuamini pamoja naye ila wachache tu.

وَقَالَ ارْكَبُواْ فِيهَا بِسْمِ اللَّهِ مَجْرَاهَا وَمُرْسَاهَا إِنَّ رَبِّي لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ

41. Na akasema: Pandeni humo kwa Bismillahi, Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, kwenda kwake na kusimama kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

وَهِيَ تَجْرِي بِهِمْ فِي مَوْجٍ كَالْجِبَالِ وَنَادَى نُوحٌ ابْنَهُ وَكَانَ فِي مَعْزِلٍ يَا بُنَيَّ ارْكَب مَّعَنَا وَلاَ تَكُن مَّعَ

الْكَافِرِينَ

42.Ikawa inakwenda nao katika mawimbi kama milima. Na Nuhu akamwita mwanawe naye alikuwa mbali: Ewe mwanangu! Panda pamoja nasi, wala usiwe pamoja na makafiri.

Ukiota mfalme au mtawala wa nchi ameingia nyumbani kwako au katika mji fulani kinyume na tabia yake,hii ni ishara ya balaa litakalowakumba watu wa nyumba au mji huo.Inaweza kuwa pia ni ishara ya kudhalilika kwa watu watukufu wa mji huo.

Dalili ni kutoka katika Qur'an suratun Namli  27:34

قَالَتْ إِنَّ الْمُلُوكَ إِذَا دَخَلُوا قَرْيَةً أَفْسَدُوهَا وَجَعَلُوا أَعِزَّةَ أَهْلِهَا أَذِلَّةً وَكَذَلِكَ يَفْعَلُونَ

Akasema: Hakika wafalme wanapo uingia mji wanauharibu, na wanawafanya wale watukufu wake kuwa wanyonge. Na hivyo ndivyo watendavyo.

  Ukiota kunguru itatafsirika kama  mtu fisadi   na asiyekuwa na haya.

 

  Dalili ni kutoka hadithi za Mtume swalla Llaahu alayhi wa sallam, kwani amemtaja kunguru kama faasiq,  neno  lenye  maana ya kukosa haya na kuwa fisadi.

  Ukiota panya itatafsirika kwamba ni mwanamke asiye na haya na muasharati.

 

  Dalili ni hadithi ya Mtume swallaLlaahu alayhi wa sallam ambayo  imetumia neno فاسقة lenye maana ya mwanamke mzinzi  na asiye na haya.

 Ukiota kizingiti cha mlango tafsiri yake ni mwanamke.

 

  Dalili ni hadithi ya Mtume swallaLlaahu alayhi wa sallam inayosimulia kuwa nabii Ibrahim (a.s)  alimueleza mwanawe nabii Ismail (a.s) kuwa "Badilisha kizingiti cha mlango wako" akimaanisha  "mke wako"

 Ukiota ubavu tafsiri yake ni mwanamke.

 

  Ushahidi ni hadithi ya Mtume swallaLlaahu alayhi wassallam inayosema mwanamke ameumbwa kutokana na ubavu uliopinda.

 Ukijiota mwenyewe au mtu mwengine  ni mgonjwa tafsiri yake ni unafiki.

 

  Dalili ni matumizi ya maneno katika lugha ya kiarabu kwani  ikisemwa Fulani ni mgonjwa katika ahad I  zake ina  maana  hatekelezi ahadi zake ambayo ni moja ya sifa za unafiki.

 Kamasi   katika ndoto huashiria  mtoto   wa kiume.

 

  Dalili ni matumizi  ya maneno katika lugha ya kiarabu kwani  msemo  kamasi  za simba hutumika pindi  kijana  wa  kiume anapofanana na baba yake.

Mtu akiota kwamba mkono wake ni mrefu ina maana atawafanyia wema watu na atakuwa mkarimu kwao.

 

  Dalili ni matumizi ya maneno katika lugha ya kiarabu, kwa sababu  msemo wa kiarabumkono wake ni mrefu kuliko wako humaanisha yeye ni mkarimu kuliko wewe.

Ukiota mtu anamrushia mwengine  silaha kama vile jiwe,mshale au akimlengesha silaha nyengine  mwenzake  ina maana  mtu huyo anayerusha anamtuhumu  kimakosa mtu mwengine.

 Katika matumizi ya lugha ya kiarabu msemo Fulani amemtupia silaha mtu hutumika pindi mtu anapomsengenya mwingine au kumtuhumu mtu kimakosa

  Kujiona mwenyewe au mtu mwengine katika ndoto akinawa mikono maana yake ni  kukata tamaa na kupoteza matumaini.Msemo kwako nimenawa mikono hutumika pindi mtu anapopoteza matumaini ya kupata jema au faida kutoka kwa mtu mwengine.

  Ukisikia moja ya majina hayo ndotoni au ukimuona mtu mwenye moja ya majina hayo ina maana ya ubora,ukuu ,ukarimu na heshima.

   Ukisikia moja ya jina hilo au kumuona mtu mwenye moja ya majina hayo katika ndoto humaanisha kupita njia iliyonyooka,kuepushwa na makosa,kuongozwa vyema  na mwenendo mzuri.

Uwa lililochanua kam vile waridi  huashiria maisha mafupi au kifo kiko karibu  kwa kuwa maua huwa hayadumu.Tafsiri kama hiyo htolewa kwa mtu ambaye  humiliki mauwa.

   Ukiota unalia usingizini ina maana ya raha na furaha,lakini kulia huko kusiwe kwa sauti,mayowe au kulia kwa machozi na kujiapiza kama vile uko kwenye msiba.

Ukiota harusi,kucheka au kucheza miziki  maana yake ni huzuni na majonzi  yanafuatia.

Watu wawili wakionekana wanapigana katika ndoto,basi yule atakayeshindwa katika ugomvi  ndiye atakayepata ushindi.

Mtu akiota analazimishwa jambo basi atavutiwa kutekeleza shuruti  fulani katika mkataba.Au ikiwa ataota anabembelezwa  akubaliane na shuruti  fulani ina maana kuwa atalazimishwa.

A'alaykum
Nimeota kuwa nimelala kitandani sasa kila nikilala upande ninaotaka nageuzwa upande ninaoweka miguu jambo hili liliendelea hivyo mpaka nikapata kizunguzungu ghafla mama yangu aliekuwa kavaa khanga moja tu alifungua mlango wa chumbani na hapo nikashtuka kutoka katika ile ndoto nikiwa bado nipo usingizini nlimuomba mama yangu msaada kwani ile ndoto iliniogopesha sana nlilia sana mama yangu lakini aliondoka baada ya muda kidogo nlishtuka  kutoka usingizini. Hii ndoto ilinishangaza sana
Tafadhali naomba unisaidie tafsiri yake