صدقة الجارية

SHIRIKI HUDUMA KWA WAGONJWA BOMBO

      Assalaam alaykum warahmatuLlaah.

 Ndugu yetu  muislamu  tafadhali changia huduma kwa wagonjwa hospitali ya mkoa wa Tanga -Bombo.

  Tumeunda umoja kwa jina la Akhlaqu Al Islamia (Ustawi wa jamii yakiislamu). Huduma tunazotoa kwa sasa ni kuhudumia wagonjwa hospitali ya mkoa ya Bombo.

Huduma hizo ni kushughulika na usafi wa mwilini wa wagonjwa wasiokuwa na ndugu wa karibu,kuwanunulia mahitaji muhimu na hata kusafisha mazingira nje ya majengo na ndani ikiwa ni pamoja na sehemu za vyooni.

   Misaada inayohitajika ni pamoja na fedha taslimu kwa ajili ya kununulia vifaa vya huduma na mahitaji ya wagonjwa.Kinyume na hivyo changia chochote unachoona kitafanikisha huduma hizo.

  Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba:

+255715484857          (Amiri),

+255773083032   (Naibu Amiri),

+255777206206   (Mweka hazina),

+255713455069    (Uhamasishaji)